Madaktari waliofukuzwa waula Namibia, Botswana, Rwanda na A.Kusini

Kwanini daa tuwafutie ubalozi woote watakaowaiba madr wetu!
Kosa lao nini mpaka tuwafutie balozi zao?? Hivi wewe tukiwa tumesimama wote na wewe una dhahabu mkononi kisha ukaamua kuitupa nikiokota mbele yako ni kosa?? Lazima ifike mahali watanzania tuwawajibishe wanasiasa sio wao kuwa miungu kwa kuifaidi keki ya taifa lakini linapokuja swala la wataalamu ni ukandamizaji usio na kifani.
 
propaganda linafundishwa shule gani niende na mimi.....!?
"MKAPA KUGOMBEA URAIS 2015",
"MREAMA ATEULIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI"
E.T.C........ETC......ETC
 
Acha waende nazan wakipata hayo mamilion watawasaidia ndugu zao kuondoa umaskini,badala ya kugoma na kusababisha vifa kwa watanzania.
 
HESHIMA mbele kwako,

Naomba nihitilafiane nawe kidogo. Mimi naona bora nayeataka kuondoka aende tu.Itakuwa fursa nzuri kwake na familia yake ikiwa atapata green pastures kwingine.

Naamini no one is indispensable,ngoja tu-create nafasi kwa wengine wanaomaliza shule. Mwanakijiji nimeongea na baadhi ya madaktari ambao wengi ni below 35yrs na most of them hawajui hata maadili ya kazi yao.

Mmmoja aliniambia kuwa akipata nafasi katiak kulipiza aliyotendewa Ulimboka atahakikishaya kuwa watu kumi watapata umauti kupitia mikono yake.Huyu ni daktari aliyekamilika na aliyemaliza internship na kufanya kazi miaka miwili.

Hebu tueleze maadili ya kazi ni yapi?

Na kuna uhusiano gani na umri ulioutaja?.. mimi ni Resident na siku ya ulimboka kulazwa MOI kwa masikio yangu..nilisikia wakubwa wangu kikazi ( Specialists/Consultants) wanne wakisema wao wata-deal na viongozi na ndugu wa viongozi wanaofika MNH na MOI, na wakasema kama hawaamini waulize yaliyotokea kwa Blandina Nyoni(katibu mkuu wa wizara aliyesimamishwa kazi) kilichomtokea mama yake mzazi, kwani alikufa akiangaliwa tu baada ya maneno ya kejeli.

Busara tu ndio ya kutumika.
 
Mbona hadithi ni nyingi? si waende tu, walikatzwa? hapa hatuna shida na madaktari wanaogoma kutibu wagonjwa kwa sababu za kipato na marupurupu.

Kwanza wakiwa huko nchi itafaidika zaidi na fedha za kigeni watazoingiza wakizileta kujenga na kusaidia jamaa zao.

Tunawatakia kila la heri, safari njema na mishahara minono. Wapwa zangu wawili (madaktari) nao ntawaambia wafanye bidii ya kwenda huko maana nnajuwa mimi ndio wa kuwatazamia miradi yao hapa. Kwi kwi kwi teh teh teh!

Bongo Bingo.

hayo ndiyo mawazo mgando kwamba, wanarudi kusalimia familia!! Doctors wanaondok na familia zao na ndio maana uhamisho wa kwenda nje unachukua muda kwabi yakubidi kwenda kuprocess kwa familia nzima na si wewe kama daktari pekee.Fanya uchunguzi na collaboration with ur higher center mkuu.
 
hayo ndiyo mawazo mgando kwamba, wanarudi kusalimia familia!! Doctors wanaondok na familia zao na ndio maana uhamisho wa kwenda nje unachukua muda kwabi yakubidi kwenda kuprocess kwa familia nzima na si wewe kama daktari pekee.Fanya uchunguzi na collaboration with ur higher center mkuu.

Ni wapi nilipoandika "wanarudi kusalimia familia"?

Halafu utakuta eti wewe ni daktari? hata unachokisoma unachakachuwa au hukielewi tena kwa lugha nyepesi ya Taifa.
 
You can't play with professionalism....ukimnyang'anya cheti Dr hujanyang'anya uwezo ni umbumbumbu na udhaifu wa viongozi wetu...let them go hata madaktari wooooooooooooooooooote waende nashauri
 
Ni wapi nilipoandika "wanarudi kusalimia familia"?

Halafu utakuta eti wewe ni daktari? hata unachokisoma unachakachuwa au hukielewi tena kwa lugha nyepesi ya Taifa.

Kwa kukurahisishia nakuwekea hapa post yangu:

Mbona hadithi ni nyingi? si waende tu, walikatazwa? hapa hatuna shida na madaktari wanaogoma kutibu wagonjwa kwa sababu za kipato na marupurupu.

Kwanza wakiwa huko nchi itafaidika zaidi na fedha za kigeni watazoingiza wakizileta kujenga na kusaidia jamaa zao.

Tunawatakia kila la heri, safari njema na mishahara minono. Wapwa zangu wawili (madaktari) nao ntawaambia wafanye bidii ya kwenda huko maana nnajuwa mimi ndio wa kuwatazamia miradi yao hapa. Kwi kwi kwi teh teh teh!

Bongo Bingo.
 
Hivi sie watanzania tumelaaniwa? Watu tunamwomc mungu atuepushie wakati tumekaa tu maofisini bila hata kuchukua hatua. Mapinduzi halisi huletwa na fikra sahihi kutoka kwa watu maalum kama wa kwenye hii jamii forum. Tunaogopa nini kuchukua maamuzi! Madocta wameanza tunatakiwa kuwafuata nyuma kwa nguvu zote. Maandamano yasiyokoma ndo dawa pekee ya kuiondoa udharimu huu. Je tuko tayari kwa hilo! Together we can.
 
#Mkirua: hoja kuu ya ma-dr sio 7.7m..hoja yao ya msingi wanataka mazingira yao ya kazi yaboreshwe..hasa vitendea kazi. ss unapokuja kwenye jamvi la JF na kukurupuka kama sisiem na kushadadia 7.7m inanifanya nisikitike kuona kwamba bado kuna dotcom wengi ambao hamjishughulishi kupata uhalisia wa mambo yanayojiri ktk 'nji' hii!!
 
Hebu tueleze maadili ya kazi ni yapi?

Na kuna uhusiano gani na umri ulioutaja?.. mimi ni Resident na siku ya ulimboka kulazwa MOI kwa masikio yangu..nilisikia wakubwa wangu kikazi ( Specialists/Consultants) wanne wakisema wao wata-deal na viongozi na ndugu wa viongozi wanaofika MNH na MOI, na wakasema kama hawaamini waulize yaliyotokea kwa Blandina Nyoni(katibu mkuu wa wizara aliyesimamishwa kazi) kilichomtokea mama yake mzazi, kwani alikufa akiangaliwa tu baada ya maneno ya kejeli.

Busara tu ndio ya kutumika.
Nashukuru kwa confirm kuwa hamna maadili.Ikiwa daktari aliyesomea anaweza kujisifu mgonjwa asiyekuwa na hatia kufa na huku akimkejeli then huu sio udaktari ninaojua mimi.Siwezi nikatofautisha udaktari huu na al qaida mabayo iko radhi kuua watu maelfu kwa ajili ya kumsaka mmarekani mmoja.
Kuna uzi unaoendelea hapa JF ambao mdau mmojawapo ametafsri kiapo wanachoapa madaktari wakati wa kuhitimu.
Labda kipitie kiapo then uje tujadili.
 
Balozi za nchi hizo tajwa zimetoa ofa nono kwa madoctor woote waliofutiwa lesseni na wizara ya afya na TZ kwa ngazi zoote kuanzia seniors hadi intern, Intern wataandikishwa kama intern pindi wakifika kwenye nchi husika chini ya uangalizi wa Senior Doctors huku wakipewa mishahara na marupurupu yakuwatosha na wakimaliza shule wanapewa vyeti na lesseni za udoctor wa nchi walipo.

Wale masenior ambao wamenyangánywa lesseni wao wakifika wanaandikishwa kwenye chama cha madoctors wa nchi husika na kupewa lesseni mara moja na kupangiwa kazi ikiambatana na haki zoote wanazostahili.

Balozi za nchi hizi zinawaomba madocta woote wajiandikishe tayari kuajiriwa kwenye nchi watakazo kati ya hizo tajwa.
haya sasa kwa mara ingine tena TZ inaelekea kupoteza Brain zake kwa kile kinachoitwa mgomo ili hali walipa kodi wanateseka kwa kukosa watabibu.

Masini nchi yangu itatuchukua muda gani kuwapata madoctor kama hawa tena kama kweli wakiitikia mwito wa nchi hizi na wakaondoka.....?

Source: Raia Mwema Leo 18/07/2012 page 3

Yaani ni aibu sana kuona mtu anayejiita GT anapotosha habari, bila shaka kwa maslahi yake binafsi!! NI AIBU, HAKIKA NI AIBU!!!!
Ni Raia Mwema gani ulilosoma mwenzetu wewe?! Kwanini unalisha sumu watu ambao hawajapata fursa ya kuona hilo gazeti?! Ni kwa maslahi ya nani hata uamue kuongeza chumvi kiasi hiki?!
Pamoja na kuwapo kwa taarifa hiyo, lakini umeongeza chumvi mnoooo!!! Kwanza, hamna sehemu yoyote kwenye habari hiyo ambayo wamesema "Wale masenior ambao wamenyangánywa lesseni wao wakifika wanaandikishwa kwenye chama cha madoctors wa nchi husika na kupewa lesseni mara moja na kupangiwa kazi ikiambatana na haki zoote wanazostahili" Hakuna sehemu yoyote kwenye habari hiyo ambayo kuna taarifa kuhusu hao seniors....ACHA UONGO na onea aibu kitendo hicho!!! Aidha, hakuna sehemu yoyote kwenye habari hiyo ambayo imeeleza "Balozi za nchi hizi zinawaomba madocta woote wajiandikishe tayari kuajiriwa kwenye nchi watakazo kati ya hizo tajwa" na wala hamna sentensi yoyote inayobeba maana sawa na hiyo!! JISIKIE AIBU! Si hivyo tu, hakuna sehemu yoyote inayobeba ujumbe wenye maana sawa au karibu na hii "Balozi za nchi hizo tajwa zimetoa ofa nono kwa madoctor woote waliofutiwa lesseni na wizara ya afya na TZ kwa ngazi zoote kuanzia seniors hadi intern" In short, hamna sehemu hata moja iliyozungumizia suala la maslahi kwa doctors au suala la senior doctors kupewa leseni on the spot!! Sana kilicjoandikwa kwenye gazeti hilo ni hiki:

"Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, madaktari hao wamekuwa wakifanya mazungumzo na Waziri huyo katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo Dar es salaam na makubaliano ya awali yaliyofikiwa ni kwamba, madaktari hao watapokewa na kuinbgizwa katika mfumo wa mafunzo kwa vitendo(interns) na kisha kupewa leseni za nchi hizo."

"Wapo madaktari karibu 50 tayari wamekwishazungumza na WaZiri wa Afya katika moja ya nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ili waende kufanya kazi huko na kwa kweli kuna makubaliano watakwenda huko lakini wakifika wataingizwa katika mfumo wa mafunzo kwa vitendo (interns) Watakuwa chini ya uangalizi wa madaktari wengine ili hatimae kuwapa uhalali wa kitaaluma kwa kuwa na leseni ya udaktari." kilieleza chanzo chetu cha habari.

Lakini wakati hayo yakiendelea, taarifa zaidi zinaeleza nchi zingine zinazowania madaktari waliofutiwa leseni na Baraza la Madaktari Tanganyika ni pamoja na Namibia, Botswana, Lesotho, Sudan Kusin, Rwanda na Swaziland.`

Hapo kwenye BLUE ndio main content ya habari yenyewe. Nilichoacha ni introduction (inayoelezea maamuzi ya Baraza la Madaktari Taganyika la kufuta usajili wa leseni za madaktari) na taarifa nyingine niliyoacha ni hitimisho linaloeleza chanzo cha mgogoro wa madaktari!!

Sasa hayo mwenzetu wewe umeyasoma Raia Mwema la nchi gani?!
 
#Mkirua: hoja kuu ya ma-dr sio 7.7m..hoja yao ya msingi wanataka mazingira yao ya kazi yaboreshwe..hasa vitendea kazi. ss unapokuja kwenye jamvi la JF na kukurupuka kama sisiem na kushadadia 7.7m inanifanya nisikitike kuona kwamba bado kuna dotcom wengi ambao hamjishughulishi kupata uhalisia wa mambo yanayojiri ktk 'nji' hii!!

acha kuwadanganya watu wewe, hoja kuu ya madaktari ni mshahara na sio vitendea kazi. ingekuwa vitendea kazi inakuwaje hospitali za makanisa madr wa serikali nao wagome?
 
Bora waende wakafie mbele sasa kama walikuwa na hiyo option kwanini walikuwa wanagoma? si wangeacha kazi kimya kimya wakaenda huko kwenye mafano manono?

Hujambo Bwana Kituko? Hiyo option ni serikali dhaifu ambayo imefanikiwa. Sasa wewe na JK nendeni mkawatibu watanzania wagonjwa maana madaktari wa Iran hamtawapata.
 
Suala la kuchanganya siasa na profession za watu ndo Matokeo Yake haya sasa!
 
Back
Top Bottom