Madaktari Walio Katika Mafunzo MNH Wapewa Barua ya Kufukuzwa Kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Walio Katika Mafunzo MNH Wapewa Barua ya Kufukuzwa Kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2mbaku, Jan 6, 2012.

 1. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Leo asubuhi madaktari walio katika mafunzo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepewa barua ya kufukuzwa kwa madai ya kukiuka masharti ya mkataba. Barua hiyo inawataka kukabidhi funguo,kitambulisho na kuondoka haraka sana katika makazi hayo ya hospitali ya taifa ya Muhimbili. Pia barua hiyo inawataka wakaombe upya wizarani mahali pa kufanyia internship.

  Siasa hizi ndani ya uongozi wa kitengo muhimu kama hiki cha afya kinaashiria nini? Kweli afya za watanzania hazina thamani tena. Intern ndiyye muhimili mkubwa wa hospitali hiyo. Leo uwafukuze zaidi ya madaktari na watumishi wa kada zingine 200 unawatakia nini wavuja jasho wa Tanzania.

  Update:
  TUGHE nao waingilia kati kuokoa jahazi la madaktari hao. Kwa tetesi zilizopo kikao kinaendelea wizarani mpaka sasa hivi. Sijui kuna posho zitakazotolewa huko?

  Hali yazidi kuwa tete Dodoma

  Huko Dodoma, madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wameendelea na msimamo wa kutofanya kazi hadi watakapolipwa fedha zao huku utoaji wa huduma kwa wagonjwa ukiendelea kudorora.

  Mgomo huo wa madaktari ambao ulianza juzi asubuhi umesababisha wagonjwa wengi waliolazwa na wale wanaofika hospitalini hapo kukosa huduma zinazostahili.

  Madaktari hao wamegoma wakishinikiza Wizara ya Afya iwalipe fedha zao za miezi miwili wanazodai.

  Zaidi ya madaktari 33 wanaidai wizara hiyo malipo ya fedha kuanzia mwezi Novemba na Desemba mwaka jana ambazo hawajalipwa hadi leo.

  Hata hivyo, kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa, Dk. Nassoro Mzee, alisema malipo ya madaktari hao yanashughulikiwa baada ya fedha kufikishwa Hazina ndogo ya Dodoma.

  "Fedha zimeshafika na zipo kwenye utaratibu wa malipo, naamini hadi Jumatatu madaktari wote watakuwa wamelipwa fedha zao," alisema.

  Hata hivyo, katibu wa hospitali hiyo, Isaack Kaneno, alisema madaktari hao wamekataa kuingia kazini hadi wapate fedha mkononi, licha ya kuambiwa kuwa ziko Hazina na zinashughulikiwa.

  "Inasikitisha kwamba wenyewe wanadai mwezi mmoja na hapohapo kuna watumishi wengine wa serikali wanadai miezi mingi, mbona hawajagoma?" alisema.

  Hata hivyo, katibu mkuu alisema kwa mujibu wa taratibbu za kazi, mfanyakazi akigoma kwa siku tatu mfululizo atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.

  Tanzania Daima ilipomtafuta Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Blandina Nyoni, kuzungumzia suala hilo simu yake iliita mara zote alipopigiwa bila majibu.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jana waziri si alisema wamepewa pesa kumbe si pesa bali barua za kufukuzwa!
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  muarobaini wa hili tatizo ni lowasa 2015
   
 4. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jana wamelipwa pesa zao, leo wamepewa barua za kufukuzwa
   
 5. m

  msafi Senior Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tena watarudi kwa masharti kama ni hapohapo mnh au hospitali zingine, watatakiwa kurudia upya internship yao hata kama watakuwa wamebakiza wiki moja, wataanza moja na hawatalipwa mshahara, bali watafanya internship kwa gharama zao.
   
 6. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunaomba Medical Association of Tanzania waingilie kati na kuitisha mgomo wa madaktari nchi nzima haraka sana.
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Siasa kazini.............. Anaongea leo kutuliza mambo...... kesho atakuja na jibu jingine!!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hatutaki tena kiongozi mwizi.
   
 9. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Inchi ikitawaliwa na semi illiterates siku zote haithamini taaluma.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mbona adhabu hii ni kali mno kwa hao vijana? Si nasikia Tanzania tuna upungufu wa madaktari.
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi mbona wabunge wakidai posho wanaongezwa na hawafukuzwi, ninawaomba madaktari wote waungane katika hili ili wote watimuliwe walete wachina. Sisi tutaenda kutibiwa kwa babu Loliondo. Hii nchi JK imemshinda sasa amekalia ubabe tu
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  halafu yatalalamika hakuna madr wakati sahivi wanawazingua...
  RIP tz
   
 13. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280

  Yale yale tunayolia nayo kila siku ya kuingiza siasa kwenye kila issue......hapa Lowasa anaingiaje sasa???yaani unaonyesha huna tofauti kimawazo na yale yanayofanywa na status quo....madaktari wamegoma ili kudai haki yao sasa wanafukuzwa......nini kifanyike kwenye hali hii ndicho kinatakiwa na si bla bla za Lowasa 2015.....yaani matatizo ya madaktari leo Jan/2012 yatatuliwe na Lowasa 2015??where is the logic my brother?we need solutions now.......

  As for the intern Drs.....kama kweli hii taarifa ni ya kweli.....basi ni kuwa na piece tu.....haya yanafanywa kila leo kwa wanfunzi wetu vyuoni tunaona na tumezoea....ushauri tu..kuweni kitu kimoja kwenye maamuzi na pia i hope MAT watatoa tamko ASAP ili kuweza kuwalinda interns....mara nyingi nimewahi kuona hali hii itokeapo kuna ma Dr wengi huathirika....i remember 2006...mgomo wa madaktari uliathiri wengi na ni kwa kuwa MAT hawakujitoa ipasavyo kuwalinda....nadhani ifike mahali sasa MAT wahamasishe madaktari woote kwenye hizi referral hospitals wagome ili interns wote warudishwe tena bila masharti haraka kazini(kwani waligomea haki yao kama last resort).

  Tena madaktari wasiwe na wasiwasi wawe tu kitu kimoja(wasisalitiane)....maana wanahitajika na serikali lazima watawarudisha kama MAT wakitoa tamko na kulisimamia.........ifike mahali tz watu waache siasa makazini jamani.....anayeathirika siku zote kwenye haya maamuzi ya serikali yasiyo na msingi ni raia wa kawaida.....interns wanaweza kufanyia popote...kuna kcmc,bugando,mount meru, seliani,IMTU,hata aghakan etc etc......ni muda tu watapoteza..its not a big deal(as far as they are deeply needed in the country)...hii fani ya udaktari si siasa jamani...
   
 14. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  inasikitisha sana aisee
   
 15. m

  mhondo JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wenyewe wakiumwa wanaenda kutibiwa India kwahiyo hawana wasiwasi hata wakifukuzwa.
   
 16. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hivyo viposho wanavyolipwa vinaweza kuwapeleka India kweli? Mwezi m1 tu hawakulipwa mgomo huo!!! Sasa watapata wapi fedha za kuwapeleka India?
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Kama unampenda sana Lowasa kanywe nae chai au gahawa. Hatuwezi kukubali kuongozwa na mwizi tena!
   
 18. T

  Technology JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  wao madenti na bado wanaleta siasa kazini!!!!! let them go to hell.
   
 19. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tofautisha kati ya intern na medical student. Uliza uelimishwe. Tahira wee. Nenda shule.
   
 20. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hatuna serikali bali tuna genge la wabakaji haki za wananchi. kumbe kudai haki yako ni kosa?
   
Loading...