Madaktari Waitishe Mgomo usiokoma kudai maslahi! Simameni Pamoja!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Lula wa Ndali Mwananzela (RAIA MWEMA)

Msiposimama pamoja, mtaangamia mmoja mmoja

TUKIO la hivi karibuni la Serikali kuamua kuwafukuza madaktari wanafunzi waliokuwa wanadai mafao yao mbalimbali na nyongeza za mafao hayo, linahitaji kulaaniwa na kuoneshwa kuwa ni la kibabe. Madaktari wa Tanzania yawezekana ndio madaktari wanaofanya kazi katika mazingira mabovu zaidi wakitarajiwa kuhudumia maisha ya wananchi huku wanasiasa wa nchini wakiishi maisha ya juu zaidi, wakijiaminisha kuwa wanastahili zaidi! Tujadili suala hili katika maeneo mahsusi kama ifuatavyo.

Tiba nchini India
Mojawapo ya vitu ambavyo vinaonesha dharau na kukosekana kwa heshima ya hadhi ya madaktari wetu ni hili la kupeleka wagonjwa India, kwa matibabu ambayo yangeweza kufanyika hapa nchini. Niliandika juu ya hili miezi michache iliyopita lakini yafaa nirudie.

Ningependa kujua kama viongozi serikalini wamewahi kukaa chini na kujiuliza swali jepesi (wengine wanaweza kuliita la kizushi) la ni kwa nini tunapeleka wagonjwa India na siyo kutibiwa hapa hapa nchini? Jibu la swali hili lina pande mbili – upande wa kwanza wapo wanaodai kuwa gharama ya kutibiwa India ni nafuu zaidi kuliko nchini. Sijui kama kuna ukweli wa hili na ni nani aliyewahi kufanya utafiti wa kupima hili. Ni kweli gharama ya nauli ya ndege kwenda na kurudi, chakula na malazi na mapumziko huko India ni ndogo kuliko kutibiwa hapa nchini?

Binafsi sitaki sana kuamini hili kwa sababu gharama inasababishwa na vitu mbalimbali, je, Serikali yetu imeshindwa kabisa kufikiria namna ya kufanya gharama ya afya kuwa nafuu hapa nchini? Na ni kitu gani kinafanya gharama iwe juu Tanzania ambacho hakiwezi kuangaliwa na kushughulikiwa? Upande wa pili ni lile linalodaiwa ni ubora wa madaktari wa India. Wapo ambao wanaamini kuwa India ina madaktari wenye ujuzi mkubwa kuliko madaktari wetu. Watu wengi hawajui kuwa daktari wa Tanzania ili awe daktari kamili, anasomea kwa miaka saba wakati yule wa India anasomea miaka 5!

Madaktari wa Marekani nao wanasomea miaka saba! Na nchi nyingine zina tofauti ya kati ya miaka mitano hadi saba, huku hadi kuwa Bingwa inakuwa ni miaka karibu tisa ya mafunzo. Sasa ubora wa madaktari wa India unatokana na nini ambacho Tanzania haiwezi kukifanya? Binafsi ningependa sana kuona chombo huru au taasisi huru kama walivyofanya watu wa taasisi za HakiElimu au Tunaweza, kwenye masuala ya elimu kupitia na kufanya ulinganifu wa madaktari wetu kulinganisha na India.

Nadharia yangu ni kuwa karibu vitu vyote vinavyofanywa India vinaweza kabisa kufanywa Tanzania. Watu wanapenda kwenda India kwa sababu zaidi ni hisia ya kuwa wanaenda “nje” kutibiwa. Lakini nyuma ya hili ninaamini kuna hisia kuwa madaktari wa Tanzania hawaaminiki. Kuwa hawana uwezo – japo wanaweza kuwa wamesoma vizuri na hata kuzidi wale wa India na vile vile kuwa kutokana na maslahi yao duni hujikuta wakiendekeza taasisi zao binafsi zaidi kuliko kufanya kazi kwa weledi katika taasisi za ajira zao.

Hili la mwisho laweza kuwa na ukweli zaidi kwani wapo watu ambao wamewahi kujikuta wanaambiwa waende hospitali ya dokta kwa uangalizi zaidi. Lakini kwenye nchi ambayo maslahi ya daktari ni duni sana, daktari huyo afanye nini zaidi ya kujipatia kipato chake cha ziada pembeni? Namfahamu Daktari mmoja (sasa Marehemu) ambaye alisomeshwa na fedha za Watanzania lakini baada ya kujitahidi kujitolea sana kufanya kazi ya udaktari aliona kuwa hailipi na matokeo yake alianzisha biashara yake ya baa na maduka na hadi anafariki, alikuwa ni Daktari wa cheo tu akikataa kabisa kurudi hospitali kutoa huduma. Wapo madaktari ambao udaktari ni sehemu tu ya kazi zao lakini wanapotengeneza fedha zaidi ni kwenye miradi yao mbalimbali.

Kutoboresha maslahi yao ni kejeli kwa utu wetu
Ndugu zangu, ni kweli walimu ni muhimu (sitaki kuingia mjadala wa ‘nani bora kati ya daktari na mwalimu’) lakini katika kujenga taifa la kisasa na lenye watu wenye afya bora hakuna nafasi ya pekee kama ya madaktari. Ni wao ndio wanatupa nafasi ya kuishi na kutumikia taifa tukiwa na afya bora zaidi. Ni watu ambao kutokana na ujuzi wa kazi zao na vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu hujikuta wakiokoa maisha yetu (iwe katika ajali, magonjwa au dharura fulani).

Ni watu muhimu sana kiasi kwamba katika Wagiriki na Wayahudi wa kale uponyaji ulikuwa ni sifa ya kimungu. Waebrania walimuita Mungu Yehova Rapha (yaani Bwana Anayeponya) wakati Wagiriki walikuwa na mungu aitwaye Askelpias ambaye alikuwa ni mungu wa tiba na uponyaji. Kati ya mabinti zake mmoja aliitwa Hygeia (tunapata neno la Kiingereza Hygiene – usafi) na Panacea yaani “tiba ya magonjwa yote”. Ile fimbo yenye nyoka hujulikana kama fimbo ya Asklepias. Hivyo basi, madaktari si watu wa kudharauliwa au kufanywa duni.

Serikali inawaafanya madaktari wetu duni
Sizungumzii suala la kufukuzwa kwa hawa madaktari wanafunzi tu, nazungumzia jinsi tunavyowaangalia madaktari na kuwatendea. Ni kweli hatuwezi kuwalipa sana lakini ukweli ni kuwa kutokana na idadi yao, madaktari wanastahili kulipwa zaidi kwa ajili ya kuwavutia zaidi lakini vile vile kuwafanya wafanye kazi yao ambayo ni wito wao kwa kweli. Unajua watu wengi hatuna wito wa kukaa na kufumua miili ya wanadamu, kuona uchafu wao na madamu yao na kuwapo pale kuwasaidia kurudi kwenye uzima au kuwasaidia wanapoelekea mauti. Ni wito wa ajabu sana ambao tusipoonekana kuuelewa tutaona kama “ajira nyingine tu”.

Daktari wa Tanzania anayeingia kwenye ajira tu asingelipwa chini ya mshahara wa kama dola 5,000 hivi kwa mwezi pamoja na mafao mengine. Ni lazima tumtoe huyu daktari kutoka kwenye miradi yake ya nyumbani na vibarua na kumhakikishia usalama wa maisha yake. Hatuwezi kuwa na madaktari ambao ili wawahi hospitali kutoa huduma inabidi wadandie daladala au kununua gari mkweche. Haiwezekani leo tunajenga majumba ya wanasiasa lakini hatujawa na programu ya uhakika ya kuwajengea madaktari wetu nyumba za kudumu.

Hivi katika miradi yote ya Jiji la Dar es Salaam ni wapi wana mpango wa kujenga nyumba za makazi kwa madaktari? Huko mikoani ni wapi ambapo wana miradi ya kujenga nyumba za madaktari karibu na hospitali au kwenye maeneo ya kisasa ambayo yatawapa nafasi ya kupumzika na kutulia na kujifunza kabla hawajarudi kukimbia kuokoa maisha ya wananchi wetu?

Hivi watu wamewahi kujiuliza kuwa Tanzania ina madaktari wangapi? Katika Tanzania yetu hii ambayo watu wanaamini ina neema tuna daktari mmoja kwa kila watu kama 30,000 hivi. Marekani ina dokta mmoja karibu kwa kila watu 400 hivi. Sasa kweli tunaweza hata kufikiria kusimamisha madaktari wanafunzi zaidi ya 200 kwa sababu za kipuuzi – kwamba wamedai kuboreshewa maslahi yao? Kweli? Ni taifa gani ambalo tunajenga?

Yaani, wanasiasa wanaweza kujiongezea posho bila kuhojiwa na yeyote tena kwa asilimia zaidi ya 300, lakini hawa madaktari wetu hata ‘kiduchu’ wanachodai imekuwa ni nongwa? Hivi, kuna mwanasiasa wa CCM anayeweza kusimama na kutuambia akiwa na macho makavu kuwa madaktari wa Tanzania wanalipwa vizuri na mazingira yao ni bora?

Huyu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa CCM) aliyedai kuwa wamejiongezea posho kwa sababu maisha ni magumu Dodoma alikuwa hafikirii kuwa huko Dodoma nako kuna madokta? Nani atawapigania madaktari wetu?
Naomba nitoe taarifa mbaya - madaktari wa Tanzania hawatopiganiwa na wanasiasa wetu! Wanajidanganya wale madaktari waliokaa Wizara ya Afya na ambao wanaishi maisha ya furaha kwa sababu wanakula na wakubwa! Hawa madaktari waliotupwa porini huko Katavi, Bukoba, Mbeya na sehemu nyingine waishi kwa kuombea kudura (kudra) tu! Hawana mtetezi. Na bahati mbaya sana hata vyama vyao haviwezi kuwatetea.

Kuna wakati, madaktari lazima wasimamie maslahi yao kwani kwa kufanya hivyo watasimamia maslahi ya wagonjwa wao na wale watumishi wa afya wa kada nyingine. Na kuna namna moja tu ambayo italazimisha watawala wetu kuangalia maslahi ya madaktari na kuwarudisha mara moja wale wanafunzi na kuhakikisha kuwa madaktari wa Tanzania wanapewa heshima na hadhi wanayostahili – mgomo.

Mimi si shabiki wa migomo ya aina hii lakini tulipofika sasa inaonekana hoja hazitoshi kuwashawishi watawala kufikiri. Mgomo siyo wa kukataa tu bali pia wa kudai kile kinachowezekana.

Kama taifa linaweza kutenga posho ya karibu bilioni 28 kwa watu 350 hivi na wakahalalisha inawezekana, nina uhakika taifa hilo hilo lina uwezo wa kutenga kiasi kikubwa tu cha fedha kuboresha mishahara na posho za madaktari karibu 2,000 tu ambao tunao!
Mgomo ni njia pekee na sahihi ya kutuma ujumbe wa kisiasa ambao umeshindikana kupokewa kwa njia za kidemokrasia na mazungumzo. Mazungumzo yamefanywa miaka nenda rudi lakini bado watawala wetu wanaona kama wanasumbuliwa na ‘madai’ ya madaktari.

Nasema madaktari hamna cha kupoteza isipokuwa utu wenu na hadhi yenu kama waponyaji. Mtaendelea kudharauliwa, kunyanyasika na kudhulumiwa huku na ninyi mkitamani muwe wanasiasa! Si mmewaona madaktari wenzenu walivyoingia siasa wanavyonona. Hamna mtetezi wala wa kuwapigania isipokuwa ninyi wenyewe! Tangazeni mgomo na simameni pamoja mtasikilizwa. Msiposimama pamoja, mtaangamia mmoja mmoja!
 
Baada ya hapo mgomo uhamie kwa walimu, kisha manesi na baadaye wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wanafanya kazi kama vibarua kwa zaidi ya miaka 10.
Lakini zaidi ya asilimia 70 ya nguvu kazi ya TZ ni wakulima, na wao wana matatizo makubwa zaidi ya madaktari , wao watagomaje?
Labda mgomo wa madaktari utakua kichocheo cha mabadiliko ya kweli kwa wote.
 
naunga hoja mkono na sisi wananchi hatuna cha kupoteza dr JK atatutibu kwa kuleta madkari wa china na uarabuni.... Still loading.....
 
Hivi, Tanzania ina madaktari wangapi ambao wanatoa huduma ya kuangalia binadamu (Full MD siyo Medical Assistants au Medical Officers)? Na kati ya hao ni wangapi HAWAKO Dar-es-Salaam wako mikoani?
 
Niliuliza huko nyuma kuwa ni vitu gani vinaangaliwa kabla ya kumuita mtu 'dakatri bingwa? Na nani anasema huyu ni daktari bingwa? Tanzania tumechoka kusikia daktari bingwa lakini watu wanakwenda India kwa "uchunguzi wa kawaida".
 
naunga hoja mkono na sisi wananchi hatuna cha kupoteza dr JK atatutibu kwa kuleta madkari wa china na uarabuni.... Still loading.....

mkuu wangu madaktari wakigoma sisi wananchi ndio tunapoteza kwa sababu sisi ndio tunaoumwa. Tuombe Mungu serikali isikie kilio chao ili wapewe mahitaji yao..wabunge wamesgajipandishia chao kinyemela kisa dodoma maisha ni magumu dodoma labda hakuna madaktari
 
hili suala la watu kupelekwa india sijui ni kwa nini..mbona wanafunzi wa kitz wanaosoma nchi za nje/wakiwa masomoni nchi za nje ni vichwa sana tu na wanawaburuzaga hadi hao wahindi wenyewe sasa tatizo sijui ni nini labda wakirudigi Tanzania wakivuta hewa ya tz akili zao hudumaa? Au hawana vifaa? Au hao wenye kukata maamuzi ya kupeleka watu india hawana exposure?
 
Hiki ndio kisingizio pekee cha kwanini maslahi ya madaktari hayaboreshwi. Think about it.
 
wagome au kama vipi waje tupige box tu,wawaachie nchi yao,kwani kitu gani bwana
 
Hivi, Tanzania ina madaktari wangapi ambao wanatoa huduma ya kuangalia binadamu (Full MD siyo Medical Assistants au Medical Officers)? Na kati ya hao ni wangapi HAWAKO Dar-es-Salaam wako mikoani?

Mkuu naona umechanganya hapo,wenye fani yao watakuja kunisahihisha na mimi.Nadhani medical officers ndiyo MD,na wengine ndiyo hao medical assistants na clinical officers kama sikosei
 
Nadhani katka i tutajiwe tujulishwe na tueleweshwe pia ni
  • Magonjwa gani ambayo hayatibkii hapa Tanzania na yapi yanatibika
  • Kwa mwaka taifa linatumia wastani wa shilingi ngapi kwa matibabu ya nje ya viongozi upande mmoja na wanachi upande mwingine..
 
Hapo kwenye Mgomo!
Hicho ni kikwazo namba moja kwa raia yeyote wa dunia hii anaetambulika kama MTANZANIA!
Mtanzania yeyote ukimwekea haki yake upande wa pili na hapo kati ukaweka kikwazo kuwa "MGOMO (GOMA)" ndio upite upande wa haki yake basi huo ndio utakuwa mwisho MTANZANIA kuifuata hyo haki yake!
Sikumbuki kama tunahistoria ya kujivunia hasa katika suala la MIGOMO hasa kwenye masuala makubwa ya kitaifa kama hili (nimelichukulia sakata hili la madaktari kama suala kuu la kitaifa kama ulivyoliwasilisha)??
Tuna tatizo kwenye idara ya "WATU WETU" sitashangaa hili likapita kama kawaida, kama lilivyopita la KATIBA....
Nimetaja KATIBA! Hivi kuna suala la muhimu kupita katiba? Ila tujikumbushe hapa kwetu tulivyoliacha likashughulikiwa kimauzauza!
Sitaki kutoa mfano mwingine, nashuhudia vioja vya kutosha katika nchi hii yangu.
Hao ma-dk waliofukuzwa waangalie ustaarabu wa kwenda nchi zinazowahitaji....
 
hili suala la watu kupelekwa india sijui ni kwa nini..mbona wanafunzi wa kitz wanaosoma nchi za nje/wakiwa masomoni nchi za nje ni vichwa sana tu na wanawaburuzaga hadi hao wahindi wenyewe sasa tatizo sijui ni nini labda wakirudigi Tanzania wakivuta hewa ya tz akili zao hudumaa? Au hawana vifaa? Au hao wenye kukata maamuzi ya kupeleka watu india hawana exposure?

..Suala la wagonjwa wa Tazania kupelekwa India ni biashara. Kwa kila mgonjwa mmoja anayepelekwa India kuna watu wanapewa commission hata hao Lions Club sio wasafi..watu wanapewa hela Kuanzia wizara ya Afya, Lions Cub etc..Ukimsikiliza vizuri Dr. Massao (yule mwenye hospitali ya upasuaji wa Moyo Tz, utaelewa mgogoro wake na Wizara ya Afya). Pale India kwenye ubalozi wetu, kuna daktari ubalozini ambaye kazi yake ni ku coordinate hizi safari .Hata hii move ya Hospitali ya Appollo ya India kufungua tawi hapa Tz ni katika kuhakikisha kuwa hata Tz ikiamua kutopeleka wagonjwa India basi waishie katika hospitali ya "Wahindi"hapa Tz. Hebu fikiria, Tanzania ambayo imeshapeleka wataalamu kibao kujifunza upasuaji wa moyo na gharama iliyoingia kuazisha kitengo Muhimbili inashabikiaje kuanzishwa kwa kitengo kingine?
 
Niliuliza huko nyuma kuwa ni vitu gani vinaangaliwa kabla ya kumuita mtu 'dakatri bingwa? Na nani anasema huyu ni daktari bingwa? Tanzania tumechoka kusikia daktari bingwa lakini watu wanakwenda India kwa "uchunguzi wa kawaida".

Tuna tatizo la ukosefu wa vifaa hasa vya uchunguzi (Diagnostics) pia kuna fani ambazo hatuna wataalamu, sio kwa sababu waTZ hawana uwezo wa kusomea lakini ni kuwa hata wakisoma kwa kuwa hakuna facilities hawataweza kufanya kazi hapa TZ..Chukulia mf; mtu asomee upasuaji wa mishipa ya damu (Vascular surgery). Dakatai bingwa ni yule ambaye baada ya kusoma degree ya kwanza anasoma tena masters kwa miaka 3-4 na kuwa binga katika eneo fulani mf: watoto, Upasuaji, Macho nk...pia wengine hsoma tena kwa miaka 3 na kuwa super speacilists mf daktari bingwa upasuaji wa mishipa ya fahamu (Neuro surgeons)

Nadhani nimekusaidia
 
Lula wa Ndali Mwananzela (RAIA MWEMA)

Msiposimama pamoja, mtaangamia mmoja mmoja

TUKIO la hivi karibuni la Serikali kuamua kuwafukuza madaktari wanafunzi waliokuwa wanadai mafao yao mbalimbali na nyongeza za mafao hayo, linahitaji kulaaniwa na kuoneshwa kuwa ni la kibabe. Madaktari wa Tanzania yawezekana ndio madaktari wanaofanya kazi katika mazingira mabovu zaidi wakitarajiwa kuhudumia maisha ya wananchi huku wanasiasa wa nchini wakiishi maisha ya juu zaidi, wakijiaminisha kuwa wanastahili zaidi! Tujadili suala hili katika maeneo mahsusi kama ifuatavyo.

Tiba nchini India
Mojawapo ya vitu ambavyo vinaonesha dharau na kukosekana kwa heshima ya hadhi ya madaktari wetu ni hili la kupeleka wagonjwa India, kwa matibabu ambayo yangeweza kufanyika hapa nchini. Niliandika juu ya hili miezi michache iliyopita lakini yafaa nirudie.

Ningependa kujua kama viongozi serikalini wamewahi kukaa chini na kujiuliza swali jepesi (wengine wanaweza kuliita la kizushi) la ni kwa nini tunapeleka wagonjwa India na siyo kutibiwa hapa hapa nchini? Jibu la swali hili lina pande mbili – upande wa kwanza wapo wanaodai kuwa gharama ya kutibiwa India ni nafuu zaidi kuliko nchini. Sijui kama kuna ukweli wa hili na ni nani aliyewahi kufanya utafiti wa kupima hili. Ni kweli gharama ya nauli ya ndege kwenda na kurudi, chakula na malazi na mapumziko huko India ni ndogo kuliko kutibiwa hapa nchini?

Binafsi sitaki sana kuamini hili kwa sababu gharama inasababishwa na vitu mbalimbali, je, Serikali yetu imeshindwa kabisa kufikiria namna ya kufanya gharama ya afya kuwa nafuu hapa nchini? Na ni kitu gani kinafanya gharama iwe juu Tanzania ambacho hakiwezi kuangaliwa na kushughulikiwa? Upande wa pili ni lile linalodaiwa ni ubora wa madaktari wa India. Wapo ambao wanaamini kuwa India ina madaktari wenye ujuzi mkubwa kuliko madaktari wetu. Watu wengi hawajui kuwa daktari wa Tanzania ili awe daktari kamili, anasomea kwa miaka saba wakati yule wa India anasomea miaka 5!

Madaktari wa Marekani nao wanasomea miaka saba! Na nchi nyingine zina tofauti ya kati ya miaka mitano hadi saba, huku hadi kuwa Bingwa inakuwa ni miaka karibu tisa ya mafunzo. Sasa ubora wa madaktari wa India unatokana na nini ambacho Tanzania haiwezi kukifanya? Binafsi ningependa sana kuona chombo huru au taasisi huru kama walivyofanya watu wa taasisi za HakiElimu au Tunaweza, kwenye masuala ya elimu kupitia na kufanya ulinganifu wa madaktari wetu kulinganisha na India.

Nadharia yangu ni kuwa karibu vitu vyote vinavyofanywa India vinaweza kabisa kufanywa Tanzania. Watu wanapenda kwenda India kwa sababu zaidi ni hisia ya kuwa wanaenda "nje" kutibiwa. Lakini nyuma ya hili ninaamini kuna hisia kuwa madaktari wa Tanzania hawaaminiki. Kuwa hawana uwezo – japo wanaweza kuwa wamesoma vizuri na hata kuzidi wale wa India na vile vile kuwa kutokana na maslahi yao duni hujikuta wakiendekeza taasisi zao binafsi zaidi kuliko kufanya kazi kwa weledi katika taasisi za ajira zao.

Hili la mwisho laweza kuwa na ukweli zaidi kwani wapo watu ambao wamewahi kujikuta wanaambiwa waende hospitali ya dokta kwa uangalizi zaidi. Lakini kwenye nchi ambayo maslahi ya daktari ni duni sana, daktari huyo afanye nini zaidi ya kujipatia kipato chake cha ziada pembeni? Namfahamu Daktari mmoja (sasa Marehemu) ambaye alisomeshwa na fedha za Watanzania lakini baada ya kujitahidi kujitolea sana kufanya kazi ya udaktari aliona kuwa hailipi na matokeo yake alianzisha biashara yake ya baa na maduka na hadi anafariki, alikuwa ni Daktari wa cheo tu akikataa kabisa kurudi hospitali kutoa huduma. Wapo madaktari ambao udaktari ni sehemu tu ya kazi zao lakini wanapotengeneza fedha zaidi ni kwenye miradi yao mbalimbali.

Kutoboresha maslahi yao ni kejeli kwa utu wetu
Ndugu zangu, ni kweli walimu ni muhimu (sitaki kuingia mjadala wa ‘nani bora kati ya daktari na mwalimu') lakini katika kujenga taifa la kisasa na lenye watu wenye afya bora hakuna nafasi ya pekee kama ya madaktari. Ni wao ndio wanatupa nafasi ya kuishi na kutumikia taifa tukiwa na afya bora zaidi. Ni watu ambao kutokana na ujuzi wa kazi zao na vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu hujikuta wakiokoa maisha yetu (iwe katika ajali, magonjwa au dharura fulani).

Ni watu muhimu sana kiasi kwamba katika Wagiriki na Wayahudi wa kale uponyaji ulikuwa ni sifa ya kimungu. Waebrania walimuita Mungu Yehova Rapha (yaani Bwana Anayeponya) wakati Wagiriki walikuwa na mungu aitwaye Askelpias ambaye alikuwa ni mungu wa tiba na uponyaji. Kati ya mabinti zake mmoja aliitwa Hygeia (tunapata neno la Kiingereza Hygiene – usafi) na Panacea yaani "tiba ya magonjwa yote". Ile fimbo yenye nyoka hujulikana kama fimbo ya Asklepias. Hivyo basi, madaktari si watu wa kudharauliwa au kufanywa duni.

Serikali inawaafanya madaktari wetu duni
Sizungumzii suala la kufukuzwa kwa hawa madaktari wanafunzi tu, nazungumzia jinsi tunavyowaangalia madaktari na kuwatendea. Ni kweli hatuwezi kuwalipa sana lakini ukweli ni kuwa kutokana na idadi yao, madaktari wanastahili kulipwa zaidi kwa ajili ya kuwavutia zaidi lakini vile vile kuwafanya wafanye kazi yao ambayo ni wito wao kwa kweli. Unajua watu wengi hatuna wito wa kukaa na kufumua miili ya wanadamu, kuona uchafu wao na madamu yao na kuwapo pale kuwasaidia kurudi kwenye uzima au kuwasaidia wanapoelekea mauti. Ni wito wa ajabu sana ambao tusipoonekana kuuelewa tutaona kama "ajira nyingine tu".

Daktari wa Tanzania anayeingia kwenye ajira tu asingelipwa chini ya mshahara wa kama dola 5,000 hivi kwa mwezi pamoja na mafao mengine. Ni lazima tumtoe huyu daktari kutoka kwenye miradi yake ya nyumbani na vibarua na kumhakikishia usalama wa maisha yake. Hatuwezi kuwa na madaktari ambao ili wawahi hospitali kutoa huduma inabidi wadandie daladala au kununua gari mkweche. Haiwezekani leo tunajenga majumba ya wanasiasa lakini hatujawa na programu ya uhakika ya kuwajengea madaktari wetu nyumba za kudumu.

Hivi katika miradi yote ya Jiji la Dar es Salaam ni wapi wana mpango wa kujenga nyumba za makazi kwa madaktari? Huko mikoani ni wapi ambapo wana miradi ya kujenga nyumba za madaktari karibu na hospitali au kwenye maeneo ya kisasa ambayo yatawapa nafasi ya kupumzika na kutulia na kujifunza kabla hawajarudi kukimbia kuokoa maisha ya wananchi wetu?

Hivi watu wamewahi kujiuliza kuwa Tanzania ina madaktari wangapi? Katika Tanzania yetu hii ambayo watu wanaamini ina neema tuna daktari mmoja kwa kila watu kama 30,000 hivi. Marekani ina dokta mmoja karibu kwa kila watu 400 hivi. Sasa kweli tunaweza hata kufikiria kusimamisha madaktari wanafunzi zaidi ya 200 kwa sababu za kipuuzi – kwamba wamedai kuboreshewa maslahi yao? Kweli? Ni taifa gani ambalo tunajenga?

Yaani, wanasiasa wanaweza kujiongezea posho bila kuhojiwa na yeyote tena kwa asilimia zaidi ya 300, lakini hawa madaktari wetu hata ‘kiduchu' wanachodai imekuwa ni nongwa? Hivi, kuna mwanasiasa wa CCM anayeweza kusimama na kutuambia akiwa na macho makavu kuwa madaktari wa Tanzania wanalipwa vizuri na mazingira yao ni bora?

Huyu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa CCM) aliyedai kuwa wamejiongezea posho kwa sababu maisha ni magumu Dodoma alikuwa hafikirii kuwa huko Dodoma nako kuna madokta? Nani atawapigania madaktari wetu?
Naomba nitoe taarifa mbaya - madaktari wa Tanzania hawatopiganiwa na wanasiasa wetu! Wanajidanganya wale madaktari waliokaa Wizara ya Afya na ambao wanaishi maisha ya furaha kwa sababu wanakula na wakubwa! Hawa madaktari waliotupwa porini huko Katavi, Bukoba, Mbeya na sehemu nyingine waishi kwa kuombea kudura (kudra) tu! Hawana mtetezi. Na bahati mbaya sana hata vyama vyao haviwezi kuwatetea.

Kuna wakati, madaktari lazima wasimamie maslahi yao kwani kwa kufanya hivyo watasimamia maslahi ya wagonjwa wao na wale watumishi wa afya wa kada nyingine. Na kuna namna moja tu ambayo italazimisha watawala wetu kuangalia maslahi ya madaktari na kuwarudisha mara moja wale wanafunzi na kuhakikisha kuwa madaktari wa Tanzania wanapewa heshima na hadhi wanayostahili – mgomo.

Mimi si shabiki wa migomo ya aina hii lakini tulipofika sasa inaonekana hoja hazitoshi kuwashawishi watawala kufikiri. Mgomo siyo wa kukataa tu bali pia wa kudai kile kinachowezekana.

Kama taifa linaweza kutenga posho ya karibu bilioni 28 kwa watu 350 hivi na wakahalalisha inawezekana, nina uhakika taifa hilo hilo lina uwezo wa kutenga kiasi kikubwa tu cha fedha kuboresha mishahara na posho za madaktari karibu 2,000 tu ambao tunao!
Mgomo ni njia pekee na sahihi ya kutuma ujumbe wa kisiasa ambao umeshindikana kupokewa kwa njia za kidemokrasia na mazungumzo. Mazungumzo yamefanywa miaka nenda rudi lakini bado watawala wetu wanaona kama wanasumbuliwa na ‘madai' ya madaktari.

Nasema madaktari hamna cha kupoteza isipokuwa utu wenu na hadhi yenu kama waponyaji. Mtaendelea kudharauliwa, kunyanyasika na kudhulumiwa huku na ninyi mkitamani muwe wanasiasa! Si mmewaona madaktari wenzenu walivyoingia siasa wanavyonona. Hamna mtetezi wala wa kuwapigania isipokuwa ninyi wenyewe! Tangazeni mgomo na simameni pamoja mtasikilizwa. Msiposimama pamoja, mtaangamia mmoja mmoja!

Nimefurahishwa na makala yako umefanya kazi nzuri ku highlight mambo ya muhimu na umechukua muda kuyaelewa matatizo ya madaktari wa Tanzania. Nitoe mchango mdogo.....Madaktari wa Tz wanafanya kazi katika mazingira magumu mno (natambua kuwa wafanyakazi wote wa umma wanafanya kazi katika mazingira magumu Tz) Hebu tazama mifano hii: Mosi,daktari anapokuwa kazini pamoja na kumtibu mgonjwa lakini yeye pia anakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kama TB, VVU/UKIMWI, Hepatitis nk haya ni magonjwa yanayoleta kifo! Katika hospitali zetu nyingi hakuna vitendea kazi vya kutosha kumkinga daktari/na wauguzzi dhidi ya hatari hizi. Madaktari wanalowa damu kila siku katika kuokoa maisha ya watu (kwa kipindi cha UKIMWI) hii ni hatari kubwa! Hakuna miwani mikubwa kuzuia damu kuwarukia machoni madaktari wakati wa upasuaji(kama zipo ni muhimbili na katika miji mikubwa hapa Tz) nina experience ya kuzamisha mkono katika uke wa wa mama aliyejifungua huku nikiwa nimevaa glovu inayoishia katika kiganja cha mkono ilihali mkono wangu ulizama hadi kwa kufika katika kiwiko (watawala wanakuambia hakuna glovu ndefu) ukifikiria sana unajiona mjinga kwa kujiweka katika risk ya UKIMWI nk (ambao hata ukiupata utaishiwa kuitwa kiwembe, malaya nk) lakini unafanyaje mgonjwa yuko mbele yako...Niwambie wanaJF, madaktari tunowaona wanaenda kazini kila siku ni kwasababu ya mambo yafuatayo:
1. Hii ndio kazi inayowapa kula ya kila siku (they have to)
2. Wana mapenzi/wito na kazi yao
3. Wako motivated na satifaction inayotokana na kuona wagonjwa wanapona, ndugu wanafurahi, wanajifunza vitu vipya katka kutibu wagonjwa
4. Rushwa..nafasi waliyopo inawapa nafasi kupata hela kirahisi kwa njia ya rushwa (Mara nyingi hii huja kama asante, kwa madaktari wengi)

Najua humu kuna madaktari wengi...mnaweza kuni challenge pia.
 
Mkuu naona umechanganya hapo,wenye fani yao watakuja kunisahihisha na mimi.Nadhani medical officers ndiyo MD,na wengine ndiyo hao medical assistants na clinical officers kama sikosei

Medical Assistants na Medical Officers wote ni wamoja .

[h=1]Clinical officer - are health care providers in Sub-Saharan Africa who practice modern medicine. They practice independently but may be supervised by a physician in some settings.[1][2][3] COs are trained to perform most or all the roles of a medical doctor, depending on jurisdiction, which include diagnosis and treatment of disease and injury, ordering and interpreting medical tests, performing surgery and referring patients to other practitioners.[/h]
Medical assistants - are health care providers who perform administrative and clinical tasks to support the work of medical doctors and other health professionals.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP] They perform routine tasks and procedures such as measuring patients' vital signs, administering medications and injections, recording information in medical records-keeping systems, preparing and handling medical instruments and supplies, and collecting and preparing specimens of bodily fluids and tissues for laboratory testing.

Hivi, Tanzania ina madaktari wangapi ambao wanatoa huduma ya kuangalia binadamu (Full MD siyo Medical Assistants au Medical Officers)? Na kati ya hao ni wangapi HAWAKO Dar-es-Salaam wako mikoani?

Mwanakijiji,

Mie sitaandika mengi kwani nimejitahidi kuelezea tatizo la madaktari kwenye comments za Raia mwema kwenye comments section. Suala la kujiuliza ni kuwa huyu Mheshimiwa Mbunge wa Kigamboni Dk (Medicine) Faustine Ndugulile kakimbia kutoka kwenye front line profession na kuishia Dodoma kwenye maisha magumu. Sasa unategemea mtu kama yeye ambaye ametokea huko si muda mrefu (late 90's) angekuwa mstari wa mbele kuchampion hilo suala...lakini kimya!!!!Bado wapo madaktari wengine wengi tu.

Tatizo la madaktari ni Apex ya nature ya Umma wa Watanzania kuwa ni wapole na wanyenyekevu wenye kupenda amani na utulivu wakiwa wapo radhi kulala njaa na ndugu zao kufa (avoidable deaths) na kuishia kusikia so called "wasomi wetu - intellectuals" wakisema "Mungu kapenda" na "Kazi ya Mungu haina makosa". Sasa huyo Mungu anapenda watu wafe vifo avoidable deaths Tanzania tu? Mbona huko US, EU, Canada, Australia, NZ, Japan etc wanaishi mpaka miili yao inachoka wanaomba wajiue?.

Mie naona tatizo letu linachangiwa na culture yetu ambayo politicians wanaipinda kinamna ili kutake advantage for their own benefit. Ni mara ngapi tumesikia Mh Rais Dk. JK ametuma salamu za rambirambi kwa marehemu wa waliozama kwenye meli au ajali ya basi etc.
Mwanakijiji wewe unaonaje?
 
Tusisahau pia kuwa Madaktari wanatokana na wale ambao wamefaulu sana kuanzia shule za chekechea, shule za msingi na sekondari. Kwa kifupi, ni ile cream ya wasomi toka mwanzo. Leo hii, wale waliokuwa wanasuasua kwenye masomo wanapata marupurupu (sio lazima mishahara) inayowafanya madaktari waonekane kama vijakazi wao. Madaktari wanashindwa kusomesha watoto, wanashindwa kuwa na usafiri wa uhakika, wanakaa (au wanajenga vibanda wanaviita nyumba) wakati vilaza wanasomesha watoto ughaibuni, wanatembelea mashangingi na kujenga mahekalu!

Its not a wonder watoto wanaofaulu vizuri Form IV wanaamua kuachana na PCB, PCM na kwenda EGM, HGK, etc. Pia its not a wonder good performers wa PCB, PCM wanaamua kwenda kusoma BAAF na Laws Mzumbe, MuCCOBS na UD. Madaktari na Engineers wanakwenda wale ambao uwezo wao kwenye fani hizo ni mdogo.

Nakuacha Ukisie matokeo ya hiyo professional drift
 
Nimefurahishwa na makala yako umefanya kazi nzuri ku highlight mambo ya muhimu na umechukua muda kuyaelewa matatizo ya madaktari wa Tanzania. Nitoe mchango mdogo.....Madaktari wa Tz wanafanya kazi katika mazingira magumu mno (natambua kuwa wafanyakazi wote wa umma wanafanya kazi katika mazingira magumu Tz) Hebu tazama mifano hii: Mosi,daktari anapokuwa kazini pamoja na kumtibu mgonjwa lakini yeye pia anakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kama TB, VVU/UKIMWI, Hepatitis nk haya ni magonjwa yanayoleta kifo! Katika hospitali zetu nyingi hakuna vitendea kazi vya kutosha kumkinga daktari/na wauguzzi dhidi ya hatari hizi. Madaktari wanalowa damu kila siku katika kuokoa maisha ya watu (kwa kipindi cha UKIMWI) hii ni hatari kubwa! Hakuna miwani mikubwa kuzuia damu kuwarukia machoni madaktari wakati wa upasuaji(kama zipo ni muhimbili na katika miji mikubwa hapa Tz) nina experience ya kuzamisha mkono katika uke wa wa mama aliyejifungua huku nikiwa nimevaa glovu inayoishia katika kiganja cha mkono ilihali mkono wangu ulizama hadi kwa kufika katika kiwiko (watawala wanakuambia hakuna glovu ndefu) ukifikiria sana unajiona mjinga kwa kujiweka katika risk ya UKIMWI nk (ambao hata ukiupata utaishiwa kuitwa kiwembe, malaya nk) lakini unafanyaje mgonjwa yuko mbele yako...Niwambie wanaJF, madaktari tunowaona wanaenda kazini kila siku ni kwasababu ya mambo yafuatayo:
1. Hii ndio kazi inayowapa kula ya kila siku (they have to)2. Wana mapenzi/wito na kazi yao
3. Wako motivated na satifaction inayotokana na kuona wagonjwa wanapona, ndugu wanafurahi, wanajifunza vitu vipya katka kutibu wagonjwa
4. Rushwa..nafasi waliyopo inawapa nafasi kupata hela kirahisi kwa njia ya rushwa (Mara nyingi hii huja kama asante, kwa madaktari wengi)

Najua humu kuna madaktari wengi...mnaweza kuni challenge pia.

Kizimkazimkuu,

Hapo nilipoweka bold ndipo panawarudisha nyuma. Ni kitendo cha aibu kuona eti daktari analalamikia mshahara mbuzi anaolipwa na serikali. Kwani hata wakiongeza wakaanza kuwalipa 5,000,000 TSh/month bado soon itakuwa haitoshi kwa jinsi inflation inavyokwenda na pia matumizi yenu yanatazidi kuongezeka. Binafsi naona nyie madaktari ndio watu wenye opportunity ya kujiajiri wenyewe na kutoka kwenye hizo hospitali za serikali na kuanzisha za kwenu binafsi.
Ni aibu kwa best brains zetu kulia njaa kwa serikali inayoongozwa na wagonjwa wa akili. Nyie mkilia njaa na hao wengineo kama walimu na wale waliokuwa wanakuwa wakatikati na wamwisho darasani hivi sasa hawana ajira za kueleweka wafanye nini? Hawa madaktari wetu wajue kuwa vyeti vyao ndio mitaji yao. Hata hizo Apollo huko India zimeanzishwa/zinamilikuwa na vikundi vya madoctors "Medical Groups" ambao wamechukua mikopo kuanzisha na kukuza hizo institutions mpaka zilipofikia. Nyie doctors kazi kulalamika serikali serikali...mmeshawahi sikia serikali gani inalipa mshahara mkubwa? Serikali ni huduma kwa umma.
Mwanakijiji ameulizia kuhusu statistics za Doctors holders wa Doctor of Medicine degree mpo wangapi..yaani hakuna hata muwakilishi wa chama chenu aliyekuja hapa mtandaoni kutupa hizo statistics. Inaonyesha how pathetic and disorganized bunch of "m$@##*s" you are ...kazi kulalamika bila kuweka concrete action plans na strategy za kufanikisha mnapata good working conditions. Msisubiri mpaka tuwatukane humu JF ndio muanze kutushutumu. Msione Wayahudi wamefikia hapa walipo (kushikilia the Only SuperPower)...ila waliplan kwenye Zionist conference 1887 kuwa wanahitaji kuwa na nchi yao. Phase 1 ikawa achieved 50 years later. Phase 2 consolidation in another 50 years ndipo hapa walipo. Waarabu na pesa zao zote "Petrodollar" wameishia kupiga kelele kama debe tupu. Binafsi ninahasira sana na madaktari wa Tanzania... natamani niwahutubie kama JK alivyowahutubia wafanyakazi wa serikali na kuwaita MBAYUWAYU... NAMI PIA NIONGEZEE SPECIFICALLY KUWA MADAKTARI WA TANZANIA NI KAMA VILE KUNGURU wanauwezo wa kujitengenezea vipato na maisha mazuri kwa kujiajiri ila kazi kuililia serikali ambayo ni proven failure(Mnikosoe mniambie lini serikali ya TZ imeweza kudeliver anything on ime and within budget?). Mpaka hapo mtakapoacha tabia ya kukimbilia ajira wizarani (mjiheshimu na kuheshimu taaluma yenu) ndipo serikali itakapo waheshimu.

Doctors nawatakia malalamiko mema.
 
Back
Top Bottom