BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,849
Madaktari waipinga ripoti ya upasuaji tata MOI
na Lucy Ngowi
Tanzania Daima
SIKU moja baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa kutangaza ripoti ya tume aliyoiunda kuhusu upasuaji tata uliofanywa na madaktari wa Taasisi ya Mifupa na Tiba Muhimbili (MOI), baadhi ya madaktari wameipinga kwa madai kuwa haikugusa baadhi ya maeneo muhimu.
Wamesema tofauti na tume ya kwanza, tume ya pili iliyoundwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa, haikuwahoji swali lolote kuhusu uongozi wa taasisi hiyo ambao umekuwa ukilalamikiwa muda mrefu sasa kuwa unaongoza vibaya taasisi hiyo.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, madaktari hao kila mmoja alianza kwa kumpongeza Waziri Mwakyusa kwa kuunda tume hiyo baada ya kubaini ya awali ilikuwa na upungufu, katika maelezo yao hawakuwa na kigugumizi kueleza kuwa ripoti ya tume ya waziri ni ya uonevu.
Huku wakisisitiza majina yao kutoandikwa gazetini kwa madai kuwa wanaogopa kushughulikiwa, walisema wameshangazwa na ripoti hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imewashughulikia watumishi wa ngazi za chini na kutowagusa wale wa ngazi za juu na wale walio karibu na menejimenti.
"Hii ni ripoti kati ya ripoti za ajabu ambazo tumewahi kuzisikia, kwani kinachoshangaza Mkurugenzi Mtendaji Profesa Lawrence Museru, ambaye ndiye msimamizi wa taasisi, pamoja na madudu yote katika taasisi hii, tume hiyo haikumgusa hata sehemu moja, inaonekana kabisa ni ripoti 'feki'.
"Kama kuna aliyeusifu uongozi huo labda ni mmoja wa wakurugenzi ambaye ni rafiki wa karibu wa Profesa Museru, tulivyokuwa tunaulizana baada ya kusoma magazeti leo (jana) kila mtu alidai kuwa hakuulizwa swali hilo. Inaonyesha ripoti hii imepandikizwa," alisema mmoja wa madaktari hao.
Madaktari hao walieleza zaidi kuwa ripoti hiyo inashangaza kwa sababu hakuna kiongozi yeyote katika 'firm' ya neurosureery ambayo inahusika na upasuaji wa ubongo aliyeguswa kwa uzembe huo, kwa kuwa wako karibu na mkurugenzi.
"Aliyepasuliwa kichwa ni wa firm ya upasuaji ubongo (neurosureery) lakini kwenye ripoti ya tume hakuna maelekezo ya mtu anayetakiwa kuwajibishwa, viongozi wa hiyo firm wako karibu na menejimenti ambayo haikuguswa katika ripoti hiyo. Sasa tunajiuliza, kwa nini mkuu wa firm na mkurugenzi wa kitengo hicho hawajaguswa kwa uzembe?" alihoji daktari mwingine.
Baadhi ya wauguzi waliotoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo walieleza kuwa hawajaridhishwa nayo kwa sababu imegusa baadhi tu ya wahusika wa sakata hilo na kuwaacha wengine ambo ni vigogo katika taasisi hiyo.
Gazeti hili pia liliwasiliana na baadhi ya madaktari wanaotuhumiwa kuhusika na upasuaji huo ambao pia walitoa maoni kwa sharti la kutotajwa majina yao gazeti.
Mmoja wa madaktari hao alisema ameipokea ripoti hiyo lakini hana la kuzungumza anasubiri kuitwa kwenye Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo ambako ataeleza kila kitu anachokifahamu kuhusu tukio hilo lilivyotokea na hali halisi ya taasisi hiyo.
Alipoulizwa kwa njia ya simu ya kiganjani kuhusu kauli hizo za madaktari wa taasisi yake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Lawrence Museru, alisema hawezi kuzungumzia madai ya madakatari hao kuikataa ripoti hiyo kwa sababu hajaisoma na aliwashangaa wanaoipinga, kwa maelezo kuwa hata wao watakuwa hawajaisoma.
"Sijasoma ripoti yenyewe, hivyo siwezi kuzungumza lolote kuhusu hawa wanaoipinga, nashangaa kwa sababu naamini hata wao hawajaisoma…lakini wanaoipinga ni kina nani, kwanini hawajitokezi hadharani kuipinga? Walipinga ile ya mwanzo, nikakubaliana nao kwa sababu ni haki yao, sasa hata hii ya waziri wanaipinga?
"Nadhani jambo muhimu kwa daktari yeyote mwenye shaka na ripoti hiyo ni kwenda kwa waziri na kumweleza kuwa hakubaliana na ripoti na atoe sababu zake, na kama hamwamini waziri bado aende kwa waziri mkuu au kwa rais, kwa sababu mtumishi yeyote analindwa na sheria na taratibu za nchi.
"Kinachonisikitisha ni nia inayoonekana sasa ya baadhi ya watu kutaka MOI ivunjwe kwa kosa hilo moja, ninakubali ni kosa na makosa yapo lakini makosa kama haya yanatokea hata Ujerumani na Marekani, sasa kwa nini hili linaonekana kushikiliwa sana?" alihoji kwa masikitiko Prof. Museru.
Akizungumzia tuhuma za kutoiongoza vizuri taasisi hiyo zinazoelekezwa na baadhi ya wafanyakazi katika uongozi, alisema yeye kama binadamu ana upungufu, hivyo hawezi kukataa kuwa na makosa.
Hata hivyo alisema baada ya tuhuma hizo kuanza kutolewa, aliwasiliana na uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya (TUGHE) ili kujua kama wana malalamiko kuhusu uongozi wake, lakini alihakikishiwa kuwa hakuna mfanyakazi aliyelalamikia staili yake ya uongozi.
"Mimi si Mungu, ni binandamu, nina makosa yangu, na hata hao wanaonilalamikia nao si Mungu ni watu na wana makosa yao. Walipolalamika niliwaita viongozi wa TUGHE nikawauliza kama wana malalamiko yoyote kuhusu uongozi wangu, wakasema hawana, sasa sijui kwa nini haya malalamiko hayapelekwi sehemu zinazostahili.
Prof. Museru alisema baada ya kuisoma ripoti ya tume iliyoundwa na waziri, anaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuizungumzia na kusisitiza kuwa anaamini imefanya kazi yake vizuri kwa sababu hata yeye ilimhoji, tofauti na inavyodaiwa na baadhi ya madaktari kuwa tume hiyo haikumfikia kumhoji.
Mwishoni mwa wiki, Waziri Mwakyusa aliitoa hadharani ripoti ya upasuaji tata katika taasisi ya MOI ambapo madaktari sita na wauguzi sita walipatikana na makosa ya uzembe yaliyosababisha kufanyika kwa upasuaji tata wa wagonjwa wawili katika taasisi hiyo, Novemba mosi mwaka huu.
Kwa maelezo ya Mwakyusa, matatizo hayo ya uzembe yaliwahusu madaktari bingwa wawili, madaktari wasaidizi watatu, daktari wa usingizi, wauguzi wa dawa ya usingizi wawili, wauguzi wa upasuaji wawili na wauguzi wa wodini wawili, ambapo ripoti hiyo ilieleza kuwa wote kwa pamoja hawakufanya kazi yao vizuri.
Waziri alisema, hali hiyo ilichangiwa na mahusiano duni kati ya mgonjwa, muuguzi na daktari kwa kuwachanganya wagonjwa Emmanuel Didas (20) na Emmanuel Mgaya (19) ambaye sasa ni marehemu, kwa kuwa ugonjwa haukuhusishwa na mgonjwa mwenye ugonjwa, bali waliridhika kwa kuangalia majibu ya vipimo pekee.
Waziri aliagiza bodi ya wadhamini ichukue hatua kali za kinidhamu kwa wale wote waliozembea katika kuwahudumia wagonjwa hao, na iendelee kuchukua hatua kwa wengine wote watakaofanya hivyo, baada ya tukio hilo, pamoja na kusimamia kwa karibu utawala wa MOI na kuimarisha utendaji wake.
Pia aliitaka bodi hiyo kuisimamia menejimenti, ili iwafikishe mara moja kwenye baraza la madaktari, madaktari wanne waliosimamishwa kazi kutokana na taarifa ya tume ya kwanza, pamoja na wengine wanne ambao tume yake imewakuta kuwa wana tuhuma za kujibu, ambao ni wasaidizi wa madaktari bingwa na dawa za usingizi.
Waziri aliagiza menejimenti iwafikishe wauguzi wanne ambao hawakuwa makini katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalamu kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua hizo hizo.
Katika sakata hilo, Didas alifanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu wa kushoto na marehemu Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu wa kushoto badala ya kichwa, kabla ya kupasuliwa kichwa kilichokuwa na matatizo na siku chache baadaye akapoteza maisha.
Waziri alisema, uchunguzi umebaini kuwepo kwa udhaifu katika kusimamia taratibu zilizopo zinazohusiana na upasuaji na huduma za wagonjwa kwa ujumla. Kwani upasuaji tata huo, ulichangiwa na kutokufuata maelekezo ya madaktari waandamizi, hali iliyosababisha orodha ya wagonjwa wa kupasuliwa kuwa tofauti na maelekezo ya jopo la madaktari bingwa.
Aliiagiza bodi hiyo imwagize mkurugenzi na wakurugenzi wakuu wa vitengo wa MOI, kusimamia utendaji kazi ipasavyo na kuwasilisha taratibu mpya zitakazoimarisha usimamizi wa idara zote.
Alisema, tukio hilo ni fundisho katika utoaji wa huduma za afya nchini, hivyo amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wilson Mukama, atoe mwongozo utakaoimarisha utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuzingatia vigezo vinavyokubalika katika upasuaji na huduma nyingine za afya na waraka huo usambazwe katika hospitali zote nchini.