Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...

Akili ndogo kuongoza kubwa!

Unafukuza madaktari wananchi wanaumia.
Ni sawa kabisa kuwafukuza kama wamekiuka terms ajira yao, sio wao tu hiyo ipo popote duniani unapokiuka taratibu za kazi unaadhibiwa. Tayari wananchi walikuwa wanaumia wakati wao hawaji kazini. Kusimamishwa kwao kazi bado hawako kazini -- means 0+0=0
 
hao waliowafukuza madaktari wako juu ya sheria? Leo bungeni spika amesema waziwazi kuwa hata serikali haitaruhusiwa kutoa kauli (kama walivyoahidi jana) kwa sababu hili swala liko mahakamani, na amri ya mahakama ni kuwa pande mbili yaani serikali na madaktari wakae kwenye meza ya mazungumzo. Sasa mbeya, bugando na dodoma ziko juu ya amri ya mahakama? Au hawa wako kenya?

Kwa upande mwingine huu ni mtihani kwa mhimili wa dola - mahakama. Kama hawatesema chochote kwa hizi hospitali za mbeya, bugando na dodoma basi ni wazi mahakama itakuwa inafanya kazi kwa shinikizo la serikali ya ccm. Hili litakuwa agizo la serikali kuwafukuza chini chini bila na mahakama ikae kimya wakati amri yake inapuuzwa! Tusubiri ili tuone independence ya judiciary yetu.

acha kupotosha waliambiwa wakae meza ya mazungumzo wakitokea kwenye mgomo?
 
Mahakama inaingiliwa pale jambo hili linatakiwa kujadiliwa bungeni ili ushauri sahihi upatikane. Kutoa maamuzi na kuyatekeleza kabla mahakama haijahukumu hakuiningilii mahakama. Hayo ni maajabu! Bunge iliunda kamati kufuatilia jambo hili, lakini bunge hilo hilo halipaswi kupokea taarifa ya kamati waliyoituma ipate kujadiliwa. Ee Mwenyezi Mungu lisaidie taifa la Tanzania, ukaturejeshee hekima yako katika jambo hili!
 
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.

are you out of your mind ? put yourself in those shoes how do they pinch ehh?
 
wengi wetu hatujui legal procedures za kuendesha migomo kazini. Serkali mara hii imejipanga vizuri kushughulikia mgomo huu ksheria. Drs wasipoangalia ,itakula kwao.
Kuendesha mgomo bila kufuata taratibu , itawapa nafasi serikali kufukuza madaktari kwa kukiuka sheria ya kutofika kazini. Hii itafanya kwa kila hospital. Madaktari watarudishwa kwa mwajiri wao - wizara ya afya.
Kurudishwa kwao kazini itakuwa kwa msharti mapya na magumu.
Wananchi wengi kwa sasa hawana sympathy na drs.
They should start thinking strategically wengine wanafamilia. Tusifuate maamuzi ya mob.

wanashinda jf wanafikiri wananchi wanawasupport kama humu tunaanza kuwachukia.
 
Kwakuwa hii ni taarifa/woningi kwa wananchi/walalahoi ambao ilikuwa ni chaguo lao mwaka 2010. Wakirudia tena kuchagua magamba wajue hali hii watakumana nayo tena. Pia kitendo cha kufukuza madaktari ni dalili tosha kuwa wanauwezo mkubwa wa kuleta wengine toka nchi za nje, swali/kiulizo Je! kama wameshindwa kuwapa haki yao hawa waliopo wataweza kuwalipa hao wengine? La sivyo basi Magamba watapewa msaada ambao pia tunachohofia nimisaada ambayo itakuwa na masharti, Itafikia mahali tutashikishwa UKUTA kisha tupewe misaada, ?????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wanadhani tutarudi nyuma kwa kitisho cha kufukuza kazi. Ngoja twende SHIRIKA LA KAZI DUNIANI. Watajua sisi ni nani! LIWALO NA LIWE
 
Serikali inapaswa kutatua jambo hili haraka iwezekanavyo, masikini ndio tunaumia, wao wanaenda kutibiwa nje...mungu saidia taifa letu maana tunapoenda huko mbele ni lazima watu watachoka , tutaishi kama syria
 
Fukuza wote. Tuungane nao twende uwanjani, tushinde, tukeshe, hadi tuiondoe nyinyiemu madrakanu. Good start for revolution. Hii nchi ilipofika hatuhitaji reforms bali revolution.
 
Ni sawa kufukuzwa. Na wengine wanaukaidi wafukuzwe wote! Watu mara nyiingi hofu husababisha kuendelea kuwa watumwa na maskini wa mawazo kwa kuogopa kuchukua hatua hata kama itatugharimu na pengine maisha. Najua kweli athari za kufukuzwa hazitawahusu 'wakubwa' moja kwa moja, lakini, hata hao wana ndugu zao kama sisi watakaoteseka.

Kawaida, kila badiliko la kijamii huja na madhara, lakini mfumo wa kijamii (Social System) una kawaida ya kurudi kwenye hali sawa (equillibrium) lakini kwa gharama kubwa.

China kwa mfano, iliamua kuacha kupokea misaada ya chakula kutoka nchi za magharibi baada ya mmoja kuandika "Who Will Feed China?" Wachina waliwatoa wazungu na misaada yao kwa kudhalilishwa. Watu walikufa njaa kwa miaka mingi, lakini walifanya kazi kwa kibii na kuleta Mapinduzi ya Kijani (Green Revolution) na sasa wanalisha dunia.

Tukubali kuteseka, watu, wapendwa, ndugu, jamaa na maraki watapoteza maisha, but this will nourish the tree that will bear the fruits of true freedom. commitments and passion to our country and its people. Madakari waondoke, tutakunywa hata mizizi ya miti, tutakufa, lakini wapo watakao survive, na kuwa madaktari na hao hawatafanya dhambi hii, maana itakuwa kumbukumbu kwa vizazi kwa wakaopoteza maisha

dats true! Bora uwaambie ukweli tu
 
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.

Ni uamuzi mgumu. Hata hivyo hauna mbadala kwani 'mchelea mwana kulia hulia yeye'
 
Back
Top Bottom