Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vancomycin, Jun 28, 2012.

 1. V

  Vancomycin Senior Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Taarifa ambazo zimethibitishwa zinatabanaisha kuwa madaktari walio katika uzoefu kazini, INTERN doctors wameanza kufukuzwa katika hospitali mbalimbali ambapo katika hospitali ya DODOMA madaktari 11 kati ya 33 wamefukuzwa na madaktari wote 70 waliokuwepo hospitali ya rufaa mbeya chini ya ulinzi mkali wa polisi wameambiwa waondoke kufikia saa 11 jioni ya leo wakati huo huo mkurugenzi wa hospitali ya BUGANDO amewafukuza madaktari wote 44 na kuwataka warudi wizarani wakati madaktari waliosajiriwa wameamuriwa kufika kesho wawe kazini au la wanafukuzwa.

  Wakati huo huo madaktari wakazi waliitwa na senate ya BUGANDO na kulazimishwa kurudi kazini lakini walikataa mbele ya senate hiyo hivyo wakaambiwa watafutiwa udahili wao na wote kwa pamoja wakapiga makofi wakisema wako tayari kwa hilo.

  Habari zaidi zinazidi kupasha kuwa hospitali ya Mwananyamala wameletewa fomu za kujaza kama wako tayari kuendelea na kazi au la,ila madaktari wamesimamia msimamo wao huo kuwa mgomo uko pale pale.

  Katika hatua nyingine CHUO CHA TIBA BUGANDO NA KILE CHA MUHIMBILI VIKO MBIONI KUFUNGWA kutoka na walimu wao ambao ni madaktari kugoma na mazingira kutokuwa rafiki kwa kujifunzia.

  Wakati hayo yakiendelea taarifa zinasema hsopitali ya Tanga BOMBO imeingia rasmi kwenye mgomo na ile ya MOUNT MERU

  Habari zaidi madaktari wanajiandaa kwa mass resignation muda wowote

  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa mwendo huu miaka ijayo mbeleni wenetu watasomea udaktari kweli? Labda kama watakukuwa na uhakika wa ajira za Botswana
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ndio hayo alipanga kuyasema bungeni ila la Olimboka likaingilia mikakati
   
 4. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Sijui mwisho wake ni nini!
   
 5. L

  Lorah JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  duh ngoja tuwafungulie ndugu zao wa mirembe waje wawasaidie huko Bungeni...
   
 6. gorretti54

  gorretti54 Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pinda na Kikwete wakawatibu wagonjwa...
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Lohhh, na kuna watu wanaendelea kulala huku wakisema "ni upepo, utapita".

  [​IMG]
   
 8. spartacus

  spartacus JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  seriously, serikali na madaktari watatuua...................
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Liwalo na liwe mzee wa mee ajiuzulu
   
 10. gorretti54

  gorretti54 Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mgomo utatengeneza mazingira mazuri ya wanetu kukimbilia fani ya udaktari....
   
 11. m

  mamajack JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Unajua serikali dhaifu bado inaamini kuwa watu wataogopa kupoteza kazi zao.
  Madaktari wanawabipu, nyie wapigieni tu.
   
 12. Rasib

  Rasib JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani, serikali kuna roho za watu...hima hima jaman
   
 13. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,268
  Likes Received: 8,334
  Trophy Points: 280
  kama hizi taarifa ni kweli basi sasa naanza kuamini tahrir square yetu haiko mbali.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ni kwanini serikali haitaki kutekeleza madai ya madaktari?
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waliodhania kwamba Dr Ulimboka ni wa hivi hivi sasa maandishi yote yako ukutani.
   
 16. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kuna wajinga wanataka wageuze majengo ya hospitali magofu na magodauni yakuwekea mali zao za kifisadi.
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Wakuu endeleeni kutujuza kila linaloendelea kutoka kila mkoa na nawaomba sana Madakatari msivunjike moyo kwa lolote,maana nchi yenyewe ndo hii,maamuzi kama yatakuwa ndio haya wala msihofu,tafakarini hili,je ni kweli kwamba hakuna maisha nje ya ajira za serikali?na ni vipi muendelee kuwa watumwa?
   
 18. s

  swrc JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii sirikali hapa ilipofikia inatisha
   
 19. k

  kitero JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mwisho wa haya yote nini jamani? sasa inahitajika kufanya maombi na mafungo kwajili ya Taifa letu tunakokwenda ni kubaya hali inazidi kuwa ngumu tuu kwa mlala hoi na inazidi kuwa nzuri kwawalio nacho.
   
 20. K

  Kapeleka Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

  Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
   
Loading...