Madaktari waeleza umuhimu wa nywele sehemu za siri

Mbona baadhi ya Mikate tunayokula inatengenezwa ( inaandaliwa ) kwa Ngano kupondwapondwa kwa Miguu huku Majasho na Makamasi yanapengewa humo humo na bado tunainywea Chai mpaka Kushiba?

Sijaona hicho kitu, labda kwa wadosi/india.
 
Psychology tu hiyo ndo inayochingia..kwamba kwa bibi now kuko poa,

Mimi nikishave huwa naona dushe limeongezeka..sasa sijui hiki kimabia kinanidanganya au vipi?
Ila kweli inawezekana ni suala la kisaikolojia tu!

😂😂😂 Itabidi ujithibitishie hilo pasi na shaka kwa kulinganisha hilo dushe before and after shaving!
 

Madaktari waeleza umuhimu wa nywele sehemu za siri​

sehemusiripiccc


Dar es Salaam. Wataalamu wa afya nchini Tanzania wamesema nywele sehemu za siri hazitakiwi kuondolewa kutokana na umuhimu wake hasa kuzuia bakteria na wadudu mbalimbali kuingia mwilini.

Wamesema kulingana na tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa, nywele sehemu za siri husaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa na kuzuia uchafu na vimelea ambavyo vinaweza kuingia mwilini kupitia sehemu hizo.

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Isaya Mhando amesema, “umuhimu wa nywele za siri ni kuonyesha kwamba huyu mtu amekomaa, ukimkuta binti au mkaka ana miaka 30 hana nywele lazima uwe na uwalakini na mfumo wake wa uzazi.”

“Hiyo ni mojawapo ya matatizo yanayoonyesha huyu mtu ana upungufu na matatizo ya homoni, lakini pia ukiona nywele tegemea kuona damu yake ya hedhi kwa msichana na sauti nzito kwa mvulana.”

Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo kwa mwanaume, Dk Erasto Wambura amesema mabadiliko ya homoni huwezesha nywele hizo kuota wakati wa balehe.

Amesema nywele hizo huota kwa sababu maalum na zina kazi zake kulingana na namna ambavyo zimeota kuanzia juu mpaka chini ya mizizi yake ambayo hata ukizikata usipoutoa mzizi huo huota tena.

“Kila nywele inayoota katika mwili wa binadamu ina kazi maalum, kwa nywele za sirini chini yake kuna baadhi ya kemikali zinazozalishwa kwa ajili ya kulinda bakteria zinasaidia ulinzi katika sehemu husika.”

“Hii ndiyo sababu ukizisumbua kwa kukata vinaota vipele kwa sababu umeondoa ulinzi hivyo bakteria wasiofaa wanakwenda kushambulia yale mashina ya nywele na wanaota hapo ndio maana mtu anapata vipele,” amesema.

Dkt. Wambura ametaja kazi za nywele za sirini kuwa ni kuchuja jasho, kukamata vumbi na vitu vingine vinavyoweza kusababisha bakteria akakaa kwa muda mrefu.

Hata hivyo amesema nywele hizo kuwepo sirini si uchafu ijapokuwa nywele hizo zinaweza kuwa chafu kutokana na jasho au uchafu unaotoka katika sehemu za siri kunaweza kusababisha nywele hizo kuwa chafu.

“Uchafu inategemea na mtu, nywele hizi hukaa kwenye mikunjo na zinapopata joto ni rahisi kutengeneza uchafu ukiwa nazo ndefu inabidi uzikate, ijapokuwa mwingine kwake anaona ni vizuri jamii tuliyolelewa tunachukulia ni uchafu,” amesema.

Hata hivyo amesema kuna madhara yatokanayo na kuziondoa mara kwa mara au kuziondoa kabisa nywele hizo kwamba ni pamoja na kuwashwa, majeraha madogomadogo kutokana na matumizi ya wembe, vipele na kupata maambukizi kwa haraka.

“Kuondoa nywele sehemu za siri kunaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya zinaa, mara nyingi wengi wakinyoa wanapata vipele au vidonda hapo inakua rahisi kupata maambukizi, unanyoa na kuziacha kidogo lakini ukiziondoa kabisa umeondoa ulinzi,” amesema Dk Wambura.
Mwambie nguo ni mbadala wa hizo nywele. Kabla ya watu kuanza kuvaa nguo ni kweli zilikua na umuhimu. Lakini kwa ulimwengu wa sasa hapana
 
Back
Top Bottom