Lugovoy
JF-Expert Member
- Mar 2, 2011
- 573
- 170
Wewe PakaJimmy, is this Monday, a Blue Monday to you? Mbona leo umemiss point? Serikali, ndiyo agents of the Devil, wao ndiyo wana wa kuzimu! Serikali, ndiyo accountable, kwa vifo vitakavyotokea!
Kumbe, unajua, na Serikali inajua kwamba Madaktari wakiacha kazi siku moja tu, watakufa watu wengi! Kama ni hivyo, ebu sasa tujadili!
Unajua kwamba Mbunge Sumari tangu achaguliwe na watu wa Jimbo lake, huko Arumeru, hakuweza kufanya lolote huko, kwa sababu ya ugonjwa? Je, ni watu wangapi walikufa katika Jimbo lake, kutokana na kukosa huduma ya Mbunge wao?
Vivyo hivyo, ni nani amekufa katika Wizara ya Maji, kutokana na kukosa huduma ya Waziri wa Maji, Profesa Mwandosya, ambaye hajaweza kufanya kazi, kwa miezi mingi? Kwa zaidi ya mwaka mmoja, wilaya nyingi, hazina Wakuu wa Wilaya. Nani amekufa, kwa kukosa huduma za Wakuu hao wa Wilaya?
Kama Jibu ni HAKUNA, basi Tanzania tujifunze kuwaheshimu Madaktari, kama wanavyowaheshimu, nchi nyingine. Serikali iache kutoa mishahara na posho nzuri, kwa wanasiasa wapiga porojo; na kupuuza maslahi ya Madaktari. Madaktari huko Marekani, wanalipwa kati ya 60 - 100$ kwa saa moja, kulingana na fani zao! Sawa, sisi hatuwezi kulipa mishahara hiyo; lakini Serikali iwalipe vizuri zaidi, kuliko wanasiasa. Madaktari msirudi nyuma katika mgomo wenu. Nchi hii, haki haitolewi katika kisahani, bila fight!
Mkuu ongezea na kwa Mh Mwakyembe hakuna aliyekufa Kyela kwa kukosa huduma ya mbunge wao kwa muda mrefu.