Madaktari Waamua Kutangaza Mgomo Rasmi Kuanzia Kesho tarehe 24/01/2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Waamua Kutangaza Mgomo Rasmi Kuanzia Kesho tarehe 24/01/2012

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by raybse, Jan 23, 2012.

 1. raybse

  raybse Senior Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lile sakata la Madaktari na Serikali Limefikia Madaktari Kuamua Uamuzi Mgumu wa Kuamua Kugoma rasmi kuanzia Kesho hii ni kutokana na Mikutano waliyoianza toka jumatano ya wiki iliyopita ya kujaribu kutafuta suluhu ya matatizo yao na Sekta ya Afya kwa Ujumla,Juhudi hizo hazikuzaa matunda kutoka kwa Serikali kuanzia ngazi ya Wizara ya Afya mpaka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo.

  Madaktari hao wana madai kadhaa ikiwemo Kuboresha Huduma za Afya nchini na Maslahi Duni kwa watumishi wa sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kufanya Kazi katika Mazingira Magumu, Lingine ni Kuondolewa kwa Katibu mkuu wa wizara ya afya Bi.Blandina Nyoni.

  Maamuzi hayo magumu yamefikiwa katika Mkutano wa leo uliofanyika Don Bosco Upanga DSM ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano isiyokoma iliyoanza Toka jumatano ya Wiki iliyopita.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimesikia mgomo ni wa wafanyakazi wote wa afya. Hali itakuwa tete nadhani. Leo nilisoma post ya kigwangala kwenye fb yake nikaona anamtumu Blandina Nyoni.
   
 3. k

  kalakata Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi maskini tusioweza kwenda private hospital tumekwisha, hivi serikali huwa haiono sababu ya kutatua migogoro kwa mashauriano mpaka watu wagome au waandamane ndio wasikilizwe! Hii si sawa kabisa
  Jamani mbadilike utawala wa hawa mabwana unatuchosha
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Blandina asipotoka hata kama mafao yataboreshwa, mgomo upo palepale??? Doh.... Imenoga hiyo!!! Mtihani mkubwa kwa JK!!!
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Watakaoteseka ni maskini hohehahe watoto na wajawazito vigogo wana madaktari wao
   
 6. k

  kiche JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sina uhakika kama hawatagawanyika!!!tumekuwa tukishuhudia migomo ya walimu ambapo wengine wamegoma wengine wamekamata chaki,naona kauli ya sumaye inaanza kutimia!!tusubiri na idara nyingine!!
   
 7. s

  shykwanza Senior Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watumishi wote wa sekta ya Afya nchini wametangaza kuanza mgomo wa nchi nzima kuanzia kesho tarehe 24/01/12 kwa madhumuni ya kudai maslahi yao. Source Clouds FM Jahazi:shock:
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa nini tusiwape cho badala ya wale Wazembe Bungeni Dodoma kujiongezea Posho kila siku bila tija yoyote kwa wananchi?? Au mpaka tuanze kufa bila tiba ndio kilio cha Ma-Daktari kitapata kusilizwa?

  Madaktari wetu mko sahihi jamani na ninawaunga mkono katika hili la MASLAHI ZAIDI ili iendane na huduma hasa mnazowapa Waheshimiwa Wabunge kwa kuwapeleka India.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa nini tusiwape cho badala ya wale Wazembe Bungeni Dodoma kujiongezea Posho kila siku bila tija yoyote kwa wananchi?? Au mpaka tuanze kufa bila tiba ndio kilio cha Ma-Daktari kitapata kusilizwa?

  Madaktari wetu mko sahihi jamani na ninawaunga mkono katika hili la MASLAHI ZAIDI ili iendane na huduma hasa mnazowapa Waheshimiwa Wabunge kwa kuwapeleka India.
   
 10. p

  plawala JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiakao cha kwanza kilikuwa trh 14 january,leo kilikuwa cha tano
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu ionyeshe kujali Madaktari wetu kabla hatujawakosa wakitimkia kwenda mataifa mengine ambapo huduma zao huhitajika sana na kuthaminiwa na jamii hizo.
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Haki inaposhindikana kupatikanika kwa round table talk, hatua inayofuatia hua ni mbaya hata kusimuliwa
  Labda watanganyika wataamka sasa, maana kiukweli Serikali inapojinadi imeleta maisha bora ilhali waletao hayo maisha bora ni wengine wanaoteseka usiku na mchana huku serikali ikikosa udhubutu wa kuonyesha japo utu kidogo kwa kupongeza na kuhamasisha mafanikio zaid huku ikiwaboreshea mazingira ya kutendea kazi wanataaluma hawa
  Ona walimu wanavyotaabika pale Sumbawanga, ileje, mpitimbi, kyela, masasi, lushoto, Ona madaktari, polisi na hata watumishi wangine wa ngazi za almashauri za wilaya wanavyonyanyaswa na kuonewa.
  Madaktari wamemfunga paka kengele, wengine waige mfano huu, si furahishwi na mgomo bali lazima tukubaliane panapokosekana haki hakuna jinsi
  Naamini wengi watapotezwa wapendwa wao kutokana na mgomo huu, wengi watapata vilema vya maisha, wengi watajikutwa wakibatizwa majina mapya kama YATIMA, WAJANE, VILEMA,
  lakini wakulaumiwa ni serikali yetu,
  Mungu ibariki Tanganyika, ILAANI SERIKALI YA M.KWERE
   
 13. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Ni taarifa za maumivu makali kwa sisi wananchi;loooooooooo!!!!
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  hili ndilo muhimu...........wacha wagome ...
   
 15. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ukiwa unaangali Bw. Mponda na Bi. Blandina Nyoni wanavyoongea huwezi amini kama kweli wanasimamia wizara hiyo.
  Ni sawa wenyenye kama wanavyoamini wameshafika kwenye level nyingine ya maisha na utawala lakini hawa wanaolalamika huku chini ndio wanaanimate kitu kinaitwa 'wizara ya Afya', kama hawapo hawa waheshimiwa wasingelikuwa wanaongea arrogantly kama wanavyofanya sasa.
  Ninachowakumbusha hawa waheshimiwa ni kuwa viongozi zamani walikuwa wakipiga siasa lakini siasa za leo sio kama za zamani maana zimeingiliwa na kumezwa na ufisadi wa kutisha.
  Mambo yanaweza kubadilika, hakuna ajuae kama hawa madaktari waweza kufungua 'mwanzo' mpya.
   
 16. k

  kiche JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tusubiri kauli ya serikali!!itakuwa ni ya kutojali na vitisho ila wakumbuke kuwa madaktari ni tofauti na walimu,wao hawatishiwi nyau nakumbuka kuna mwaka waligoma muhimbili tu badala ya kutatua tatizo wakakimbilia wanajeshi eti kwenda mujimbili kuokoa jahazi ambapo na wao walichemsha!!!

  Na si ajabu utasikia mtu anasema wanachochewa na wanasiasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Udaktari tabibu ni noble profession na mgomo ni upuuzi ukizingatia wamekula kiapo kwa Mungu. Serikali imewasomesha buree wakati watanzania wengine wanalipa kila kukicha. Hizo ni kodi za watanzania. Walipe fadhila kwanza. Waache upuuzi. Kama wanataka maisha ya hollywood wabadilishe fani and it is too late now!! Hii ni ndoa na wanatakiwa kuitumikia kwa uadiilifu. Kama ni mgomo ungepaswa sis walipa kodi. Hadi hiyo mishahara yao ni kodi zetu. Na hata maboresho ya huduma ni kodi zetu pia. Sasa tutawasaidia mpaka lini. Acheni upumbaf fanyeni kazi ya ujenzi wa taifa hadi pesa zipatikane tutawaangalia mbeleni.
   
 18. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Jambo la mbolea kwa madaktari kufanya. Message inayotumwa ni kwamba serikali inapaswa kujitambua kuwa nchi yetu ni maskini. Fedha tunayoipata kutokana na uchumi wetu tunapaswa tuitumie kwa mpangilio kwa kugharamikia mambo ya msingi halafu zile anasa zije baadae. Ndivyo tunavyofanya hata kwenye familia zetu. Mimi kama baba wa familia siwezi kunywa bia mpaka nihakikishe watoto wameshiba na wana afya ya kuridhisha. Serikali ya CCM wanafanya kinyume, watoto wana njaa na ni wagonjwa kupindukia lakini wakuu wa serikali wanafanya anasa za kutisha. Ili ijulikane kuwa hii ni nchi yetu sote madaktari wameonyesha njia. Next time ni waalimu.
   
 19. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As usual: They are not serious, sijawahi ona Mgomo Tanzania ukifanikiwa;do you know why sijaona madai yao hadharani ya kwamba wanataka kulipwa kitu gani bila facts plus figures then its the wrong foot:Kama ni huyo Nyoni iliyokuwa something ya mkulu au hao akina Deo na shekhe ubwabwa Mponda nothing will happen hao interns they can continue with mikutano yao na pia kwa kuwa hawatapewa posho watachoka sasa hivi.Tanzanians are so disunited when it comes to their rights na hii ni ajabu na kweli. If you don't believe me let us see ngoma ya kitoto haikeshi hatafika ijumaa.
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni habari mbaya sana kwa wananchi tulio maskini lakini ni haki yao
   
Loading...