BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,365
- 8,097
Chama cha Madaktari wa Wanyama Tanzania (TVA) kimetoa taarifa ya kupinga na kuonesha kusikitishwa kwake juu ya kitendo cha Kampuni ya Uzalishaji Vifaranga wa Kuku ya Kibo Poultry kuteketeza Vifaranga 50,000 hadharani kwa madai ya kukosa soko.
TVA wamesema pamoja na kutambua matakwa ya Kanuni za vituo vya Utotoleshaji (GN 959 of 2019 Regulation 11: Restriction to Rearing of Chicks beyong 72 at Hatcheries) zinazoruhusu kuahribu vifaranga waliokaa zaidi ya saa 72 kwa njia zinazoruhusiwa na kuheshimu Sheria ya Ustawi wa Wanyama Sura 154, Chama kinalaani kitendo hicho na hakijaridhishwa na njia zilizotumika katika uteketezaji wa Wanyama hao kwa kuwa ni za mateso na hasa ikifahamika kwa kuku ni viumbe wenye hisia (Sentient Beings) na ni kinyume cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama Sura 154: (Sheria namba 19 ya mwaka 2008 kifungu cha 4, 29 na 32 na kanuni zake.
Chama cha Madaktari wa Wanyama Tanzania kinaziomba Mamlaka husika kuchukua hatua stahiki ili kudhibiti tabia za ukiukwaji wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama na Kanuni zake unaoendelea kujitokeza mara kwa mara nchini.
Soma zaidi Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza