Madaktari wa Nairobi waanza mgomo kwa kutolipwa mishahara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,069
10,012
Shughuli katika hospitali za umma Nairobi, Kenya zimekwama baada ya madaktari kuanza mgomo wao. Hayo yanajiri baada ya madaktari hao kutoa ilani ya siku saba kwa kile wanachokitaja kuwa ni mazingira mabovu ya kazi.

Kenia Ärztestreik Streik (picture alliance/AP Photo/B.Curtis)
Mgomo wa madaktari hao ulioanza usiku wa manane huku maambukizi ya COVID 19 yakiongezeka, unayaweka maisha ya maelfu ya wagonjwa katika hatari baada ya mazungumzo kati ya chama chao na shirika la kutoa Huduma jijini Nairobi kusambaratika.

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari na Wafamasia nchini Kenya tawi la Nairobi Daktari Maelo Deogratious anadai kuwa madaktari wanaohudumia wagonjwa wa COVID-19 hawana bima ya afya ilhali maisha yao yamo hatarini.

Fedha zilizotolewa na rais
Rais Kenyatta alitoa shilingi bilioni tatu kwa wizara ya afya, huku sehemu ya fedha hizo ikitakiwa kutolewa kwa bima ya madaktari. Madaktari hao wanadai kuwa hawajapokea fedha hizo.

Kwa mujibu wa chama cha Madaktari na Wafamasia jijini Nairobi hawajakuwa na bima ya afya tangu Julai mosi. Ripoti iliyotolewa na madaktari hao inasema kuwa baadhi yao walioambukizwa virusi vya corona walilazimika kugharamia matibabu yao walipokuwa wanaugua.

Kenia Kenyatta National Hospital - Krankenhaus in Nairobi (picture-alliance/dpa/Kenyatta National Hospital)
Madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta Nairobi, Kenya

Aidha, wanadai kuwa hawajalipwa mishahara yao ya mwezi wa sita na saba. Maelo anasema kuwa jimbo la Nairobi halina eneo maalum la kuwatenga madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya ambao huambukizwa ugonjwa huo, wakiwahudumia wagonjwa, huku madaktari 15 wakiwa tayari wameuguwa virusi vya corona.

Mishahara yachelewa
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya Mercy Mwangangi, anasema kuwa mishahara ya madaktari ilichelewa kwa sababu ya usimamizi mpya wa jiji.

Mazungumzo kati ya madaktari na serikali yamekuwa yakifanyika kwa kipindi cha miezi sita sasa na hayajafanikiwa. Madaktari watano wamepoteza maisha yao tangu janga la virusi vya corona lilipoingia nchini Kenya, huku idadi hiyo ikihofiwa kuongezeka.

Nusu ya idadi yote ya maambukizi ya virusi vya corona imeripotiwa katika jimbo la Nairobi. Kenya imerekodi zaidi ya visa 31,000 vya ugonjwa wa COVID-19, watu 17,800 wamepona huku idadi ya waliokufa ikizidi 500.

Source: DW
 
Wazee wa kuvunja rekodi na KRA yao wakati wa corona lkn wanashindwa kulipa mishahara ya miezi miwili ya wahudumu wa afya
mbwembwe kama zote. hoo! tumekusanya kodi zaidi, mikopo ya covid19 plus misaada toka kwa mme wa Kenya. Tangaza sana maambukizi lakini wapi!
 
Tatizo ni mvutano wa maseneta kuhusu mswada wa mgao wa hela kwa gatuzi mbali mbali nchini Kenya, sio kwamba hela hazipo. Ndio maana mishahara yao imecheleweshwa. Kwa wasiojua, sekta ya afya nchini Kenya ipo mikononi mwa gatuzi 47 za Kenya, yaani 'counties', sio serikali kuu. Watz acheni kujiliwaza wakati madaktari wenu ambao wanalipwa sawa na manesi wa Kenya, bila nyongeza kwa muda mrefu, hawana sauti kabisa kuhusu maslahi yao kazini.
 
Wacha kutetea ujinga, tatizo la madaktari wenu kutolipwa kwa wakati ni tatizo la miaka mingi sio jipya, wacha kusingizia maseneta.

Wewe wacha kutetea ujinga, matatizo ya Kenya ni mengi sana, kumbuka madakatari wenu walishawahi kugoma kwa zaidi ya siku 100 bila ufumbuzi kupatikana, hii ni dalili ya serikali dhahifu, hivi inaeezekanaje huduma za Afya kusimama kwa siku 100 na bado serikali ikabaki madarakani?

Jambo ambalo ni jambo la kipuuzi mnalirudia mara kwa Mara ni hilo la kusingizia Counties, kwani Kenya ndiyo nchi pekee yenye utawala wa Counties hapa Africa, mbona huko Hakuna Matatizo?

Ukweli ni kwamba, lolote lile linalofanyija Kenya, halifaniki hata kama nchi zingine linafanikiwa. Kenya is really a failed state.
 
Tatizo ni mvutano wa maseneta kuhusu mswada wa mgao wa hela kwa gatuzi mbali mbali nchini Kenya, sio kwamba hela hazipo. Ndio maana mishahara yao imecheleweshwa. Kwa wasiojua, sekta ya afya nchini Kenya ipo mikononi mwa gatuzi 47 za Kenya, yaani 'counties', sio serikali kuu. Watz acheni kujiliwaza wakati madaktari wenu ambao wanalipwa sawa na manesi wa Kenya, bila nyongeza kwa muda mrefu, hawana sauti kabisa kuhusu maslahi yao kazini.
Blah blah blah, that is just one, amongst many signs of a failed state we're seeing.
As a pro jubilee lazima utatetea tu.
 
Sasa serikali yenyewe imewajibu madaktari kwamba haina pesa, wewe ni nani unayesema pesa ipo?, wacha kupenda kutetea ujinga
 
Blah blah blah, that is just one, amongst many signs of a failed state we're seeing.
As a pro jubilee lazima utatetea tu.
Sijamtetea mtu yeyote yule. Mimi nimewapa tu facts kama zilivyo, maanake wengi wenu huwa mna uelewa finyu kupindukia. Alafu kama kawa huwa hamsomi taarifa kwanza na mkisoma huwa hamuelewi chochote. Mgogoro kuhusu mswada ambao upo Seneti ni jambo ambalo kila mkenya analifahamu vyema. Lawama zote zipo kwa rais U.K na Rt. Hon RAO kwa 'interfence' yao kwenye masuala ambayo Seneti inafaa itoe maamuzi huru bila presha kutoka kwa mtu yeyote yule. Nashangaa sana kwamba hata kiswahili pia hamkielewi, au hamjaona haya yanayohusu gatuzi la Nairobi kwenye taarifa? ..."Mishahara yachelewa Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya
Mercy Mwangangi, anasema kuwa
mishahara ya madaktari ilichelewa
kwa sababu ya usimamizi mpya wa
jiji." :confused:
 
Sasa serikali yenyewe imewajibu madaktari kwamba haina pesa, wewe ni nani unayesema pesa ipo?, wacha kupenda kutetea ujinga

Una matatizo ya kiakili sio bure. Sasa statement ya Kenya Medical Association kuhusu suala lingine ndio ushahidi wako kwamba hamna hela? Yaani hii hii Kenya ndio imevuruga akili zako kiasi hiki? Pole sana jombaa.
 
Sijamtetea mtu yeyote yule. Mimi nimewapa tu facts kama zilivyo, maanake wengi wenu huwa mna uelewa finyu kupindukia. Alafu kama kawa huwa hamsomi taarifa kwanza na mkisoma huwa hamuelewi chochote. Mgogoro kuhusu mswada ambao upo Seneti ni jambo ambalo kila mkenya analifahamu vyema. Lawama zote zipo kwa rais U.K na Rt. Hon RAO kwa 'interfence' yao kwenye masuala ambayo Seneti inafaa itoe maamuzi huru bila presha kutoka kwa mtu yeyote yule. Nashangaa sana kwamba hata kiswahili pia hamkielewi, au hamjaona haya yanayohusu gatuzi la Nairobi kwenye taarifa? ..."Mishahara yachelewa Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya
Mercy Mwangangi, anasema kuwa
mishahara ya madaktari ilichelewa
kwa sababu ya usimamizi mpya wa
jiji." :confused:
Why is it that doctors want establishment of a National health services Commission rather than work under counties?
Kenya's devolution has been nothing but tribal politics and corruption
 
Why is it that doctors want establishment of a National health services Commission rather than work under counties?
Kenya's devolution has been nothing but tribal politics and corruption
I support the doctors quest for a national outlook in the overall health services sector in Kenya. Apart from their work environment, standardization in all the parameters is needed across the health sector countrywide. Some county governments are not getting it right in their management of health services. Methinks the health services function should be balanced between the national and county governments in the longrun, for better delivery and more robust improvements in all the necessary areas.
 
Una matatizo ya kiakili sio bure. Sasa statement ya Kenya Medical Association kuhusu suala lingine ndio ushahidi wako kwamba hamna hela? Yaani hii hii Kenya ndio imevuruga akili zako kiasi hiki? Pole sana jombaa.
Wewe ni pimbi Sana, unaumwa utapia mlo wa ubongo, madaktari wenyewe wanasema serikali inawajibu kwamba haina pesa ndio sababu haijaweza kulipa madaktari kwa miezi mitatu mfululizo, wewe unataka ushahidi gani zaidi ya hiyo statement?, wewe unayesema pesa ipo unatumia ushaidi gani?.
 
Back
Top Bottom