Madaktari wa Muhimbili wanawadharau wagonjwa, hawawahudumii ipasavyo!

wantuzu

Senior Member
Nov 24, 2011
143
28
Ndugu zangu heri ya mwaka mpya 2016...

Ndugu zanga ni mwaka mpya 2016 na tuna kila jambo la kumshukuru Mwenyezi kwa kila jambo.

lakini binafsi nna jambo linalonitatiza na sijui kama linaweza kupata suruhu ya haraka nalo ni Hospitali ya Rufaa Muhimbili .

Muhimbili
ni hospitali ya rufaa kama wengi tujuavyo na inawataalam wa kutosha sote tunalielewa lakini tatizo linalowasibu wengi walowahi kuhudumiwa hospitalini hapo ni huduma haswa huduma toka kwa wauguzi mawodini... wauguzi wamekuwa hawawahudumii wagonjwa pindi wagonjwa hao wanapohitaji huduma yao, wengi mnalifaham hili kuwa mgonjwa anaweza apige yowe kuomba msaada mpaka akajifia baada ya saa kadhaa; wauguzi wapo kwenye chumba chao kana kwamba hakuna lililotokea...
ninacho tamani hapa ni kupata majibu sahihi ni kwa nini hawataki kufanya kazi kama taratibu za uuguzi zinavyo elekeza na labda niwe muwazi nimeamua kutumia njia ya kuuliza humu nikitarajia wamo wengi humu kwa majina mbadala so nawaomba wafunguke ili kama jamii tujuwe wapi pa kuanzia katika kulitafutia suluhu jambo hili
 
Kuna tofauti kati ya nurse na doctor na hata kazi zao ni tofauti japo zinategemeana. Kwenye tittle ya thread yako unawataja madaktari ila unachokizungumza ndani wauguzi. Usikariri kuwa kila mtu unayemuona hospitali ni daktari.
 
Sasa kwanini usiseme wauguzi kwenye heading yako mpk leo hujui tofaut ya dokta na muuguzi
 
Enz za kikwete hamkuyasema haya, maguful kawapa kiburi

Kiukweli kama ulishauguza mgonjwa kupitia Muhimbili Hospital utamuelewa mtoa mada ana maanisha nini! Kama hujawahi kaa kimya pita pembeni; kwa muhimbili huduma hutolewa kwa kujuana sana au kama unakata pochi ya kueleweka. Sio kwa madaktari wala nurses wa wodini.
Huwa nafika mahali najiuliza ni kwamba madaktari ni wachache sana kulinganisha na idadi ya wagonjwa au ni kibri tu cha madaktari kwamba wanafanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili?

Kiukweli madaktari na nurses wa Muhimbili wanatakiwa kujirekebisha. Serikali nayo inatakiwa kuongeza hizi hospitali za rufaa pamoja na wataalam ili kupunguza msongamano pale Muhimbili.
 
kwanza umekosea heading....rekebisha hili ueleweke.sifanyi kazi huko wala sijui mazingira yaliyopo huko but katika system kuna kitu huwa tunakosea kama watanzania in general,kama ulivyosema that is a refferal hospital tena ni national hospital kwahiyo wao walitakiwa only to attend refferal cases na so kila Mgonjwa anayeamua kutibiwa pale bila refferal.tunawapa mzigo mkubwa sana kuhudumia referred and non referred cases wakati wengi wetu tungeweza tibiwa katika hospitali za wilaya husika.so lazima wawe overloaded na in one way or another wakizidiwa workload hata patient care inapungua,kumbukeni they are also humans.
 
Pole Sana Mleta Mada
Tunajua Tulio Wengi Uchungu Na Ugumu Wa Kuuguza Ndugu Jamaa Na Marafiki, Inauma Nami Naungana Na Mleta Mada Tujibuni Taratibu Tuelewe
 
Kuna wakati unaweza kuona hivyo kuwa hawafanyi kazi ipasavyo lakini kiuhalisia wanajituma sana ila ni masaa mengi wanayofanya ndio wanakuwa knackered
 
Hii tabia ndio inawafanya hata wauguzi na madaktar waafrika weusi katika hospitali nyingi na huduma za afya ulaya wasiaminike kabisa.

Kuna madaktar na wauguzi waafrika ulaya very smart na weledi ila ngozi yao tu na imani wazungu wamejijengea kutokatana na ethics mbovu za kazi kama hao muhimbili zinawapa sana changamoto kazini.

Sisi tunaishi kimungumungu tu ndio maana wenye hela zao kamwe hawathubutu kutibiwa muhimbili. Hospitali shule na vyuo vimejengwa kwa walalahoi kama fadhila na huko kuzijenga ni deal pia kwasababu kila mradi nchini mafisi wamegeuza deal iwe sekta ya afya elimu yani kila kitu.

Hii kamwe siyo nchi ya kujivunia chini ya mfumo kandamiz na fedhuli
 
Tatizo ni kwamba wanasiasa wameweza kuwaaminisha wananchi kuwa ubovu kwenye sekta ya afya ni kwa sababu ya uzembe wa wahudumu wa sekta ya afya. Ukweli ni kwamba pamoja na mapungufu waliyonayo lakini wahudumu hawa ambao wanaonekana kama hawana maadili na hawathamini afya na utu wanajitahidi kufanya kazi katika mazingira mabovu yasiyo na vitendea kazi na kutothaminiwa. Serikali isijifiche kwenye mgongo wa madaktari na wauguzi,ifanye jitihada za dhati ili kuboresha huduma za afya kwa kutilia mkazo mafunzo ya masomo ya sayansi ili kupata idadi kubwa ya wataalamu, iongeze idadi ya wanafunzi wa shahada za juu kuliko hali ilivyo sasa, ijenge hospitali kubwa zilizo na vifaa na madawa ya kutosha kanda ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaokuja muhimbili kufuata huduma za afya vinginevyo chuki za wananchi kwa watoa huduma ya afya hazitoisha kamwe.
 
hata kwenye makosa ya serikali wanasingiziwa madaktari na manesi.
serikali haileti dawa ooooh! madaktari wanaiba na kupeleka kwao.
serikali haileti vitendanishi, ooooh!! madaktari wanaiba.
jamani tuweni wakweli. serikali ya kikwete imefanya sana usanii kwenye sekta ya afya.
walichofanya wao ni kupokea msaada wa ujenzi wa kitengo cha moyo pale mnh kutoka korea basi.
hata vifaa vingine vilivyotakiwa kuwemo vilichakachuliwa na kuibiwa.
hakuna vitendanishi na vitendea kazi.
hospitali ni shida. kuna wakati nurse inabidi azunguke wodi zote kutafuta gloves tu ili amhudumie mgonjwa.
huyu mtu anapatwa na hasira hata moyo wa kuhudumia watanzania unapotea.
just imagine bajeti ya mnh labda ni bil 3 kwa mwaka na mmeletewa m 250 tu aafu mnakuja kusikia kuna mtu kaikosesha serikali mapato ya billion 80.!!!
inatia hasira.
 
Hilo Jipu nalo litumbuliwe, hivi kwa nn madaktari wengi wananata sana? Wanajisikia sana? Mbona wanakufa? Mbona wana#nya? Mbona wa matatizo kama watu wengine? So whatz so special to them?##ushamba#ulimbukeni#ugoroko
 
Back
Top Bottom