GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,865
Mmesemwa sana ila hamsikii na leo ‘ nawachana ‘ live / mubashara humu JF kuwa tafadhalini hebu tofautisheni basi kati ya Kung’oa misumari katika Mabati na Kung’oa Meno yetu haya yaliyo katika midomo yetu.
Nyie ndiyo Madaktari pekee wa meno hapa nchini ambao mnamfanya Mgonjwa wa meno kabla ya kuja Kwenu kwanza huko huko alipo aanze Kusali sana kwa Mwenyezi Mungu ili ampe nafuu ya maumivu au inambidi huyo Mgonjwa kabla ya kuja Kwenu ahakikishe amenunua dawa zote za kutuliza maumivu kwani akija tu Kwenu hawezi kutoka salama.
Ili muone mlivyo na matatizo kwanza mnavyompokea tu Mgonjwa anayetaka Kung’oa meno kwenu tayari ni ‘ adhabu ‘ tosha kwani kuwa mnakuwa na ‘ jazba ‘ sana na sasa ‘ shughuli ‘ nzima Mgonjwa atakutana nayo huko ndani akiwa anang’oa jino lake.
Wengi wenu mkiwa mnatung’oa meno yetu huwa mnakuwa mmenuna ( Sura Limao ) halafu hata hivyo Vifaa vyenu huwa mnaviingiza katika midomo yetu kwa nguvu kubwa utadhani ‘ Dereva ‘ wa Lori anaweka gia ili apandishe vizuri Mlima Kitonga.
Na ndiyo maana siku hizi mnakimbiwa mno na Wagonjwa wa Meno na mnawapata tu hao Mangumbaru / Washamba ambao hawawajui ila hata wao wakishapata ‘ maumivu ‘ yenu nao ‘ hujanjaruka ‘ na kusepa Hospitali zingine.
Nimewaheshimu sana na sitaki niwaharibieni Kazi ila najua kwa uzi huu ‘ Madaktari ‘ husika mtakuwa mmejijua japo hata kwa majina yenu nawafahamu ila leo nawaweka ‘ Viporo ‘ nikiwa na matumaini makubwa kuwa baada ya GENTAMYCINE leo ‘ kuwashtueni ‘ basi mtabadilika upesi na kuanza Kutung’oa meno Kiutaratibu, Kiumakini na Kiurafiki kabisa.
Hospitali ya Amana ni nzuri sana na inafanya vyema ila tatizo kubwa lipo tu kwa hao wang’oa misumari / wang’oa meno wenu ambao kiukweli wanatuachia ‘ Maumivu ‘ na ‘ Majeraha ‘ makubwa mno sisi Wagonjwa wa Kutukuka wa Meno.
Shikamooni Madaktari wote wa Meno wa Hospitali ya Amana!
Nawasilisha.