Madaktari wa Boston wafanikiwa kupandikiza uume!!

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,166
b84e4cccb40021133c9c9a8e4f1ec2ef.jpg

Hospitali moja mjini Boston imekuwa ya kwanza nchini Marekani kufanya upasuaji kupandikiza uume.
Thomas Manning mwenye umri wa miaka 64 alipatiwa kiungo hicho baada ya kugundulika kuwa uume wake uliathirika na saratani.
Madaktari wamesema zoezi hilo limefanikiwa na kumfanya Manning kuwa mtu wa tatu dunia nzima kufanyiwa upasuaji huo. Mmoja wa madaktari waliofanya upasuaji huko Boston ni Dicken Ko, amesema wanaume wanaopoteza maungo yao hupata athari za kisaikolojia kwa kuwa ni maeneo nyeti yanayoathirika wengi wao hawapendi kufahamika hadharani.
 
Hii ni nzuri ingawa kwa Watz hapo wataanza kufikiria kupandikiza uume mkubwa tu!
na sio kwa matatizo, maana ndo story zao vijiweni.
 
Wamesema kuwa wamempandikiza uume lakini hawajasema kama unafanya kazi au la?

Usikute kawekewa kama pambo tuu.
 
Hii ni nzuri ingawa kwa Watz hapo wataanza kufikiria kupandikiza uume mkubwa tu!
na sio kwa matatizo, maana ndo story zao vijiweni.

heh heh naona kesi za kutumia vilevi zitapungua mtaani,watashindana kuchagua dushelele kubwakubwa
 
lakini tujiulize huo mpya unapatikana wapi!?.
Kama kwa 100% baada ya upasuaji mashine inafanya kazi, Organs zitakuwa zinavunwa kutoka kwa waathirika wa ajali na magonjwa yasio hatarishi sana then inahifadhiwa kusubiri wateja.
 
Kama kwa 100% baada ya upasuaji mashine inafanya kazi, Organs zitakuwa zinavunwa kutoka kwa waathirika wa ajali na magonjwa yasio hatarishi sana then inahifadhiwa kusubiri wateja.
biashara mpya soon to start taking place!
 
Karibu kiumeni kuna mabaradhuli yanajiondoa huku pongezi kwako kwa kuongeza idadi ya marijali duniani.
 
Back
Top Bottom