Madaktari tafadhari rudini kazini mnawauwa wasio na hatia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari tafadhari rudini kazini mnawauwa wasio na hatia...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gango2, Feb 8, 2012.

 1. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,229
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Ni kweli mmegoma, hakuna ambaye hajawasikia, but kwa kufanya hivyo hammuikomoi serikari wala pinda wala dr mwinyi au kikwete bali mnawakomoa wananchi wenzenu, either jirani yako au ndugu yako.

  cha msingi ni moyo wa huruma na upendo. Natumai wengi wenu ni waumini makanisani na misikitini, sidhani kama kunamsikiti au kanisa linalofurahia kitendo chenu hicho, ni cha kinyama na ki- uaji kabisa.

  nanyi wana JF sometimes tuache ushabiki, najua wengi wenu mnauwezo wa kupata vijisent vinavyoweza kuwapeleka regency or mikocheni hosp na hosp nyingine za binafsi, bt kunawatu hawana uwezo huo jamani.

  tafadhari hebu fikeni pale muhimbili mshuhudie watu wanavyopata tabu kwa sababu ya mgomo huu, narudia tena hatumkomoi PINDA hapa tunajikomoa wnyewe. SERIKALI yetu ni wauwaji tumeshawaona hawana nia ya kutusaidia, ni nyie ndo mnaoweza kuokoa maisha ya hawa watu.

  pia kumbukeni kuwa kunasoko huru la ajira kwa sasa jamana, wakati wanafanyia kazi mahitaji yenu, mkiona wanachelewa achaneni nao, tafuta sehemu unakofikiri wanalipa vizuri, MUHIMBILI pana vifaa vingi ambavyo havipatikani sehemu nyingine so kama unaparticle za kugoma goma kushinikiza mshahara kupanda its better ukaacha kazi waingie wale wenye moyo wa kujitolea kutumia rasilimali za hospitali kuokoa maisha ya walala hoi

  pia kumbukeni nchi yetu masikini sana, kuanza kuomba mishahara ya juu, mtatengeneza gaps na watumishi wwengine wa uma. so chondechonde rudini kazini.

  Gango...!!!
  dsm
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Watanzania wana hatia, waliaambiwa kuchagua ccm ni janga la kitaifa bado wakaichagua, wiki mbili watu wanakufa hakuna aneandamana kuhoji serikali wote tumeridhika, wanaobomoa nchi hii ni watanzania ambao wewe unasema hawana hatia
   
 3. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ...Gango, hakuna dakatri anayefurahia hali hii inayoendelea sasa hivi, lakini hii ndi njia pekee iliyobaki. kwa wananchi wanaoona madai ya madaktari ni ya msingi la kufanya ni kuunga mkono harakati hizi .(kama walivyofanya wanaharakati leo). Watu wengi mnakimbilia katika kujadili mishahara na kusema madaktari wanadai mishahara mikubwa. kama kuna watumishi wanaoridhika na mishahara wanayopata (i.e. wanaamini kuwa kwa ujuzi/elimu yao na mazingira ya kazi yao wanapata stahili yao) hilo lisihusishwe na mgomo huu. madakatari wametafakari na kutazama vigezo vingi na kufikia conclusion kuwa wanapaswa kuongezwa mishahara. Serikali inachopaswa kusema ni kuwa 1. haina uwezo wa kuongeza mishahara hiyo hivyo asiyetaka kazi aache 2. Inakubali kuwa mishahara ni midog hata hivyo haina uwezo wa kuongeza kufikia kiwango wanachotaka madaktari na serikali itaje uwezo wake. Kuhusu kutengeneza gap na watumishi wengine sio sababu/hoja yenye nguvu; Nikuulize wanawezaje kuwalipa mishahara mikubwa watumishi wa benki kuu, TRA na kadhalika? Ipo namna; pengine nikufamaishe kuwa sababu inayowafanya madaktari leo wawe na tofauti kubwa na watumishi wengine waumma wanapoanza kazi ni kwasababu daktari huanza kazi kama afisa wa ngazi ya kati, hivyo hata leo wanaweza kubadilisha cheo cha kuanzaia kazi na mishahara ikapanda (wao wanajua zaidi).
  HURUMA KWA WAGONJWA:
  Wengi wetu hatufahamu, lakini madaktari Tanzania wanafanya kazi ya kujitolea mno nitakupa mifano miwili
  1. Daktari anapoitwa usiku kuja kuhudumia mgonjwa(baada ya masaa ya kazi) mara nyingi anagharamia usafiri wake kuja na kurudi nyumban unaweza kukokotoa gharama ya mafuta kwa daktari anayeishi Sinza kwa mfano.
  2. Dakatari anayefanya saa za ziada (on call) kwa massa za ya 24 analipwa shs 10,000. Ni watumishi wangapi wa umma wanaofanya overtime ya kiasi hicho.

  Mara nyingi sipendai kuzungumzia experince yangu binafsi katika hii kazi kwa kuwa it is so painful (na kwasababu hiyo niliamua kuacha kuona wagonjwa)...kujitoa kuhudumia wananchi katika mazingira magumu na hatarishi wananchi ambao siku zote wanalaumu tu madaktari wana tamaa ya hela, n.k

  Katika hili la mgomo msimamo wangu ni kuwa ni madaktari wasilaumiwe katika yote yanayotokea, ni wakati sasa wa serikali kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuacha ubabaishaji!
   
 4. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yaani wewe kwa akili yako unaona wamegoma ili kumkomoa mtu? Kweli safari bado ndefu, kaka wale hawajagoma ili wamkomoe mtu, wanadai maslahi yao.

  Na usiseme habari za huruma, watanzania wenyewe ndio hatujihurumii, haya yanatukuta kwa sababu ya kuipenda CCM ambayo viongozi wake wameshajiona kama miungu hapa duniani.

  Shida yenu badala ya kuilaumu serikali inayowatibua madaktari, nyie mmekazana kuwalaumu madaktari. Kwani wao waliwaambia wanasoma ili washike usaha na makohozi yako kwa hobby?
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Madaktari,walimu,Jeshi,idara ya mahakama kisha watafuatia makarani ndio nasi tumalizie...R.I.P dada yetu Ireen...umeondoka tungali tukikuhitaji...perhaps Mungu alikuepusha usije zaa Daktari ama mwanasiasa!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ATHARI ZA UNAFIKI NA UMBUMBUMBU.... No pain, no gain
   
 7. s

  sugi JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Shut up!walijiweka madarakani hao vigogo???,t shirt na kofia zitawatibu,eee watanzania tupate akili!
   
 8. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,229
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  acha ushabiki hapa bana halihitaji siasa za ccm wala cdm now, haisaidii kitu kuanza kushabikia now!!!!
   
 9. A

  AMKA Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Good for Drs ili watanzania tujifunze mana tumezoea sana kupewa tisheti kofia na khanga haya viuzeni sasa mwende kutibiwa nje na nyie. SOME PEOPLE CAN NOT LEARN A LEASON UNLESS THEY KIKED HARD
   
Loading...