Madaktari Sita kutoka Misri wawasili nchini kusaidia matibabu Muhimbili.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

Jumla ya madaktari sita na wataalamu wawili, mmoja wa teknolojia na mwingine wa utawala kutoka Misri wamewasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa tundu ndogo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dare es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa madaktari hao.

“Madaktari hawa watasaidia kutoa tiba na kuwafundisha madaktari wetu utaalamu huu, hivyo ujio wao utasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kwenda nje ya nchi,” amesema Dk. Mwinyi.

Ameongeza kuwa madakatari hao watakuwepo katika hospitali hiyo kuanzia Juni 10 hadi 15, mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma hizo. Dk. Mwinyi aliushukuru ujio huo kwa kuwa utasaidia kubadilishana uzoefu na teknolojia na kuboresha afya ya Watanzania.

Kwa upande wake, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Hossam Omar alisema ujio wa madaktari hao ni kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta hiyo, ambapo watauendeleza katika maeneo mengine ya sekta hiyo na nyingine.
 
Matatizo ni MADAKTARI au ni kuwatunza MADAKTARI wetu kuwapa MISHAHARA MINONO; MARUPURUPU; SERIKALI kununua Vyombo BORA HOSPITALINI

Na sio kuleta Madaktari toka nje ambao wanaweza kuwa sio BORA kama wakwetu... na tutawalipa hao wa nje Mishahara Minono Majumba mazuri...
 
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

Jumla ya madaktari sita na wataalamu wawili, mmoja wa teknolojia na mwingine wa utawala kutoka Misri wamewasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa tundu ndogo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dare es Salaam.

Huo ugonjwa wa tundu ndogo ni ugonjwa wa moyo?
 
miaka 50 ya uhuru bado tunaomba madaktari kutoka nchi za nje kweli ukistaajabu ya musa..... kwa sasa nchi yetu ilitakiwa iwe na wataalu waliojitosheleza kwa kila nyanja lakini ndio kwanza tunaimba wataaalam kutoka nje ya nchi tukiwa na rasilimali nyingi za wataalam ambao hatuwaandalii mazingira ya kuwawezesha kusoma na kupata utaalamu wa kuweza kusaidia taifa. kinachobaki ni bla bla tu na kuwa omba omba ni aibu sana kwa taifa letu.
 
Mkuu sio madaktari tu, bali hata walimu wa sayansi. Tumemsikia mkuu wa kaya akiomba kutoka Japan, just baada ya miaka 50 ya uhuru. Yaani tunaomba kuanzia pesa hadi rasilimali watu!
 
I guess... nadhani tuna hao ma-specialist KIKWETE alisema alikuwa anapeleka Madaktari Nje kimya kimya Nje Kusoma -- Sasa hawakurudi? ndio wanakimbilia WaMisri?

ukiangalia gharama zilizotumikakuwaleta hao madaktari unanunua vifaa kwa ajili ya laparascopic surgery kwa hospitali zote za zonal referals
 
Hapa si bure kuna uchafu umejificha! Siamini kuwa its a genuine visit. Kama ni kubadilishana mawazo basi wawkaribishe na Madaktari wetu waende huko kwao. Huu ni upuuzi wa kisiasa. Mwinyi anadhani watanzania wa leo ni wajinga kama yeye kwa kukubali huo ujinga ndani ya miaka 50 ya Uhuru?
 
Na huku zanzibr pia kuna wagonjwa,hao madokta watatu waje kutibu na huku.
 
Matatizo ni MADAKTARI au ni kuwatunza MADAKTARI wetu kuwapa MISHAHARA MINONO; MARUPURUPU; SERIKALI kununua Vyombo BORA HOSPITALINI

Na sio kuleta Madaktari toka nje ambao wanaweza kuwa sio BORA kama wakwetu... na tutawalipa hao wa nje Mishahara Minono Majumba mazuri...
Madaktari wa kwetu ni wazuri sana ila maskini wanakosa vifaa sahihi vya kufanyia kazi. Sasa hao Wamisri wakondokaa wataacha hivyo vifaa vya upasuaji au wataondoka navyo? Hata kuomba walimu kutoka nje sina uhakika kama ni ufumbuzi wa tatizo lililopo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom