Madaktari Sawa Watatoka Cuba, India na China. Manesi Je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Sawa Watatoka Cuba, India na China. Manesi Je?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NdasheneMbandu, Mar 8, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Serikali ipo kwenye hatua ya mwisho ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuleta madaktari kutoka nchi za Cuba, India na Cihina ili kuziba pengo kubwa lililoachwa na madaktari watanzania ambao wamegoma. Ninachojiuliza ni je, madaktari hao wa nje watalipwa na nani na watakaa hapa nchini kwa muda gani? Na je, manesi nao wakiamua kuwasindikiza madaktari, Serikali itafanya nini? Italeta manesi wengine kutoka nje?

  Maswali haya na mengine mengi, yananielekeza kuamini kuwa suluhisho la suala hili ni kwa Serikali kuamua KUSHUKA kwa rais kukubali kuwastaafisha mawaziri wake kwa maslahi pana ya umma. Wapo wanaosema kwamba rais akifanya hivyo, atakuwa amejishusha sana. Lakini tujiulize, hivi ni nani mkubwa kati ya rais na wananchi kwa ujumla wao? Kwa nchi inayoheshimu utawala wa demokrasia kwelikweli, rais lazima atajiona kuwa yeye ni mtumwa wa wananchi wake. Kwa hiyo, inapotokea kelele za wananchi wake ambao ndiyo waajiri zimezidi, lazima achukue hatua hata kama wakati mwingine hafurahi kufanya hivyo. Asipofanya hivyo, kama ilivyo sasa kwa kikwete, ataendelea kuwatesa wananchi na kuwasababishia vifo ambavyo kimsingi vingeweza kuepukika.

  Kauli ya anayejiita 'Mtoto wa Mkulima' Bw. Mizengo Pinda kwamba madaktari wanafanya makosa kumpa masharti BWANA MKUBWA yaani kikwete, imeniudhi sana. Ni kauli inayoashiria kibuli cha viongozi wa kiafrika. Kwamba rais ni bwana mkubwa asiyeweza kulazimishwa na mtu yeyote kufanya jambo fulani. Hili ndiyo tatizo la msingi la viongozi na hasa wa ccm kujiona kuwa kama MIUNGU MTU. Kwangu mimi, kiongozi anayefuata MATAKWA YA WANANCHI huyo ndiye kiongozi mzuri. Asipofanya hivyo, atuambie anafanya kwa maslahi ya nani!
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Hawa madaktari waliogoma imekula kwao kudadadeki. Hizo mil. 3 wanazotaka watazisikia kwenye radio sasa.
   
 3. Zurii

  Zurii Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania hawajaelewa ukweli kuhusu madai ya Madaktari. Its not about the money. Kuna recognition ya mchango wao kwenye taifa. Kupotea kwa thamani ya profession ya Udaktari. Ilifikia kiwango yule Mama anawaambia eti Nani aliwatuma mkasomee udaktari. Its about time the country places priority and value to this special and rare profession. From working environment to supportive facilities Waache siasa wasolve matatizo yanayo wakabili madakatari kitaalamu. Kwani
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  hao madaktari waje na vifaa vya kazi
   
 5. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata wahamishe majengo yao huko waliko na kuyaleta hapa nchini, bado it is not going to be sustainable. Kwa mfumo wetu hovyo wa kiutendaji, lazima nao watachoka tu.
   
 6. Zurii

  Zurii Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa nakubaliana na wewe asilimia 100% au wanakuja na vifaa kutok ahuko kwao? Hivi hii nchi yetu na hawa viongozi kweli wana akili sawa sawa? So wanataka kuprove kwamba hela ipo ila ni bora apewe mchina na mcuba kuliko kumba mtanzania! Ovyo sana
   
 7. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais kwamba kumchagua kikwete na ccm yake ni sawa na kukaribisha janga la kitaifa. Now, I am beginning to learn the context and meaning of Dr. Slaa statement.
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Nukuu pia alisema nchi haitatawalika
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Too late. Ushabiki wa Wanaharakati, wanasiasa na hata baadhi ya watu wengine wa kawaida kabisa hata ambao hawana uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya Kata zao hatukuliona kama hilo ni tatizo lililochangia kukua kwa hamasa ya madaktari kugoma. Tuache Serikali itekeleze majukumu yake. Tukianza kuhoji kama Serikali itaweza hayo sasa majungu. Suala la wageni watalipwa shilingi ngapi , ni lazima tukubali hizo ndizo gharama zenyewe hasa pale wazalendo wanapokosa uzalendo. Ikibidi sasa hata mishahara ya Watumishi ipunguzwe zaidi ili kukabiliana na tatizo , hii ni kama vita huwezi kukwepa uwe unaunga mkono mgomo au la. Letu sote.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika mgomo huu SLAA ni mtuhumiwa numba moja. Asijifanye kukaa kimya kana kwamba wananchi hawajui hilo.

  Mambo yakizidi kuwa mabaya asifikiri atapona , wananchi wataanza naye si alishasema kwamba nchi haitatawalika? kwa nini abaki? Kwanza yupo au kishakimbilia Karatu.
   
 11. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Serikali makini haijidanganyi kwa kuwa na mipango ya dharura ambayo inaharibu bajeti ya Nchi
  bali inakua makini kwenye kutatua matatizo hayo kiumakini
  umeme wa Dharura umechukua kipindi kizima cha urais wa jk na sasa madaktari wa dharura kama
  wataletwa sijui itakuaje "Mungu ibariki TANZANIA,Mungu ibariki Afrika"
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Huku ndo kudandia gari usojua laenda wapi, unajua madai yao ya msingi kweli? Si lazima kila thread uchangie hasa kama huelewi mada!!!!!
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tumelalama mgomo mgomo, umeanza sasa wasiwasi wetu nini Malengo yetu si yametimia? Tusiisakame tena Serikali. Tuliotaka kuwafurahisha tumeshawafurahisha. Nilifikiri sasa humu JF tungekuwa tunashangilia mgomo kuanza kwa akili zetu finyu tulivyokuwa tukiunga mgomo bila hata haya. Sasa mbona tunachangia kama tumeingia na hofu fulani? kwa nini tusiwe na ujasiri uleule?
   
 14. K

  Koffie JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kadandia vipi sasa? asitoe maoni yake? hao madaktari wasiwe kama watoto wadogo ambao wana demand kitu papo kwa papo,, naunga mkono serikali kuleta madaktari mbadala, tuone watakula wapi. Tusitake kunyanyasa wananchi hapa kisa eti daktari!! Na sisi wabeba zege tukigoma nani atawajengea majumba yenu? acheni upuuzi. Piga chini hao
   
 15. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unauza ng'ombe ili kushinda kesi ya kuku
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,232
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo hela za kuwalipa madaktari wa cuba wanazo ila za kuwalipa madaktari wa hapa hawana?
  na hao madaktari wataenda mpaka nanjilinji au wataishia muhimbili?

  ama kweli akili ni nywele..........
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanadai Mawaziri wajiuzulu. Yaani Madaktari bwana thehe thehe thehe, kwa hiyo wasipojiuzulu watoto wa Madaktwari haya hawatakwenda choo? Kazi kweli kweli. Daktari acheni hizo bwana. Mnajua kazi yenu kama kazi nyingine tu. Hivi Daktari ukipewa kazi ya kutengeneza hata stuli utaweza kweli? ukiambiwa umfundishe mtoto wa miaka mitatu hadi ajue kusoma utaweza? ukiambiwa kazi yako ni kuimba kwenye jukwaa ili watoto wako wapate kula utaweza? ukiambiwa ukatembee na viatu unauza mitaani kutoka Igoma hadi Nyakato, Ghana hadi Kirumba utaweza kweli Daktari? Basi hivyo wenzenu tunavyoteseka kuhakikisha familia zetu zinaishi. Kazi yenu kama kazi zingine
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hueleweki. Kapumzike kwanza.
   
 19. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Du,hii imekaa vizuri,ngoja nijiandae kuomba post ya ukalimani muhimbili,maana najua nafasi zitakuwa nyingi kwa sisi ambao ni billingual,hao madaktari wa Cuba na China kila mmoja atahitaji mkalimani wa kukaa naye wakati anamsikiliza mgonjwa wa kibantu,pia prescription ya Kichina manesi na watu wa Pharmacy watahitaji wa kuwatafsiria.Nadhani ahadi ya kuongeza ajira kwa watanzania itakuwa imetimia.Kidumu chama cha mapinduzi.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hilo wa si la dharura , Maktari walifikiri wao tu ndiyo wamesomea fani hiyo. Big up Government.
  Sisi tuendelee na majungu yetu humu JF wakati Serikali ikiwajibika.
   
Loading...