Madaktari Ocean Road watoa tamko kuunga mkono Mgomo; Waweka vifaa chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Ocean Road watoa tamko kuunga mkono Mgomo; Waweka vifaa chini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mayoscissors, Mar 8, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Baada ya kikao cha madaktari wanaofanya kazi katika taasisi ya saratani ya ocean kuhusu mgomo unaoendelea wa madaktari kote nchini, tumeazimia mambo yafuatayo:

  1. Sababu za mgomo wa madaktari ni za msingi.
  2. Maamuzi na majibu ya serikali hayatoshelezi,hayaridhishi na hayakidhi mahitaji ya madaktari.
  3. Kutokana na haya tajwa hapo juu,sisi madaktari wa ocean road tunaungana na madaktari wote nchini kusitisha utoaji huduma mpaka hapo ufumbuzi utakapopatikana.

  Tunawaomba radhi sana wagonjwa wetu wapendwa kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ni matarajio yetu kuwa huduma zitakuwa BORA ZAIDI baada ya kipindi hiki kigumu.

  Wenu katika utumishi wa umma,
  MADAKTARI WA OCEAN ROAD.
  08/03/2012
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mnawaomba radhi wakati mnajua watakufa na saratani? Muwapelekee ujumbe makaburini.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Tumewasikia tutakuja Aga Khan Hospital au Regency Hospital. si ndio mnataka hivyo.
   
 4. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kabla ya kwenda kukutana na wazee wa gerezani kesho, jk apeleke w.akw.ere ocean road kupiga mionzi wagonjwa wa kansa...sijawahi ona serikali ya mafirauni kama hii!
   
 5. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sawa madaktari mm cpingi mnachodai ni haki yenu ya msingi
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Jamani hii inasikitisha sana, imagine mgonjwa wa saratani anaposoma habari hii. Pinda do something.
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

  JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  badala ya kushughulikia tatizo kwa kuongea na madaktari wao wanabaki kusambaza propaganda kwa wananchi kitu ambacho kinachochea mgomo zaidi
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwa nini asiende kuhutubia wagonjwa pale muhimbili??
   
 10. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya madaktari wangu, twende kazi.
   
 11. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Msianze kuwa wapole shikilieni msimamo wenu wa kumshauru rais awafukuze alete wale wa kichina mnaosema.
   
 12. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako ni kudhani kila mmoja anaweza kuwa Daktari...
  Hapo tu....
   
 13. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  eti walahi ...ungefanya nini unadhani wale ni wakwea nazi wa bagamoyo kuwa utapata wengine kesho..
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  wanataka muende Samunge kwa babu
   
 15. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mtu akiwa zoba unamsifu ana hekima! Nadhani si ajabu nawe waweza kuwa zoba kama yeye.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa,mtatukuta ahera.mmesoma kwa kodi zetu sasa mmetusaliti
   
 17. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  tataona hizo ngojera na kang za kesho ukumbini
   
 18. R

  RMA JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakulaumiwa ni utawala mbovu wa kifisadi wa ccm!!
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hii ni wazi kwamba wasomi wa tanzania wanawasaliti wasiosoma.
   
 20. k

  king11 JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo si madaktari tatizo ni wananchi sisi hatuna mkataba na madaktari bali tunamkataba na serikali ambayo ndio tumeiweka madarakani hivyo basi tunatakiwa tuwaambie serikali wahakikishe tunapata huduma ya afya pasipo kujua kuwa madaktari wamegoma au lah....hatuna mkataba na madaktari bali tunamkataba na serikali wakishindwa kutoa huduma ni wakati wa kuiwajibisha
   
Loading...