Madaktari ni nini suluhisho la kudumu la ugonjwa wa dermatitis?

oladipo

JF-Expert Member
Mar 8, 2022
1,421
2,286
Wakuu habari za asubuhi?

Ni muda wa miaka miwili sasa nimekuwa nikisumbuliwa na huu ugonjwa wa ngozi ujulikanao kitaalamu kama dermatiris au eczema. Nishaenda hospital zaidi ya mara tano na kuandikiwa dawa mbalimbali lakini umekuwa ukijirudia mara kwa mara

Nimejitahidi kufata masharti niliyopewa na bado siponi na mbaya zaidi kila ninapoamka uso unakuwa umetandwa na utando mweupe japo limekuwa linanikera sana

Je, ugonjwa huu una tiba mbadala inayoweza kumaliza kabisa huu ugonjwa au hauna tiba ya kudumu!

Kwa anaejua please naombeni msaada wa tiba

Eg ugonjwa huu unanitokea maeneo ya usoni pekee yake.
 
Pole sana.
Suala la kwanza ni kuelewa msingi wa tatizo lako:

1: Mfumo wako wa mwili kupigana na baadhi ya vitu unavyokutana navyo kwa kugusa au kula na hatimaye kukuletea tatizo husika.

2: Ngozi yako kutokuwa imara sana kuhimili mabadiliko yanayotokea nje ya mazingira ya mwili.

3: Ni kutambua kuwa tatizo hili ni la kudumu kwa maisha yako, ni suala la kujua na kutathini jinsi ya kuishi nalo.

Suluhisho au kupata unafuu:

1: Kuelewa kwa mazingira uliyopo vitu vinavyotatiza mwili au ngozi yako ambavyo unaweza kubadili/modifiable risk factors. Mfano: Nyama, karanga, blueband, samaki, aina ya nguo, mazingira ya kazi, stress, unene uliopitiliza nk.

2: Kutambua hali ya kimazingira ambayo huwezi kubadili/non modifiable risk factors. Mfano: mabadiliko ya hali ya hewa/seasonally, unyevunyevu/humidity, pollen.

3: Matumizi ya mafuta yanayoendana na hali ya ngozi yako. Mfano: Epimax au Ezera moisturiser zimeonekana kufanya vyema kwa watu wengi

4: Matumizi ya dawa zinazotumika kutibu tatizo husika.

5: Matumizi ya sabuni za kuogea zinazoendana na hali yako. Mfano: sabuni ya dove imeonekana kufanya vyema kwa watu wengi.

Kuwa na ufuatiliaji kwa daktari mmoja hasa bingwa wa ngozi au aliyeonyesha kulielewa na kukuhudumia vyema kwa tatizo lako ni jambo jema pia.

Ukiunganisha vyote hapo juu, matokeo huwa ni mazuri kuliko ukijikita kwenye kutibu kwa dawa tu.

Pia, unaweza kuhitaji kuwa na sehemu ya kuandika ni mara ngapi unapata tatizo, limedumu kwa siku ngapi na vitu unavyotumia na dawa uliyotumia ili kuwa more objective.
 
Pole sana.
Suala la kwanza ni kuelewa msingi wa tatizo lako:

1: Mfumo wako wa mwili kupigana na baadhi ya vitu unavyokutana navyo kwa kugusa au kula na hatimaye kukuletea tatizo husika.

2: Ngozi yako kutokuwa imara sana kuhimili mabadiliko yanayotokea nje ya mazingira ya mwili.

Suluhisho au kupata unafuu:

1: Kuelewa kwa mazingira uliyopo vitu vinavyotatiza mwili au ngozi yako ambavyo unaweza kubadili/modifiable risk factors. Mfano: Nyama, karanga, blueband, samaki, aina ya nguo, mazingira ya kazi, stress, unene uliopitiliza nk.

2: Kutambua hali ya kimazingira ambayo huwezi kubadili/non modifiable risk factors. Mfano: mabadiliko ya hali ya hewa/seasonally, unyevunyevu/humidity, pollen.

3: Matumizi ya mafuta yanayoendana na hali ya ngozi yako.

4: Matumizi ya dawa zinazotumika kutibu tatizo husika.

5: Matumizi ya sabuni za kuongea zinazoendana na hali yako.

Ukiunganisha vyote hapo juu, matokeo huwa ni mazuri kuliko ukijikita kwenye kutibu kwa dawa.
Pia, unaweza kuhitaji kuwa na sehemu ya kuandika ni mara ngapi unapata tatizo, limedumu kwa siku ngapi na vitu unavyotumia na dawa uliyotumia ili kuwa more objective.
Ahsante sana mkuu
 
Back
Top Bottom