Madaktari na Polisi: Wachukuliwe hatua stahiki kwa makosa ya utendaji wao

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
780
Pamoja na jitihada kubwa za madaktari wetu za kuokoa maisha ya watu kila siku. Na pia jeshi la polisi kwa kulinda raia na mali zao. Nawapongeza wote kwa kazi nzuri wanazofanya kila siku.

Lakini pia kumekuwa na makosa mengi ya utendaji wa madaktari na wasaidizi wao kupelekea vifo vya watu na wagonjwa wengi bila ulazima. Na pia kwa polisi wamekuwa wanafanya mauaji ya watuhumiwa yasiyo ya lazima. Hivyo kupelekea manung'uniko mengi kwa jamii na hasa watu wenye uwezo mdogo wa mali na elimu.

Ambao hawana uwezo wa kufuatilia kujua viini vya vifo au kulazimisha uchunguzi wa vifo vya ndugu zao kufanyika na ripoti kupatikana. Kama uchunguzi utakuwa ukifanyika baadhi ya madaktari hawa wanaweza kufungiwa au hata kufunguliwa mashtaka ya jinai.

Itategemea kesi na kesi sababu baadhi ya wagonjwa licha ya kufa wengine wanaachwa na vilema vya maisha na hawana bima wala mtu wa kuwatetea.

Sasa umefika wakati wa madaktari wa Tanzania kuchukuliwa hatua stahiki kwa vifo vingi wanavyovisababisha kwa makosa ya kiufundi au kidaktari. Vifo hivi usababishwa aidha kwa uzembe au kwa kutokuwa na weledi wa kutosha kufanya opesheni na tiba mbali mbali au kutokujua kitu wakifanyacho.

Huu umekuwa ni utamaduni wa Tanzania sababu madaktari wamekuwa hawachukuliwi hatua za kisheria za kusababisha vifo bila ambavyo vingeepukika kama wangekuwa mahiri kwa kazi zao. Watu ambao wamekuwa wanafiwa na wagonjwa wao kumekuwa hakuna uchunguzi maalumu wa maiti zao ili kujua tatizo gani limepelekea mtu kufariki.

Kauli ya daktari pekee imekuwa ndiyo ya mwisho kusema kifo kilisababishwa na kitu fulani. Saa ingine hata vile vifo vya utata havifanyiwi hata uchunguzi wa mwili wa sababisho la umauti kama (Post mortem) Mtu akifa ndugu anapewa maiti kirahisi rahisi tu, sababu hata kama daktari ndiye kachangia au kasababisha kifo cha mgonjwa huwa hana wasiwasi wa kuendelea na kazi yake.

Sasa imefika wakati tuache mambo haya. Madaktari wa nchi zilizoendelea huwa wako makini kuhakikisha kuwa kutofanya kazi zao kwa weledi, kutapelekea kusitishwa kwa leseni zao au kukataliwa wao wa kuendelea kutoa huduma za kiudaktari maisha yao yote.

Na utamaduni huu upo sana pia kwa jeshi letu la polisi la saa ingine kuua raia bila hatia na kusinginzia watuhumiwa wamekufa wakiwa wanapelekwa hospitali. Na wakati huo huo mazingira ya wao polisi yakutupiana risasi na hao watuhumiwa huwa ya utata na hayaingii akilini.

Na hii yote wanafanya hivi sababu uchunguzi haufanyiki na askari hawachukuliwi hatua zozote. Sababu wao kitendo cha kumtuhumu mtu kuwa jambazi wanafikiri tayari kwao ni uhalali wa kumuua. Na siku zote polisi wanasema watuhumiwa wamekufa wakiwa wanapelekwa hospitali. Wakati wameshauawa tayari sehemu husika ilimradi polisi wafunge kesi kwa kuonekana eti wameua majambazi wakati siyo uhalisia wa matukio.

Hapa wanaotaabika ni ndugu wa hao marehemu ambao hawapati ukweli halisi wa mazingira yalitokea kupelekea mauaji ya ndugu zao. Na zaidi mambo haya yanaleta chuki katika jamii sababu hayana uwazi. Na swala hili haliishii to kwa madaktari na polisi lakini pia kwa wafanyakazi wengine pia watoao huduma kwa jamii. (Public Services)

THE TIME NOW HAS COME FOR THESE PEOPLE TO TAKE FULL RESPONSIBILITY AS ANY OTHER PROFESSIONAL AND TO BE PUNISHED ACCORDINGLY! THEY CANNOT JUST GET AWAY FOR THEIR WRONG DOING! ITIKADI HII SASA IFE NA BODI ZAO SASA ZIWASHUGHULIKIE!
 
Unakamatwa kwa kununua simu ya wizi, unapigwa, unalala selo, unatoa laki 500000 hadi millioni, kisha unaachiwa kisha kesho yako unamkuta yule polisi aliyekukamata anaitumia ile simu. Hili suala linaudhi na linaota mapembe
 
Back
Top Bottom