Madaktari na miandiko ya mcharazo

Justine_Dannie

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,963
1,617
Habari zenu wakubwa na wadogo!
Kwa muda sasa au ni desturi ya wataalamu wetu wa afya aka madokta kutuandikia majibu au mapendekezo ya kutatua au kutibu matatizo yetu kiafya kwa miandiko ya kuzonga zonga aka mcharazo.
Sasa basi naomba kufahamishwa nini sababu ya kuandika hivyo?
Je wakiandika vizuri kuna ubaya gani?
NAWASILISHA.
 
Habari zenu wakubwa na wadogo!
Kwa muda sasa au ni desturi ya wataalamu wetu wa afya aka madokta kutuandikia majibu au mapendekezo ya kutatua au kitibu matatizo yetu kiafya kwa miandiko ya kuzonga zonga aka mcharazo.
Sasa basi naomba kufahamishwa nini sababu ya kuandika hivyo?
Je wakiandika vizuri kuna ubaya gani?
NAWASILISHA.
Kwanza uelewe kuwa maandishi yale kwenye cheti hayakulengi wewe.Yale ni mawasiliano ya kitaaluma kati ya wanataaluma,huwezi kuelewa kitu pale mpaka akutafsilie mwana taaluma au ujifunze short hand za udaktari.Hata hivyo imerahisishwa sana kwa kuwa huandikwa kwa kiingereza,kama ikiiandikwa kwa kilatin ambayo ndiyo hasa lugha ya kisomi huwezi kabisa kuelewa.Waandishi wa habari pia wanapowasiliana huwezi kuona ndani mpaka watakapo tafsiri kwa lugha nyepesi.Mfano mdogo ni JMT,sio watu wote wanaweza kuelewa maana yake na zaidi sana ni sentensi inayoweza kuwakilishwa na herufi tatu tu.Karibu.
 
Hawana mda wa kuremba,chemistry na biology zina notsi nyingi sana sasa washazoe kucharaza kwenda mbele!!cha msingi upate huduma sahihi upone basi mengine mbwembwe tu.
 
Kwanza uelewe kuwa maandishi yale kwenye cheti hayakulengi wewe.Yale ni mawasiliano ya kitaaluma kati ya wanataaluma,huwezi kuelewa kitu pale mpaka akutafsilie mwana taaluma au ujifunze short hand za udaktari.Hata hivyo imerahisishwa sana kwa kuwa huandikwa kwa kiingereza,kama ikiiandikwa kwa kilatin ambayo ndiyo hasa lugha ya kisomi huwezi kabisa kuelewa.Waandishi wa habari pia wanapowasiliana huwezi kuona ndani mpaka watakapo tafsiri kwa lugha nyepesi.Mfano mdogo ni JMT,sio watu wote wanaweza kuelewa maana yake na zaidi sana ni sentensi inayoweza kuwakilishwa na herufi tatu tu.Karibu.
Mara nyingi nimewahi kutibiwa hospital za nchi za Ulaya. Nimegundua wanapoandika prescription ya dawa au maelezo ya mgonjwa hutumia computer (ambayo huandika herufu za kawaida japo lugha inaweza kuwa ya kidaktari) na hakuna mambo ya mchalazo kama kwetu.
 
Wengine wanaandika kitu ukimrudishia kesho yake yeye mwenyewe hajui alichoandika..
 
Uwiano wa tabibu mmoja kwa wagonjwa wangapi? Ataweza kuandika kwa madaha kweli?
 
...... " gifted people often have a bad handwriting because their brains are working faster than their hands" Hiyo ndo sababu ndugu
 
Back
Top Bottom