Madaktari mnalipwa mshahara mzuri lakini mnaishi maisha ya kuunga unga sana

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,350
2,000
Hii ni gross au net?
Hiyo 1.48Million ni Basic Salary.
Na kwa sababu kwa sasa wengi wao hawana tena marupurupu mengine, Gross Salary inakuwa sawa sawa na hiyo Basic Salary.

Kujua Net Salary yao, hapo inategemea na Makato kutoka kwenye basic salary yao, Wengi wao kwa wastani wanakatwa Kodi (18%), Mifuko ya Pensheni (6%), Bima ya Afya (4%), Chama cha wafanyakazi (2%) na Bodi ya Mikopo (15%) nk. Hivyo kwa ujumla wanakatwa kama 45% kutoka kwenye basic salary yao, na hapo wanaishia kupata wastani wa Net salary(Take home) ya wastani wa shilingi 850,000/= kwa mwezi.

Kumbuka huo ni mshahara wa Daktari wa ngazi ya juu katika ajira za serikali anapoanza kuajiriwa hapa Tanzania.
Kwa ajira za utumishi wa serikali, Degree ndio ngazi ya juu katika kuajiriwa, na katika fani ya utabibu degree ni Medical Doctor(MD) na hivyo huyo ndio medical Officer(Daktari) kisheria.
Na huo ndio mshahara wake anapoanza kuajiriwa serikalini. Na huenda ndio Mtumishi wa serikali wa kitaaluma anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko fani zingine zote zinazoajiriwa serikalini kwa sasa.

Zipo ngazi zingine katika fani ya Utabibu za chini kama Asistance Medical officer, Clinical Officer, Assistance Clinical Officer. Mishahara yao iko chini ya hapo, pia watumishi hawa kijamii wanajulikana kama madaktari japokuwa sheria haziwatambui kama madaktari(Medical officer).

SOURCE:Tume ya utumishi wa Umma nk.
 

CCNP Engineer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
463
1,000
Hiyo 1.48Million ni Basic Salary.
Kumbuka huo ni mshahara wa Daktari wa ngazi ya juu katika ajira za serikali anapoanza kuajiriwa hapa Tanzania.
Na huo ndio mshahara wake anapoanza kuajiriwa serikalini. Na huenda ndio Mtumishi wa serikali wa kitaaluma anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko fani zingine zote zinazoajiriwa serikalini kwa sasa.nk.


Wewe ni muongo wa kutupwa!!
Unajua ma Engineer wenye Degree serikalini wanaanza na Mpunga kiasi gani...
Huna data kaa kimya
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
49,257
2,000
1. Unavyosikia sikia nje, sivyo vilivyomo ndani... Siri ya mtungi...

2. Kujipenda kwa mtu haijalishi professional yake... Ni mwaamko na tabia za mtu mwenyewe...
Kuwa maridadi au kuwa ovyo ovyo...


Cc: mahondaw
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,350
2,000
Maisha ya watumishi wengi wa umma hayana tofauti sana kwa sababu...
1/Wengi wao wanategemea mishahara tu.
2/Vipato vyao vya mishahara havitofautiani sana.

Kwanini Madaktari wana maisha mabovu?
Majibu yake haya hapa..

1/Sio kweli kuwa wote au wengi wao wako hivyo. Katika kada ya utumishi wa umma, huenda madaktari ndio wana nafuu kubwa kimaisha kulinganisha na wengine.

2/Sio wote wanaoitwa madaktari basi ni madaktari, zipo kada nyingi sana za Afya zinafanya kazi hospitali lakini sio madaktari(Medical Doctor) lakini kijamii zinajitambulisha au kutambuliwa kama madaktari, na nyingi katika hizo zinalipwa mishahara midogo sana.

3/Heshima na Umuhimu wa Daktari kwenye jamii bado ni mkubwa sana, hivyo jamii inategemea kumwona Daktari akiwa na maisha fulani hivi ya juu yanayoendana na heshima hiyo. Bahati mbaya sana hilo haliwezekani kibongobongo kwa sababu Madaktari wanalipwa mishahara ya kawaida sana (Too much expectation from nothing).

4/Hulka na utamaduni wa Asili wa madaktari ni kutunza siri (Confidentiality), Faragha(Privacy), Humanity(Utu) na Kuangalia mambo kwa taswira pana(Vision) hivyo hiyo imepelekea kuishi maisha ya kutokupenda kuonyesha uhalisia wa maisha yao ya mafanikio au kujikweza ovyo ovyo kwenye jamii. Hivyo ni vigumu sana kufahamu maisha ya Daktari kirahisi rahisi. Wengi wao ni Disminder kumwonekano lakini wana maendeleo makubwa sana kimaisha.

5/Aina ya Kisomo walichopitia, Aina ya Kazi wanazofanya kila siku, muda mwingi wanaoutumia kufanya kazi na utamaduni wa kimaisha waliouiga kutoka kwa mentor wao umewafanya baadhi yao(hasa kizazi cha madaktari wa zamani zaidi) kuishia maisha yenye kupenda Pombe na maisha yasiyofikiria kitu kingine nje ya kazi zao. Hivyo tegemea kuona baadhi yao wako ovyo ovyo tu.
 

manji h

Member
Jul 15, 2016
43
150
Katika kazi ambazo inasemekana zina mshahara mnono basi mojawapo ni kazi ya UDAKTARI..

Cha kushangaza ni maisha ya kuunga unga wanayoishi madaktari yaani unaweza kukutana na daktari mtaani ukadhani ni kichaa unakuta kavaa nguo hazijanyooshwa, viatu vichafu, nywele hajachana yaani yupo ovyo ovyo tu...

Madaktari badiliken bwana kama mnavokuwa wasafi maeneo yenu ya kazi basi hata mtaani kuwen hivyo
Madaktar mda wote tuna waza kukufanya uwe healthy fit hatuwaz kupaka poda.....am proud of my work..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom