Madaktari mgonjwa anapokuja kwenye hospital zenu kupima ni vyema mukawaeleza majibu ya vipimo vyao

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,200
2,000
Madaktari wetu kwa baadhi ya hospital na vituo vya afya wamekuwa kama sio madaktari kabisa.

Leo mtoto wangu amepelekwa hospital moja mkoani singida kupima afya mara baada ya kuonekana anatapika na kuharisha.

Sasa alipopimwa mama mtoto akaandikiwa dawa bila ya hata daktari kumwambia mtoto anasumbuliwa na nini?.

Jioni natoka kazini, ile kufika nyumbani nakuta mtoto bado anaumwa tu ,kunyonya hataki wala nini.

Sasa mwanamke namuuliza mtoto kapimwa amekutwa anasumbuliwa na nini?. Anasema daktari kampima na kuanza kumuandikia dawa. Sasa namuuliza huku muuliza daktari kilichogundulika kinamsumbua?. Anasema hapana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
cosmonaut

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
1,363
2,000
Standard zetu bado zipo chini sana.
Dr. Mmoja anahudumia Wagonjwa kibao, unakuta una Mgonjwa kwenye chumba chako wakati nje wapo Wagonjwa Kama 50 wote wanasubiri uwahudumie, so mazingira yatakulazimisha kufanya kama alivyofanyiwa shemeji yetu.Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu, ma dr kwenye hospitali zetu ukiingia TU anakuliza unaumwa Nini ukinza kumwambia yeye tayari Kisha maliza kuandika ukapime Nini/unaumwa Nini.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juuchini

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
797
1,000
Ni kweli mkuu, ma dr kwenye hospitali zetu ukiingia TU anakuliza unaumwa Nini ukinza kumwambia yeye tayari Kisha maliza kuandika ukapime Nini/unaumwa Nini.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi Daktari anatakiwa kukaa na mgonjwa 30 minutes 15minutea lab. Investigation na 15 minutes making diagnosis and prescribing na max. Number of patients to be attended by a Doctor is 15 patients per day.
Sasa rudi kwenye hizo health facilities zetu Daktari kwa siku anakutana na wagonjwa 50- 80.
Huo muda wa kumweleza mgonjwa utatoka wapi?
Serikali iboreshe huduma ya Afya
Mzigo upungue kwa wahudumu was afya.
Mazingira ya kutolea huduma yawe rafiki.
Ni hayo tu kwa leo!
 
Eng Kahigwa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
766

Mwezi uliopita mwanangu wa miezi 5 alipelekwa hospitali flani ya serikali na mama yake, huwezi amini dawa alizopatiwa ni za vidonge.. dah! Nilichoka kwakweli.
 
Juuchini

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
797
1,000
Mwezi uliopita mwanangu wa miezi 5 alipelekwa hospitali flani ya serikali na mama yake, huwezi amini dawa alizopatiwa ni za vidonge.. dah! Nilichoka kwakweli.
Usishangae sasa kwenye health facilities za serikali matibabu yapo ya namna mbili:
Matibabu ya kisiasa: haya ni matibabu ambayo huduma hutolewa bila kufuata misingi ya kazi, mfano dawa ambayo mara nyingi hupatikana huko ni septrin.
So wanasiasa wanaagiza madaktari waandike hiyo septrin kwa magonjwa yote kitu ambacho ni hatari sana.
Lakini Daktari inabidi aandike hakuna namna.
Matibabu halisi: hapa unaandika kulingana na matatizo ya mgonjwa lakini hata akikosa hospitali yuko tayari kununua bila malalamiko.
Hiyo ndo hali halisi
Hasa local government ni shida Sana.
 
Dah! Sasa wanatuweka kwenye hali ngumu mno...na kama hatupo serious kwenye maswala ya afya, tusitegemee maendeleo chanya kwa nchi yetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom