Madaktari kwanini wamtibu Dr Ulimboka wakati wapo kwenye mgomo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari kwanini wamtibu Dr Ulimboka wakati wapo kwenye mgomo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jimy P, Jun 29, 2012.

 1. J

  Jimy P Senior Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdaktari wanahitaji Mshahara wa Milioni 3.5, Katika nchi Maskini ni Vigumu kulipwa mshahara huu, Nadhani wafanye Analysis kama inawezekana kwani kwa sasa anayetoka Chuoni analipwa Kuanzia Laki Tisa, Na Serikali imewaongezea Posho walizokuwa wanahitaji isipokuwa la kulipwa mshahara huo na nadhani imefika wakati kama unaona kazi unayofanya hailipi badilisha kazi au usisomee kitu ambacho halilipi, nawashauri wote wanaosoma Udaktari na Wanaotarajia kusomea kama unadhani hailipi au Ukimaliza Chuo lazima uajiriwe na Serikali usisome au acha unachosome somea kitu kingine,

  Nadhani imefika wakati tujue kuwa Professional nyingine ni muhimu pia kama wanavyodhani Madaktari wao ni muhimu zaidi halafu Board ya mikopo inatoa asimilimi 100% kwa wanafunzi wanaosomea Udaktari hizi ni Kodi za Watanzania ambazo lazima muwatumikie,

  Idara ya afya ni miongoni mwa idara zinazooongoza kwa Rushwa Tanzania,

  Madakri wamegoma kuwatibu Watanzania lakini Dr Ulimboka kafika wameacha Mgomo wameenda kumshughulikia wanaacha watanzania wanaendelea kufa

  Madaktari mnachelewa ofisini, mnapokea Rushwa haya yote hamsemi mtayerekebisha vipi,

  Umefika wakati Serikali kutumia Sheria za Utumishi la sivyo itafika sehemu Watumishi wote wa Serikali wahitaji Milion 3.5

  Viongozi wenye dhamana fanyeni maamuzi magumu whether is wrong or Right,
  Mhe EL Alishawahi kusema Msiogope kufanya Maamuzi whether is wrong or Right.

  Mhe Waziri mkuu kila kitu lazima mseme Top Leaders kwani huko mikoani hakuna viongozi au Wilayani.
  Watekeleze wajibu wao na Fanya Maamuzi kama kiongozi Mkuu wa serikali lazima mbadilike ili nchi iende.
  Hao wanaotaka kushika nchi watanzania wanafikiri hawatacheka na mtu anayekwenda kinyume na Sheria Na taratibu za Kazi na ndivyo itakuwa hivyo
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  dr ulimboka ni kafara wa kutetea haki ya afya ya mtanzania!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Usifikiri nakutukana nikisema hili ni swali la kijinga.
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Mimi nina swali... Kwanini wanataka kuua Kiongozi wa madaktari wakati wapo kwenye majadiliano?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Je Ulimboka angekufa, je mgomo ungeisha??
  Kikwete na watndaji wake wanafikiri kwa kutumia enye ndembendembe
   
 6. J

  Jimy P Senior Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unadhani nani aliyetaka kumuua?
   
 7. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wanamtibu kwa sababu hukumuua ulivyo mteka kama ungemuua wasingemtibu.............ukijua ni kwa nini wabunge wanaenda kutibiwa india utajua kwa nini wanamtibu
   
 8. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Mleta mada tuambie Mishahara ya BOT, TRA na Mashirika mengine tulinganishe na daktari
   
 9. J

  Jimy P Senior Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usingeisha nadhani imefika wakati tumjue aliyefanya tukio hilo, watanzania wote tutumie ulinzi shirikishi
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,829
  Trophy Points: 280
  Mleta mada hajui anacho kisema.
   
 11. J

  Jimy P Senior Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani wana harakati wapiganie wabunge watibiwe hapa hapa nchini au wabunge wakija Jimboni waelezwe watanzania hatupendi wanavyotumia kodi zetu kutibiwa nje
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Serikali imkamie yeye tu wa kupigwa na kuwaacha Madaktari wengine huru?
   
 13. J

  Jimy P Senior Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kipi nisichokijua?

  Mfano wewe leo Mzazi wako akaugua ukaenda Hospital ukanyimwa huduma na Mzazi wako akafariki ila Dr Olimboka anatibiwa utajisikiaje? Hata hayo maandamano utashiriki
   
 14. J

  Jimy P Senior Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mishahara ya BOT na TRA sina data ila imefika wakati tuzungumze kwenye mchakato wa katiba mpya viwango vya mishahara
   
 15. m

  mishalejuu Senior Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni jazbar...mtoa mada yuko sahihi madaktari wameawa na rushwa za kila aina. pampja na ufisadi... Ni Daktari yupi wewe umjuaye hana duka la madawa? Dawa wanazuza madukani mwao zinatoka wapi....majority wanakuwa wamezipora katika hospitali zetu za wananchi......theni ukienda hospital unaambiwa hapa dawa hii hakuna nenda famasi ya fulani pal mjini ndo anauza dawa nzuri...kumbe duka ni la kwao.....wanaJF hawa hamwajui? au hamjawahi kuugua mkaambiwa hayo? kama bado subirini....
   
 16. e

  eff.com New Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nchi dhaifu lazima itakuwa na viongozi dhaifu.
   
 17. J

  Jimy P Senior Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna nchi dhaifu cha msingi wafanye maamuzi magumu, wasisite site kama Pinda alivyo mgumu kutoa maamuzi maamuzi magumu
   
 18. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Mama ako kwa nini alizaa na WASSIRA wakati ni mume wa mtu?
   
 19. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Usikimbilie huko sana utachanganyikiwa mkuu, jiulize Professor (Lecturer) anayemsomesha Daktari analipwa sh. ngapi? Si zaidi ya 2.5 M mkuu. Je serikali ya Baba Riz 1 itaweza kuwapa 3.5?
   
 20. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Hivi BOT na TRA au Mamlaka ya CDA au TPA au TCRA ni muhimu kuliko Madaktari? Chezea daktari wewe? Ni Second to none but God only
   
Loading...