Madaktari kutoka Tanzania wapokelewa kwa heshima Botswana

Walimu ni South Sudan kwa sasa na Botswana, Libya ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa kuwalipa waalimu.
 
waende tu, kwanza ni incompetent ile mbaya, bora tubaki na hospitali za watu binafsi. wataenda huko watachokwa watarudi tu na kazi wataanza kutafuta upya.....yaani huo mkwara kwamba madaktari watahama nchi ni wa kujinga sana kwasababu hakuna hata doctor mmoja anayefanya kazi ya hisani hapa, wote wanaganga njaa/wanatafuta pesa na hizo kazi walizipata kwa mbinde...wakiondoka basi tutaajiri wengine chuo si kina magraduate kila mwaka...kwani nini bwana hata tutishane?

Wewe huwajui watanzania kumbe. Sifa wanazopewa watanzania katika kuchapa kazi ugenini usipime! Kwa kuwa wanapewa mazingira bora ya kufanyia kazi kulikoni hapa, wanajituma ile mbaya ugenini ambako hawapewi ahadi hewa bali REAL things, weacha tu. Unanikumbusha sungura mfupi na asiyejua kuchuma matembe anapokosa kuyafikia anadai "kwanza ni mabaya na hayatamaniki hata kuyaangalia, ni machungu hayo....lelelele, lelelele..." wakati wenzake wanajilamba hadi kisogoni kwa butamu.

Nyie Tanzania endeeni kusomesha wataalam halafu wakaendeleze nchi zingine, kwanza hata kusoma kwenyewe kwa tabu, ya nini kuteswa mpaka kufa kwakati hata waganga wa kienyeji wanapata mamilioni kwa mwezi (eg maji marefu) kwa kusinzia kwenye viti vinavyoswing na VX zinawangojea nje, PLUS uhakika wa maisha baada ya miaka mitano hata kama haingii mjengoni tena??? Nawatakia kheri waliochumpa na kupata tenda huko nje, wakumbukeni ndugu zenu mliowaacha kwenye tanuri wakiuwawa na kung'olewa makucha na meno kwa kuwa tu wanauliza kuongezewa shilingi kidogo wanunue fourth hand car angalau na waboreshewe mazingira ya kazi na kujenga chumba na sebure uswahilini.

Sio siri, siku hizi kuitwa daktari Tanzania ni kama tusi la nguoni, ati utalipwa mbinguni, kwani mbingu ni kwa madaktari tu? Nyie hamtaki mbingu? Kudadadeki. Tanzania inawafanya wanafunzi waone shida sana kuchagua kusomea udaktari hivi sasa, labda kama ana maono ya kwenda kufanyia kazi nje au aje aachane nayo akafanye kazi nyingine. Ndio maana wengi wanaenda kusoma MBA, sikujua sababu, sasa naiona wazi kabisa.
 
Ni kweli mshahara ni mdogo ukilinganisha na mfumuko wa bei!

Serikali; kwa ujumla wake wote serikali yetu haijampa mtumishi wa umma heshima yake kimasilahi, hasa kodi ya mshahara anayokatwa mtumishi kila mwezi, mfanyabiashara mwenye biashara ya mamilioni halipi kwa mwaka.

Natamani Serikali yetu kupitia kilio cha madaktari na waalimu wanaojipanga kugoma ifungue masikio yake kuyaweka sawa masilahi ya watumishi wake kwa ufanisi wa Taifa na wananchi wake inaowaongoza....!
 
hapa tunapoongea sasa hivi wamepokelewa madaktari watano kutoka Mbeya tanzania na tayari residence permit zao zinatengenezwa ili kuanza kazi mara,
watakuwa wanafanya kazi hospitali za Gaborone city council na mishahara yao itakuwa allmost mara saba ya mshahara waliokuwa wanapata tanzania wa laki tisa

My take:
serikali ya tanzania isifikiri inawakomoa hawa madaktari ambao nchi za huku kusini zinaheshimika kuliko jambo lolote lile,kama walifikiri wanawakomoa kwa kutumia SADC ili wasipate kazi huku wajua serikali ya Botswana ni serikali imara na madhubuti na haiendeshwi kinafiki
Tunawatakia maisha mema huko ughaibuni!!!Zamani kidogo niliona advet moja toka USA wakihitaji madaktari specifically from TZ zaidi ya 400, naona vijana wa TZ wana market kubwa huko ulaya!!!!
 
Watanzania kwa maneno bana kulikuwa na tetesi kuwa serikali inaleta madaktari wageni kuja Tanzania watu waliishambulia serikali eti ni aibu kubwa kutibiwa na wageni leo tena mnawasifia Botswana...kama wamepata kazi huko na wanalipa vizuri safi sana...serikali aina uwezo wa kuwalipa mshahara mnaotaka.
Mkuu na hao madaktari wageni watawalipa njugu au kiasi gani???? Hizo fedha watazitoa wapi, wacheni roho za korosho kwa vile Watanzania ndio muwanyanyase kuwalipa kiduchu????

Manyi tuko pamoja, ni kweli nimejaribu kugusa upande wa starehe kwa sababu kama "Ya sakafuni yameshindikana" (upande wa basic needs ) vipi kama wakihitaji "Ya shinikizoni" upande wa basic wants?...Ndio maana nimeenda upande wa Basic Wants
 
i doubt kaa wapasua kichwa badala ya miguu can be marketable anywhere than the land which redefined incompetence..

I guess you got it wrong; mtu kupasuliwa kichwa badala ya kupasuliwa miguu siyo kosa la dakatari aliempasua, kwani daktari anafuata documents ziliombatana na mgonjwa huyo huko theater. Iwapo mgonjwa aliambatana na document zinaozonyesha kuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa basi daktari atafanya hivyo. tatizo hilo linatokea kirahisi sana iwapo hospitali haina information management system ya kuaminika kama ambavyo muhimbili ilivyo. Document zote muhimu zinakuwa kwenye makaratasi na inawezekana kabisa makaratsi yakachanganyikana biana ya wagonjwa wakati wanahamaishwa kutoka chumba kimoja hadi kingine. Nadhani mojawapo ya mazingira mazuri ya kazi yanayoombwa na madaktari ni hiyo ya efficient information handling system.
 
hapa tunapoongea sasa hivi wamepokelewa madaktari watano kutoka Mbeya tanzania na tayari residence permit zao zinatengenezwa ili kuanza kazi mara,
watakuwa wanafanya kazi hospitali za Gaborone city council na mishahara yao itakuwa allmost mara saba ya mshahara waliokuwa wanapata tanzania wa laki tisa

My take:
serikali ya tanzania isifikiri inawakomoa hawa madaktari ambao nchi za huku kusini zinaheshimika kuliko jambo lolote lile,kama walifikiri wanawakomoa kwa kutumia SADC ili wasipate kazi huku wajua serikali ya Botswana ni serikali imara na madhubuti na haiendeshwi kinafiki

900,000 x 7 =6,300,000 Tsh!Duh kumbe ile mil 7.7 waliyokuwa wanaitaka ni kubwa kuliko hata wanavyolipwa Botswana?Kwakweli asiyetaka kazi na akatafute muajiri anayeweza kumlipa hivyo namuunga mkono JK!
Anyway naungana mkono na JK kuwatakia maisha mema n yenye mafanikio huko waendako.

NB: Nina swahiba wangu m-botswana siku moja katika kumdadidsi juu ya nchi yao kuwa kapu la kupokea waafrika alionyesha chuki za wazi za kutokufurahia jambo hilo,na kwa kinywa chake aliniambia Xenophobia iliyotokea South Africa si mbali itaibuka na kwao ni bomu ambalo limeshaanza kufuka moshi,maana uraiani watu wanakerwa sana na uwepo wa lundo la wageni wanaoishi nchini kwao.Tena nasikia watanzania ni wachache uki-compare na wazambia,malawi na nchi nyingine za kusini mwa Africa.Hivyo ndugu zangu madaktari mnaozamia Botswana mkae chonjo.
 
I guess you got it wrong; mtu kupasuliwa kichwa badala ya kupasuliwa miguu siyo kosa la dakatari aliempasua, kwani daktari anafuata documents ziliombatana na mgonjwa huyo huko theater. Iwapo mgonjwa aliambatana na document zinaozonyesha kuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa basi daktari atafanya hivyo. tatizo hilo linatokea kirahisi sana iwapo hospitali haina information management system ya kuaminika kama ambavyo muhimbili ilivyo. Document zote muhimu zinakuwa kwenye makaratasi na inawezekana kabisa makaratsi yakachanganyikana biana ya wagonjwa wakati wanahamaishwa kutoka chumba kimoja hadi kingine. Nadhani mojawapo ya mazingira mazuri ya kazi yanayoombwa na madaktari ni hiyo ya efficient information handling system.
Mwalimu ni kutokuwa makini na kutofuata taratibu.Information kuwa ndani ya makaratasi si tatizo, hata hapo majuu ulipo siyo hospitali zote zina Health information management system na watu hawachangaji wagonjwa.
 
Bravo.

Namkumbuka Dr. Kimaro (RIP) aliyekuwa Rais wa DARUSO miaka ya 1992, Rais Mwinyi aliapa kuwa hatafanya kazi yeyote Duniani, lakini Botswana alifanya kazi.

Mchukiaufisadi, Dr. Kimaro keshafariki? sina habari kabisa. na nimekuwa najiuliza Dr. Kimaro aliishia wapi. unaweza nipa details, alifariki lini, na kwa sababu zipi? Au nae walimliumboka nini?
 
Mwalimu ni kutokuwa makini na kutofuata taratibu.Information kuwa ndani ya makaratasi si tatizo, hata hapo majuu ulipo siyo hospitali zote zina Health information management system na watu hawachangaji wagonjwa.

Madai yako yanaweza kuwa kweli lakini hilo siyo kosa la daktari. Utaratibu wa upasuaji ni hivi: daktari kiongozi wa operation na wasaidizi wake wanapitia ripoti ya mgonjwa kwa makini sana na kuplani namna ambavyo operation itakavyofanyika. Muda ukifika mgonjwa mhusika anapelekwa theater na shughuli za upasuaji zinaanza; mgonjwa huyo hapelekwi na dakatri bali atapelekewa na manesi ambao pia hufuata rekodi walizonazo kuhusu mgonjwa. Sasa iwapo jopo la madakatri kule theater walisoma taarifa ya mgonjwa wa kichwa na wakajiandaa kufanya operation ya kichwa halafu wakapelekewa mgonjwa wa mguu utategemea wafanye nini. Kosa ni namna ambavyo information ilivyokuwa handled, ama daktari alipekewa faili la mgonjwa mwingine, au mgonjwa aliyepelekwa alikuwa kawekewa faili la mgonjwa mwingine. kwa hiyo whether information handling system ni ya makaratsi au ni ya computer, makosa ya aina hiyo yanatokana na bad information flow, siyo makosa ya kitaalamu.

Tatizo hilo linapotokea huwezi kumlumu dakatari aliyefanya upasuaji bali ni system nzima ya kuhandle wagonjwa. Huku ninakoishi manesi kabla hawajamchukua mgonjwa ni wajibu wao kuhakikisha kuwa mgonjwa wanayemchukua ndiye hasa wanayemhitaji. Huwa wanamwuliza maswali kama matatu hivi yanayomtofautisha na mtu mwingine yeyote: Date of Birth, Home Address, na Last 4 digits of Social Security number. Huwa hawatumii majina kwa sababu watu wengi wanaweza kuwa na majina yanayofanana. Inabidi na sisi kwetu ambako home adress zetu ni P.O.Box, na wala hatuna National ID number ya aina yoyote tutafute utaratibu mwingine wa kuwa-Identify watu wetu uniquely.
 
I guess you got it wrong; mtu kupasuliwa kichwa badala ya kupasuliwa miguu siyo kosa la dakatari aliempasua, kwani daktari anafuata documents ziliombatana na mgonjwa huyo huko theater. Iwapo mgonjwa aliambatana na document zinaozonyesha kuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa basi daktari atafanya hivyo. tatizo hilo linatokea kirahisi sana iwapo hospitali haina information management system ya kuaminika kama ambavyo muhimbili ilivyo. Document zote muhimu zinakuwa kwenye makaratasi na inawezekana kabisa makaratsi yakachanganyikana biana ya wagonjwa wakati wanahamaishwa kutoka chumba kimoja hadi kingine. Nadhani mojawapo ya mazingira mazuri ya kazi yanayoombwa na madaktari ni hiyo ya efficient information handling system.

Waaambie bwana. Surgeon sio Physician. Surgeon ukimwambia tumbo linauma sana anapasua na kuangalia kinachokusumbua. Akikikuta anakiondoa, akikikosa anaacha in situ na kufunga tena tumbo in layers. Physician ni kama medical politician, kila tatizo lina differencials kibao na ili kupata uhakika lazima maabara zitumike na kumpa nafasi ya uhakika wa kulijua tatizo na tiba yake. Mliyo mnuguna waitu? Sorry, Omukama waitu?
 
hapa tunapoongea sasa hivi wamepokelewa madaktari watano kutoka Mbeya tanzania na tayari residence permit zao zinatengenezwa ili kuanza kazi mara,
watakuwa wanafanya kazi hospitali za Gaborone city council na mishahara yao itakuwa allmost mara saba ya mshahara waliokuwa wanapata tanzania wa laki tisa

My take:
serikali ya tanzania isifikiri inawakomoa hawa madaktari ambao nchi za huku kusini zinaheshimika kuliko jambo lolote lile,kama walifikiri wanawakomoa kwa kutumia SADC ili wasipate kazi huku wajua serikali ya Botswana ni serikali imara na madhubuti na haiendeshwi kinafiki

Nyumbani ni nyumbani,hata kama watalipwa fedha nyingi kiasi gani haitawasaidia katika maendeleo yao tena Botswana wana utaratibu ambao watahakikisha fedha yote wanayokulipa inashia nchini kwao iwe kwa matanuzi au kwa maendeleo ikibidi kujenga huko kiwanja watakupatia hata mke/mume ukitaka,majuto ni baada ya kurejea nchini ndiyo utawashangaa uliowaacha wana hospitali zao majumba ya kifahari wakati we mtoro huna mbele wala nyuma na Pula unazo za kutosha ambazo hazikusaidii chochote zaidi ya huko Tswana.
Tumeona wengi walikwenda kufanya kazi huko siyo tu madaktari hata wa field zingine,huu mtego kidogo na wengine tuingie ingawa siyo tiba ila tulikwepa kabisa maisha artificial kila kitu supermarket wengine tumezoea kulima chakula chetu wenyewe na kujipangia siyo kupangiwa,kingine ni ile home sickness kama vile umewasaliti ndugu zako/wazazi wako kwa ujumla maisha ya nje siyo mazuri kama nyumbani.
 
Mimi nawashangaa watu wanaosema Madokta waende.Hivi huwa mnatembelea Shule zetu kuona jinsi Wanafunzi wengi wanavyoyaogopa masomo ya Sayansi?.Hata hao ambao wanaenda huko wanenda kusoma nadhari kwani shule hazina Maabra kwa ajili ya Masomo hayo.Watanzania tumechanganyikiwa hata hatujui dunia ya sasa inaendeshwaje.

Mkuu Nyalutubwi you have made my day!! Na kweli tumechanganyikiwa, we eti amiri jeshi mkuu anasema "...waondoke wakatafute mwajiri atalayewalipa mshahara wanaotaka" Wakati ni yeye na serikali yake ndo imewasomesha kwa mkopo, sasa ata re-cover wapi hiyo hela?

JK ni rais ambaye amevunja katiba big times, na tunamuimbia na kumpigia makofi utadhani wakati Yesu anaingia Yerusalemu!!!
 
i doubt kaa wapasua kichwa badala ya miguu can be marketable anywhere than the land which redefined incompetence..

Pamoja na hayo Abdullahim, ha-justfy maneno ya mkuu wa nchi aliyoyatoa badala ya kumaliza mgomo kwa kutumia nguvu iwayo yeyote ile aliyonayo kama rais!!! Yaani akaona dawa ni kuwatishia nyau!!! Tumekosa muelekeo, na rais ni dhaifu tu!!!

One isolated case, should never be used against them for the whole of their lives bana!! Maana hata huku kwenye mabox yetu "wanakosea"
 
nilikua nawashusha konfo tu kaka, hahaaaaaa..
 
Wewe huwajui watanzania kumbe. Sifa wanazopewa watanzania katika kuchapa kazi ugenini usipime! Kwa kuwa wanapewa mazingira bora ya kufanyia kazi kulikoni hapa, wanajituma ile mbaya ugenini ambako hawapewi ahadi hewa bali REAL things, weacha tu. Unanikumbusha sungura mfupi na asiyejua kuchuma matembe anapokosa kuyafikia anadai "kwanza ni mabaya na hayatamaniki hata kuyaangalia, ni machungu hayo....lelelele, lelelele..." wakati wenzake wanajilamba hadi kisogoni kwa butamu.

Nyie Tanzania endeeni kusomesha wataalam halafu wakaendeleze nchi zingine, kwanza hata kusoma kwenyewe kwa tabu, ya nini kuteswa mpaka kufa kwakati hata waganga wa kienyeji wanapata mamilioni kwa mwezi (eg maji marefu) kwa kusinzia kwenye viti vinavyoswing na VX zinawangojea nje, PLUS uhakika wa maisha baada ya miaka mitano hata kama haingii mjengoni tena??? Nawatakia kheri waliochumpa na kupata tenda huko nje, wakumbukeni ndugu zenu mliowaacha kwenye tanuri wakiuwawa na kung'olewa makucha na meno kwa kuwa tu wanauliza kuongezewa shilingi kidogo wanunue fourth hand car angalau na waboreshewe mazingira ya kazi na kujenga chumba na sebure uswahilini.

Sio siri, siku hizi kuitwa daktari Tanzania ni kama tusi la nguoni, ati utalipwa mbinguni, kwani mbingu ni kwa madaktari tu? Nyie hamtaki mbingu? Kudadadeki. Tanzania inawafanya wanafunzi waone shida sana kuchagua kusomea udaktari hivi sasa, labda kama ana maono ya kwenda kufanyia kazi nje au aje aachane nayo akafanye kazi nyingine. Ndio maana wengi wanaenda kusoma MBA, sikujua sababu, sasa naiona wazi kabisa.

mkuu umeongea point
 
Back
Top Bottom