Madaktari kuandamana Julai 16 saa nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari kuandamana Julai 16 saa nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Jul 14, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA Cha Madaktari nchini (MAT), kimesema maandamano yao yako pale pale na tayafanyika Jumatatu ya Julai 16, saa nne, na si vinginevyo. Aidha, MAT, kimelaani kutekwa na kupigwa kwa mwenzao Dk. Steven Ulimboka na kufutiwa leseni kwa wanafunzi wa vitendo (interns). Uamuzi huo wa MAT, ulitolewa jijini Dar es Salaam, katika kikao cha dharula cha madaktari 500 walioketi katika ukumbi kituo cha Utamaduni wa Korea. MAT, kupitia Katibu wake, Rodrick Kabangila alisema “Kwa pamoja tulilaani vitendo vya unyanyaswaji wa serikali dhidi yetu, kwanza uamuzi wa Baraza la Madaktari (MCT), wa kuwafutia leseni wanafunzi wa vitendo bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kutoa maelezo yao. “MCT lilishindwa kuwaita na kupata maelezo yao badala yake walijichukulia hatua za haraka za kuwafukuza, wakati suala hilo lipo mahakamani”alisema Kwa mujibu wa Kabangila, madaktari wanalaani hatua ya kunyimwa chakula na kufukuzwa na FFU kwenye vyumba vya kulala (hosteli), madaktari kabla ya taarifa ya maandishi kutoka Wizarani. Pia, wanafunzi hao na wengine walinyimwa posho kabla ya barua ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hivyo, vitendo hivyo na vingine vinaonyesha udhalilishwaji mkubwa kwao, ikizingatiwa kuwa ni wanataaluma wanaohitajika ndani ya nchi. Katika maelezo yake, taaluma hiyo ina umuhimu mkubwa, na ikiwa unyanyasaji huo utaendelea, kutasababisha idadi kubwa ya madaktari kuondoka nje ya nchi. Alionya kwamba endapo wataondoka taifa litakosa madaktari na kutafanya Wananchi zaidi ya milioni 12 kukosa huduma ya afya. Mbali na hilo, Katibu huyo alisema, bado milango iko wazi kukutana na serikali ili kukaa mezani kwa lengo la kumaliza mgogoro wao ambao umedumu kwa muda mrefu sasa. Kimsingi, Kabangila alisema kutokana na hatua hizo, wameandaa maandamano pindi watakapopata kibali kutoka vyombo vya usalama. Hata hivyo, alisema maandamano ni haki yao na kibali ni kwa ajili ya ulinzi wao. Alifafanua kwamba, maandamano yana lengo la kupinga dhuluma na uonevu dhidi ya taaluma muhimu ya udaktari na madaktari wenyewe. Alisema, MAT inasikitishwa na dhuluma hiyo kwa kuzingatia uwiano duni wa madaktari hapa nchini ambapo daktari mmoja hutibu wagonjwa 30,000 kwa mwaka chini ya viwango vya kimataifa. “Tutafanya maandamano ya amani, madaktari wote na wadau wa sekta hii wenye mapenzi mema tunawaomba washiriki… madaktari tutavaa makoti yetu meupe na watakaoshiriki nasi wavae vitambaa vyeupe. Maandamano yataanzia nje ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, tutaishia kwenye geti la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, tukiwa na mabango ya kulaani kitendo cha kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande alichofanyiwa Dk. Steven Ulimboka,” alisema. Dk. Kabangila alisema kuwa wataishinikiza serikali iunde tume huru kwa ajili ya kuchunguza suala la Dk. Ulimboka itakayofanya kazi haraka na wahusika wote wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. HABARI ZAID BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: MADAKTARI KUANDAMANA JULAI 16 SAA NNE
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana kuona kuwa interns ndio wamekuwa mbuzi wa kafara katika msuguano huu!
   
 3. a

  albinomzee Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Naomba tuwe siliazi kwahili madaktari.sisi tutawaunga mkono moja kwa moja.ila msije mkaonyesha uoga wa CWT na walimu wao ikifika dakika ya mwisho.Naomba pia wale wana maombi waanze leo kuliombea geshwi la polishwi na kamanda makengeza,ili lipate intelejensia inayoonesha hakutakua na tishio la shambulizi kutoka kwa alshabaaab wala boko haram.solidarity forever.
   
 4. mwangalizi

  mwangalizi JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  Rekebisheni hivyo, maana mlitaka kumtosa uli na kujiletea dharau, pamoja sana
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  For once Mwema and Co. Tafadhali wapeni Madaktari ushirikiano na ulinzi wanapo wasilisha ujumbe wizarani. Tumechoka tumechoka ukandamizaji na ukatili wa jeshi la polisi.
   
 6. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wananchi nao tutaandamana kwa kutuacha tufe wakati Madk. Mpo, nyampafu. Mungu awape zawadi yenu n bukumu yenu hapahapa. Yaani mnagombana na govt halafu mwatuua sie? Damu za ndugu zangu walikufa kwa nyie kuoma ziwe chakula chenu. Laana au baraka ziwauate nyie na familia zenu kwa kadiri mungu atakavyoona inafaa.
   
Loading...