joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Waziri wa Afya wa Kenya wakati akitangaza kifo cha mgonjwa wa Corona hapo Jana Alhamisi, alisema kwamba mgonjwa huyo alifika Hospitalini hapo akiwa anaumwa maradhi mengine, hivyo alihudumiwa na madaktari na manesi wa kawaida na kulazwa katika wadi za kawaida pamoja na wagonjwa wengine hadi alipofariki na kupelekwa katika chumba cha maiti, muda wote huo alikua hajagundulika kama alikua ameambukizwa virusi vya Corona. Ndugu na jamaa wa mgonjwa waliomba kufanyike " Postmortem " ndio ikagundulika kwamba alikua na COVID-19.
Taarifa zisizorasimi zinadai kwamba, ndugu wamesema kwamba, huenda aliambukizwa virusi akiwa hapo Hospitalini kwasabu ni zaidi ya miezi miwili sasa hajawahi kutoka nje ya nyumba yake kwa sababu alikua na mgonjwa wa asiyeweza kutembea, na hapo nyumbani hakujawahi kutokea mtu yeyote mwenye dalili hadi sasa.
Ikumbukwe kwamba hiyo sio Mara ya kwanza kwa madaktari Kenya kuwachanganya wagonjwa wenye maambukizi ya Corona na wagonjwa wa kawaida. Wiki moja iliyopita huko katika hospitali ya KNH, mtoto wa miaka 13, alilazwa ICU pamoja na wagonjwa wa kawaida bila kujulikana kama alikua na virusi vya Corona, hadi alipofariki, jambo lililosababishwa chumba cha ICU kufungwa na wagonjwa kuhamishiwa kwengine.
Uzembe wa namna hii hadi kufikia kiasi kwamba madaktari hawajui dalili za Corona, huwezi kuukuta kwengine zaidi ya Kenya.