Madaktari KCMC wafungiwa kwenye ukumbi wa mkutano na wana usalama

Dr Klinton

Senior Member
Jan 21, 2012
123
152
taarifa ni kuwa madaktari KCMC wamefungiwa ktk ukumbi wa mkutano na wana usalama
Naona nguvu ya dola sasa inatumika
 
wala haina shida........wacha wawafungie then tutaona nani mshindi.......upuuzi wa serikali sasa mwisho
 
taarifa ni kuwa madaktari KCMC wamefungiwa ktk ukumbi wa mkutano na wana usalama
Naona nguvu ya dola sasa inatumika
huwezi kushindana na madaktari na hilo linajulikana hata nchi za wenzetu. Madaktari wenyewe tunao 10 tu nchi nzima. Wapeni HAKI zao kampuni yenyewe ni ya MUZUNGU na wao wana matumizi pia.... kama nyie mlioko hko Dodoma.....(nchi ishauzwa kwa wazungu)
 
Serikali maji yako shingoni. Kwa hii ishu ya madaktari, serikali inajitafutia matatizo tu, kwani 'huwezi kumlazimisha punda kunywa maji'
ndo kama ishu ya walimu, mwisho wa siku idadi kubwa ya wanaomaliza std 7, hawajui kusoma wala kuandika, form iv, zero kibao...
 
taarifa ni kuwa madaktari KCMC wamefungiwa ktk ukumbi wa mkutano na wana usalama
Naona nguvu ya dola sasa inatumika
Dr Klinton nashukuru kwa taarifa,lakini je source ya news hii unahakika?na je wamewafungia kwa sababu gani?au walikuwa kwenye mkutano?
Hali ya Dodoma ikoje?mbeya na mwanza vipi nako?
Nilikuwa naangalia bunge maana nilishahisi kutakuwa na hoja ya dharura ili kujadili mgomo wa ma- dr,Mh Zitto alisimama kutoa hoja lakini Makinda akaahirisha bunge kutoa muda wa kamati za bunge kupitia taarifa mbalimbali na akaishia tu kusema ametaarifiwa na serikali kuwa itatoa taarifa kuhusu mgomo wa madaktari,na bunge limeahirishwa mpaka kesho,sasa hapo mnatakiwa kukaza buti hasa,hata kama wakiwafungia ninyi mshikamane na muwe kitu kimoja,nawashauri mawasialiano yawe mbele,otherwise mtapishana na ama propaganda zao zitasambaa na kuweza kusababisha kuhitilafiana.
Tuko pamoja sana.tena kwenye kukataa kujadili mibunge ya CCM imenikera sana,najua wanapanga njama mbaya sana.
 
Hawana tofauti na Mfa maji, Daima haishi kutapatapa.

Ili uweze kupona JIPU inabidi ulipasue kisha uondoe hadi na kiini chake, vinginevyo kwa kulikuna hapo bado jipu unalo tu.

Serikali iondoe kiini cha mgomo na siyo kutapatapa na mambo yasiyokuwa na uhusiano!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hii yote inatokana kwa sabb viongoz tulio waweka madarakani wanaufinyu wa kufikiri, raisi, waziri mkuu, na spika wote wamekubaliana kuwa posho ya wabunge iongezwe, lakini madaktari serikali haina pesa inawezekana kweli?
 
Serikali this time hawana pa kutokea,.wanatakiwa wajiangalie upya..
 
mbona wanakata majani wanaacha mizizi wakidhani mti utakauka, ngoja tusubiri kuona matokeo

pia wamewapa fursa kujadili mambo yao kwa uhuru zaidi, wakitoka watawaambia walikuwa wanajadili masuala ya kitabibu
 
Pinda at work... sio busara ata kidogo kutumia minguvu badala ya hekima.. ipo siku tutamfungia pinda asitoke kwake. anataka watu waendelee kufa?

hii safu ya viongozi kipindi hiki sioni mwenye afazali

K.J ndo kabisaaa
Pindwa - yaani huyu hata bure hafai
spika wetu - ndo :yawn:

mawaziri wao ndo sioni mwenye adhali.. nchi inajiendea endea tu, hawa wanajiongezea afu wanakataa wenzao wasiongezwe..
 
Back
Top Bottom