Madaktari kama kweli ni wazalendo tupeni mbadala na sisi walala hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari kama kweli ni wazalendo tupeni mbadala na sisi walala hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by segwanga, Jun 29, 2012.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwanza heshima kwenu madaktari wote na pole kwa majukumu yenu ya kudai haki zenu.Najua hamko vizùri kisaikolojia kútokana na kamanda wenu kùharibiwa maisha yake na watu wadharimû wasiolitakia mema taifa letu.Nawasifu kwa ushirikiano wenu ktka kulishughulikia suala la daktari ulimboka. Lakn naomba mkumbùke dr ulimboka alipokuwa ametelekezwa ktk msitu wa pande akiwa hajiwezi,raia ndo walimwokoa.Je sisi raia tunaoteseka na magonjwa mnatusaidiaje maana kama sio sisi dr ulimboka pengine asingekuwepo.Tupeni mbadala basi angalau tufanyeje,nyie tu ndo mnaotawala nchi hii kwa sasa sio serikali ya ving'ora na mizinga.
   
 2. M

  McMuga Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona simple hilo!,na nyie andamaneni kwenda ikulu,hapo serikali italegea. Sio unakaa unalalamika tu.
   
 3. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Manyaunyau tufae wenzio basi, lakini punguza gharama kidogo!
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Segwanga hivi umewahi kujiuliza swali iweje vyombo vyote ambavyo vimewekwa kusimamia haoja mabzo madakatari wanazipigia kelele kama vile bunge, vyama vya wafanyakazi n.k vimeshindwa kiasi inafika hatua kuwa bila ya madakatari wenyewe kujisimamia hakuna kinachofanyika miaka nenda rudi? Ukumbuke kuwa dai kuu la madkatari hawa ni kuborshwa kwa mazingira ya kutolea huduma za matibabu ikiwemo kuwepo kwa hospitali za kutosha, wodi za kutosha za kulaza wagonjwa na kuwepoa kwa vifaa vya tiba vya kutosha na dawa. Mathalani katika bajeti ya mwaka huu Wizara ya Afya iliomba Bilioni 198 kusambaza dawa katika hospitali za Serikali kwa njia za kujibana sana lakini imetengewa Bilioni 78 tu pungufu ikiwa ni Bilioni 120 ilihali fedha za posho na safari zimetengwa zaidi Bilioni 500. Ni kuitokan na hali hii madkatari wamesema kabisa wamechoka kuwashuhudia watanzania wenzao wakipoteza maisha kwa kukosekana vifaa vidogo vidogo vya matibabu tena vyenye gharama nafuu sana kila mwaka. kwa kuwa vyombo vilivyowekwa na Katiba na Sheria vinaonekana kushindwa majukumu yao ya kuisimamia Serikali ili iweze kuelekeza fedha za kutosha katika sekta za huduma za jamii kama hii ya afya, ilihali wakijirundikia fedha nyingi kila mwaka madakatari nao wameamua waanze kujiteta wenyewe ili angalau kuweza kumudu kuboreshea mazingira ya kufanyia kazi.

  Hebu sama hapa chini ni kwa vipi chombo kama bunge kinavyokwazwa na kushindwa kusimamia Serikali ili ielekeze raslimali nyingi katika sekta ya afya:-

  [h=2]MNYIKA-Taifa na Madaktari: Tumefikia hapa tulipo kwa sababu ya Rais Kikwete na Bunge[/h]
  Sababu ya hali tete ya nchi na maisha ya wananchi kwenye sekta ya afya ni udhaifu wa serikali na uzembe wa bunge. Rais Jakaya Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka Steven na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro. Spika Anna Makinda aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha.
  Taifa limeingizwa kwenye hali tete katika sekta ya afya na maisha ya wananchi wanaotegemea huduma toka hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma yapo mashakani.
  Tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa serikali wa kushughulikia matokeo badala ya chanzo cha mgogoro wake na madaktari na uzembe wa bunge katika kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi kusuluhisha pandembili zinazolumbana kwa gharama ya vifo na nyingi kwa wagonjwa wasio na hatia.

  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianza ikashindwa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijaribu akashindwa, Rais Jakaya Kikwete naye akaingilia kati kuondoa udhaifu uliokuwepo naye anaelekea kushindwa; kwa kuwa wote wanashughulikia matokeo ya mgogoro badala ya chanzo.
  Chanzo cha mgogoro wa serikali na madaktari na wananchi kuhusu sekta ya afya ni bajeti finyu inayotengwa na serikali na kiasi kidogo cha fedha kinachotolewa katika sekta hii nyeti, na hivyo kushindwa kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari kwa upande mmoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kwa upande mwingine.

  Rais Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro:
  Hatua ya serikali kukimbilia mahakamani na kutumia kivuli cha mahakama kukwepa kushughulikia madai ya msingi ya madaktari ni kuendelea kushughulikia matokeo na hivyo kuendeleza migogoro na migomo.

  Hata kama serikali ikitumia vyombo vya dola kukamata au kujeruhi madaktari, inapaswa kutambua kwamba mgomo wenye madhara makubwa kwa nchi umekuwa ukiendelea chini chini kwa muda mrefu kwenye sekta ya afya nchini na kuchangia vifo vya wananchi kwa magonjwa yanayotibika kutokana na huduma mbovu na kukosekana kwa madawa na vifaa tiba katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma.

  Rais Kikwete anapaswa kujitokeza na kutoa ahadi ya kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuongeza fedha za bajeti ya afya katika mwaka wa fedha 2012/2013 kupitia mkutano wa nane wa bunge unaoendelea hivi sasa ili kushughulikia chanzo badala ya kupanua wigo wa migogoro katika taifa.
  Aidha, Rais Kikwete anapaswa kutumia nguvu zake za ukuu wa nchi na uamiri jeshi mkuu kulaani tukio la kutekwa, kuteswa na kutaka kuuwawa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dr. Ulimboka Stephen ambapo baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa vyombo vya dola wanatuhumiwa kuhusika. Ili kurejesha imani juu ya Serikali na vyombo vyake badala ya kutegemea jopo la wapepelezi kutoka jeshi la polisi pekee ambalo nalo baadhi ya vituo vyake Jijini Dar es salaam vimetuhumiwa, Rais Kikwete aunde tume huru ya kuchunguza tukio husika ambalo limeongeza madoa kwa nchi kitaifa na kimataifa.

  Spika aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha:
  Kwa kipindi cha takribani miezi minne nimetumia njia za kibunge kutaka suala la madai ya madaktari lijadiliwe bungeni ili kushughulikia chanzo badala ya matokeo hata hivyo hitaji hilo la kikatiba limekuwa likipuuzwa na kusababisha bunge lizembee kuchukua hatua kwa wakati kuepusha mgogoro na mgomo.

  Izingatiwe kwamba katiba ya nchi ibara ya 63 (2) inatamka kwamba "Sehemu ya pili ya bunge (yaani wabunge) ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba".
  Nawaomba wananchi wa Tanzania waliotutuma kuwawakilisha kumtaka Spika Makinda na wabunge wote kuwajibika kujadili bungeni hali tete ya sekta ya afya nchini na kauli tata za serikali katika kushughulikia hali hiyo. Spika, uongozi wa bunge na wabunge kwa pamoja tutakiwe kukataa visingizio vya serikali vya kutumia mahakama kuathiri haki, kinga na madaraka ya bunge ya kuisimamia serikali juu ya suala la madaktari na hali ya sekta ya afya nchini.

  Hivyo; wabunge, umma na wadau wa haki za binadamu tuungane pamoja kutaka Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyoshughulikia suala la madai ya madaktari itolewe bungeni na hadharani na bunge liruhusiwe kutumia mamlaka yake ya kuisimamia serikali kujadili taarifa hiyo na kupitisha maazimio maalum ya kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea na pia kuboresha hali ya huduma katika hospitali, vituo vya afya na zahanati inayoendelea kutetereka.
  Kanuni ya 64 (1) (c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayoelekeza kwamba "Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika bunge, mbunge hatazungumzia jambo lolote ambalo linasubiri uamuzi wa mahakama"; inatumiwa vibaya na serikali kuficha udhaifu na kudhibiti mamlaka ya bunge kwa kisingizio cha mahakama.

  Hata hivyo, zipo njia zaidi ya nne ambazo umma unaweza kutaka spika na wabunge wazitumie kukwepa bunge kuonekana linazembea kuchukua hatua za kuisimamia serikali na kuokoa maisha ya wananchi katika hatua hii ya dharura.

  Mosi, hoja inaweza kutolewa ya kutengua kanuni husika kuliwezesha bunge kujadili Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu madai ya madaktari kwa kuwa imekuwa kawaida kwa serikali kutoa hoja za kutengua kanuni wakati mwingine kuilinda serikali na kupunguza madaraka ya bunge. Mathalani, kanuni ya 94 inayolitaka bunge kukaa mwezi Februari kama Kamati ya Mipango kutoa mapendekezo ya mpango wa taifa, ilitenguliwa na matokeo yake ni kuwa serikali iliandaa bajeti ikiwemo ya sekta ya afya na kuwasilisha mwezi Juni bajeti ya serikali isiyozingatia kwa ukamilifu mpango na madai ya madaktari.

  Pili, Spika anaweza kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni 114 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kutaka kamati husika ya bunge kukutana kwa dharura na kuishauri wa haraka serikali kufuta kesi iliyoko mahakama kuu kitengo cha kazi ili kulipa fursa bunge kutumia madaraka yake ya kikatiba kujadili na kupitisha maazimio ya kuweza kusuluhisha pandembili za mgogoro badala ya mahakama. Uamuzi wa kurejea mahakamani unapaswa kuwa wa mwisho baada ya hatua zingine kushindikana.

  Tatu; Spika kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni ya 114 (17) na 116 kuitaka Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kupatiwa na kupitia nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, na kuandaa taarifa maalum ya masuala yanayoweza kujadiliwa bungeni bila kuingilia suala lililo mahakamani. Izingatiwe kwamba Serikali imefungua kesi dhidi ya Chama Cha Madaktari (MAT) na haijafungua kesi dhidi ya Jumuiya ya Madaktari na Taasisi zingine katika sekta ya afya; hivyo kufunguliwa kwa kesi hiyo hakuwezi kulizuia bunge kujadili masuala mengine yanayohusu madaktari na sekta ya afya nchini.

  Nne; Kanuni ya 53 (2) au 47 (1) za Kanuni za Kudumu za bunge inaweza kutumiwa kwa Waziri husika kwamba suala la namna ambavyo serikali imejipanga kutoa huduma katika hospitali kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea au mbunge yoyote kutoa hoja kuhusu hali kwa sasa ilivyo katika hospitali na sekta ya afya kwa ujumla kufuatia kuendelea kwa mgogoro kati ya serikali na madaktari na masuala hayo yakajadiliwe. Izingatiwe masuala hayo hayahusu mgogoro ulioko mahakamani bali ni ya dharura kwa ajili ya kuepusha madhara zaidi kwa wananchi na nchi kwa ujumla wakati taifa likisubiri taratibu za mahakama kukamilika.

  Ni muhimu umma ukapuuza taarifa isiyokuwa ya kweli iliyotolewa na Naibu Spika Job Ndugai bungeni tarehe 27 Juni 2012 ya kudai kwa tayari kamati ya huduma za jamii imewasilisha taarifa yake bungeni wakati ambapo taarifa hiyo iliyohusisha kazi ya kubwa ya kamati na matumizi ya ziada ya fedha za wananchi imefanywa kuwa siri hata kwetu wabunge. Naibu Spika Ndugai kwa kauli hiyo amekwepa kutekeleza muongozo wake mwenyewe alioutoa katika mkutano wa sita wa bunge mwezi Februari mwaka 2012 kwamba baada ya kamati kumaliza kazi yake taarifa ingewasilishwa bungeni na kujadiliwa. Tayari nilishamuandikia barua Spika tarehe 27 Juni 2012 kupuuza maelezo hayo ya Naibu Spika na kutoa kwa wabunge na bunge taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii ili wabunge tusiendelee kupokea kauli za upande mmoja wa serikali bila kuwa na maelezo na vielezo vya upande wa pili wa madaktari.

  John Mnyika (Mb)
  Bungeni-Dodoma
  28/06/2012
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  WATANABE nakubalìana na ww kuwa serikali ndio iliotufikisha hapa tulipo nachoomba madoç wangetusaidia kwa namna moja au nyingine kuwa wakati wanamalizana na serikali wananchi tutakuwa tunapata matibabu sehemu gani kama ni private hosptal aù kwa waganga wa kienyeji.Walichokifanya ni kama baba mwenye nyumba anaondoka na anaiacha familia yake haina chakula na hajawapa alternatives za kupata chakula
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  WATANABE nakubalìana na ww kuwa serikali ndio iliotufikisha hapa tulipo nachoomba madoç wangetusaidia kwa namna moja au nyingine kuwa wakati wanamalizana na serikali wananchi tutakuwa tunapata matibabu sehemu gani kama ni private hosptal aù kwa waganga wa kienyeji.Walichokifanya ni kama baba mwenye nyumba anaondoka na anaiacha familia yake haina chakula na hajawapa alternatives za kupata chakula
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. J

  Jimy P Senior Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdaktari wanahitaji Mshahara wa Milioni 3.5, Katika nchi Maskini ni Vigumu kulipwa mshahara huu, Nadhani wafanye Analysis kama inawezekana kwani kwa sasa anayetoka Chuoni analipwa Kuanzia Laki Tisa, Na Serikali imewaongezea Posho walizokuwa wanahitaji isipokuwa la kulipwa mshahara huo na nadhani imefika wakati kama unaona kazi unayofanya hailipi badilisha kazi au usisomee kitu ambacho halilipi, nawashauri wote wanaosoma Udaktari na Wanaotarajia kusomea kama unadhani hailipi au Ukimaliza Chuo lazima uajiriwe na Serikali usisome au acha unachosome somea kitu kingine,

  Nadhani imefika wakati tujue kuwa Professional nyingine ni muhimu pia kama wanavyodhani Madaktari wao ni muhimu zaidi halafu Board ya mikopo inatoa asimilimi 100% kwa wanafunzi wanaosomea Udaktari hizi ni Kodi za Watanzania ambazo lazima muwatumikie,

  Idara ya afya ni miongoni mwa idara zinazooongoza kwa Rushwa Tanzania,

  Madakri wamegoma kuwatibu Watanzania lakini Dr Ulimboka kafika wameacha Mgomo wameenda kumshughulikia wanaacha watanzania wanaendelea kufa

  Madaktari mnachelewa ofisini, mnapokea Rushwa haya yote hamsemi mtayerekebisha vipi,

  Umefika wakati Serikali kutumia Sheria za Utumishi la sivyo itafika sehemu Watumishi wote wa Serikali wahitaji Milion 3.5

  Viongozi wenye dhamana fanyeni maamuzi magumu whether is wrong or Right,
  Mhe EL Alishawahi kusema Msiogope kufanya Maamuzi whether is wrong or Right.

  Mhe Waziri mkuu kila kitu lazima mseme Top Leaders kwani huko mikoani hakuna viongozi au Wilayani.
  Watekeleze wajibu wao na Fanya Maamuzi kama kiongozi Mkuu wa serikali lazima mbadilike ili nchi iende.
  Hao wanaotaka kushika nchi watanzania wanafikiri hawatacheka na mtu anayekwenda kinyume na Sheria Na taratibu za Kazi na ndivyo itakuwa hivyo
   
 8. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama serikali ndio tatizo kwanini wawagomee wagojwa!Madaktari waliogoma ni maadui wa uhai!wameweka maslahi mbele kuliko wagonjwa na kwa sisi watanzania tulio wasomesha!Tuliwasomesha ili watutibu na si ili watuache tufie hospitali huku wao wakinywa bia Vilabuni!Wale wanaojidai wanapigania haki za binadamu sina imani nao tena!
  Nitasikitika sana kama serikali haitawachukulia hatua watu wote ambao ni chanzo cha mgomo!
   
 9. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,003
  Trophy Points: 280
  Cha kufanya hapo tunaenda kwenda hospital za private
   
 10. THE STORM

  THE STORM Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 15
  INFACT ILITAKIWE TULIPWE MILIONI KUMI NA TANO,KWA KUWA MTU KAMA MAJI MAREFU ANALIPWA MIL 10!
  OFCOURSE TUMEGUNDUA HAILIPI NDIO MAANA TUNAACHA UKATIBU WEWE K.M. MKUBWA!
  TUNAFANYA MASTERS ZA FANI NYINGINE KWA SASA,SO WEWE WAHI UKATIBU!
  HIVI WEWE K UNAFIKIRI WAZAZI WETU NA NDUGU ZETU WENGINE HAWALIPI KODI AU!!??NO WONDER WE SI DR!
  YAA NI KWELI,MG WETU KWA SASA NI SIR ULI PEKE YAKE WAKO MPELEKE INDIA!
  NI DHAHIRI KUNA BWANA YAKO ALIYEKUFANYA UANDIKE HUO ***** WAKO HAPO JUU VINGINEVYO UTAKUWA NI SHOGA AU NDIO HIO ULIYO ITAJA!NAOMBA NIKUJULISHE CLINICAL MEETING HUANZA SAA MOJA NA NUSU BILA KUKOSA NA DR ALIYEKESHA KUMUUDUMIA MKEO AKIJIFUNGUA NDIO ANATOA REPORT YA USIKU MZIMA!
  KWA MTAZAMO WANGU MAAMUZI MAGUMU NI KUWAPA WABUNGE LAKI TISA NA MA DR MIL KUMI KWA MWEZ!KUWAPA NYUMBA NA MAGARI ILI WASICHELEWE KAZINI!KUWAPA WALIMU HAKI ZAO NA MISHAHARA KWA WAKATI!
  KUMTEKA MTU NA KUMTESA NI KINYUME NA SHERIA KABISA!!NI UDHARIMU,UDICTATOR,USHENZI NA UDHAIFU!EMBU JIOKOE KUTOKA UTUMWA WA MAWAZO WE FA.L$#a!HUONI AIBU!NINGEKUJUA NINGEKUOVERDOSE MLY MKB WEWE!
   
 11. THE STORM

  THE STORM Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 15
  hivi wewe unatumia masaburi kufikili!!!!???wewe umemsomesha daktari wapi wewe!kwanza kwa kauli zako sidhani unalipa kodi kabisa wewe!
  Nimeumia mara nyingi kwa kushuhudia watz maskini wakifa,lakini nikikujua walah nita tabasamu ukikata roho!damu ya uli mtailipa tu,iposiku yako wewe!
  Chukukueni hatua zote mak wakubwa nyie!si mmetufukuza kazi??!!??!!kaleteteni wachina pumbaf wakubwa!liwalo na liwe ikibidi hata mama yako afe,ingawa najua hajui mtoto wake ushakua hivyo!
   
 12. m

  muchetz JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45

  Hapa inaonyesha uko disconnected. Unaongea kama vile haujui, lakini ukweli unataka kupotosha. Wabunge(mfano tu) tayari wanalipwa zaidi ya milioni 6 ( na kuna tetesi watajiongezea mpaka 10 milioni). Kwahiyo inawezekana. Labda useme haiwezekani isipokuwa kwa wezi wetu!!!!
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Segwagna nashukuru kwamba umeanza kuelewa ila una tatizo katika kutambua nini maana ya Serikali. Serikali ni mimi, wewe, yule n.k; hata madakatari ni sehemu ya serikali, na sio kikundi cha watu wachache waliopora hatamu za uongozi kwa manufa yao binafsi kama ilivyo hapa nchini ambapo watu wachache ndani ya CCM wamepora hatamu hizo.

  Umetoa mfano kuwa kitendo cha madajatari ni sawa baba mwenye nyumba kuondoka na kuacha familia haina chakula, madakatari sio wa kwanza kufanya hivyo mwaka 1991 CCM ilipopitisha azimio la Zanzibar na kufuta lile la Arusha ndipo Baba mwenye nyumba CCM alipowatelekeza watoto wake yaani Watanzania katika nyumba iitwayo Tanzania. kama utakuwa umesoma waraka wa mbunge Mhe John Mnyika vyema utagundua uhuni uliofanywa na CCM na kikundi cha watu wachache wajiitao serikali kukwepa kutekeleza makubaliano waliyoingia na madakatari.

  Kuhusu kutibiwa hospitali za binafsi, hilo sio jukumu la madakatari bali jukumu lako wewe na mimi ambao ndio tunaoiweka serikali madarakani tunapaswa kuipima na kuihuikumu kwa matendo yake ya kushindwa kutenga fedha za kutosha kuwalipa madakatari na kuwapatia vifaa vya kutupatia matibabu bora ilihali serikali hii hii ikishamirisha zaidi ufisadi

  Serikali imetangza kuwa kuanzia sasa itaingia mikataba na hospitali binafsi ili watanzania wote tukatibiwe huko ambako kuna vifaa na hospitali hizo zitawaajiri madakatari hawa hawa ambao serikali haitaki kuwalipa na kuwapatia vifaa vya kuwapatia watanzania matibabu. Kwangu mimi pia naona huo kuwa ni mpango mzuri kwa kuwa serikali hii dhaifu imeshindwa kabisa kupanga na kusimamia sekta ya afya kama sekta mojawapo ya umma ambapo imgesimamiwa vyema ni gharama nafuu kuliko kuwapeleka watanzania wote kutibiwa hospitakli za binafsi. Kwa madini na raslimali tulizo nazo watanzania zinzweza kabisa kutuhakikishia matibabu mazuri zaidi katika hospitali zenye vifaa bora na vya kutosha vya tiba na madakatari na wauuguzi wenye kufanya kazi kwa moyo kutokana na malipo mazuri isipokuwa huu ufisadi wa CCM ndio unasababisha matatizo yote haya.

  Mwisho nataka ukumbuke kuwa katika madai 10 ya madakatari madaia 7 ni ya kutaka kuboreshwa kwa mazingira ya kuwapatia matibabu watanzania ambayo kwa muda mrefu mazingira hayo yamesahaulika kabisa mfano halisi jana katika taarifa ya habari ta ITV imetokea ajali ya akina mama wawili waliokuwa wawepanda pikipiki kukanyagwa na gari kubwa wakafikishwa hospitali ya rufa ya Bombo Tanga, hakuna kifaa cha XRAY, hivyo madakatari wachache wa dharura waliokuwepo wakashindwa kuendelea kuwahudumia akina mama hao. Ni dhahiri kwa hali zao watapoteza maisha kwa kukosa huduma kutokan na hospitali ya serikali kukosa kifaa cha X-ray. Gharama ya shangingi moja analopanda waziri wa tanzania lina uwezo wa kununua vifa vya X-ray kwa hospitali 3. Kadhia kama hizi ndio madaia 7 ya madaktari; tuache kusikiliza propaganda za CCM na vyombo vya serikali yake tutafute ukweli na kiini cha matatizo na tuchukue hatua
   
 14. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Jimy P labda ni wewe ndio unaishi nchi maskini, lakini mimi mwenzio ninaisha nchi tajiri sana hapa duniani iitwayo Tanzania ambayo ni moja ya nchi zinzoongza hapa duniani kwa kuchimba dhahabu, Tanzanite, inaoongoza kwa kuwa mbuga nyingi na za kuvutia za wanyama, ardhi kubwa yenye kufaa kilimo inayoweza kufikia ukubwa wa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zikichanganywa pampja, ina mito na maziwa gesi inatotirirka yenyewe, mafuta yanyotiririka yenyewe, uraniuma katika kila pembe ya nchi n.k

  Kutokana na usimamizi mbovu wa uchumi toka CCM na Serikali yake katika nchi tajiri kama hii wastani wa bei za bidhaa ni kama ifuatavyo kilo moja ya Mchele ni Shs 2,000/= na zaidi; Sukari ni shs 2,000/= na zaidi unahitaji si chini ya Shs 20,000/= hadi 30,000/= kujaza mafuta katika gari kwa siku kwenda na kutoka kazini tu kwa kuwa zaidi ya masaa 6 hupotea katika foleni huku injini za magari zikinguruma.

  Sasa katika mazingira kama haya mshahara wa Shs 3,500,000/= ambao ni sawa Shs 116,666/= kwa siku utanunua nini katika hali ngumu ya maisha kama hii? unatarjia vipi dakatari ajitolee kuchezea damu yako hajui kama ua ukimwi au la katika kupata kiwango hiki duni ambacho wabunge licha ya kupata Mshahara wa Milioni 6 walilalamika kuwa gharama za maisha ziko juu hivyo posho ya kukaa ya Shs 80,000/= kwa siku moja haiwatoshi (SIo mshahara). Katika bajeti hiii mshahara huo umepandishwa toka Milioni 6 kufikia Shs Milioni 10; je kati ya Mhe Komba na Wassira (Wabunge) wanaochapa usingizi huko bungeni na madkatari nani anastahili kulipwa Milioni 10?

  Umezungumzia kodi inayotumika katika Bodi ya mikopo mimi nilifikiri kama kweli una uchungui na fedha za kodi kwanza ungeanza kuzungumzia fedha za kodi zinazopotea kila mwaka kwa njia za ufujaji soma ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Serikali.

  Amkeni watanzania wenzangu na tuache kujifinyanga katika prpaganda za CCM na Serikali yake.
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Si mliambiwa mtatibiwa LUGALO na hospitali nyinginezo zote za JESHI! Sasa ndugu huko unakoishi kama hakuna LUGALO basi nenda JESHINI waambie umekuja kutibiwa kwa maagizo ya Mzee LIWALO NA LIWE!!
   
 16. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mkweche inaelekea hauna elimu ya kutosha kuhusu haki zako kikatiba. Hivi lini wewe kama raia ulikaa chini na cha ma cha Madakatari na kuahidiwa kupata huduma bora za afya? lakini natambua kama raia yupo mtu (JK) na kikundi chake (CCM) walikuita katika mkutano na kukuahidi uwachague na watakupatia huduma za afya. Sasa iweje leo Mkweche upoteze muda kuwasema madakatari ambao ni watumishi tuu wa hao waliokuahid?

  Sisi kama raia tunataka kuelekezwa wapi pa kwenda tukiwa na matatizo ya kiafya tukifika huko tukakuta madakatari ni wachana, wacuba, wazungu ama ndugu zetu hii sio kazi yetu;ni kupta huduma bora za afya kama tulivyoahidiwa.

  Hivi sasa Serikali imetangaza kutumia hospitali za binafsi kuwapatia watanzania huduma za afya, tusubiri tuone kama hospitali hizi zitaweza kusamba nchini nzima katika kipindi kifupi ikiwa katiak miaka 50 Serikali za TANU na CCM zimeshindwa kusambaza hospitalia nchi nzima kiasi cha kulazimika kutumia hospitali za madhehebu ya dini.

  Ni imani yangu kuwa kwa wingi wa madini Tanzania iliyonayo inawezekana kabisa kuanzshwa mpango wa huduma ya afya ya umma ambao utapelekea kuwepo hospitali zenye vifaa vyote vya huduma katika ila penbe ya nchi hii badala ya utaratibu wa sasa wa kifisadi ambapo mabilioni hutengwa kila mwaka kwa ajili ya sekta ya afya na kuishia kujenga maghorofa ya watu wachache.

  Mkweche ukumbuke kuwa kisingizio kuwa Serikali haina fdha za kutosha kuwapatia watanzania huduma bora za afya ilikuwa ikikubalika enzi za utawala wa Mwalimu Nyerer kwani kwa makusudi aliamua taifa kutochimba madini na kuyatuzna kwa vizazi vijavyo; na vizzi vyenyewe nidio sasa ambapo tunachimba kila aaian ya madini yaliyopo hapa nchini. Sasa iweje CCM na Serikali yake ishindwe kutekeleza ahadi9 ya kutoa huduma bora za afya ilihali inasemehe kodi ya Dola Bilini 1 za Kimarekani kwa mwaka?
   
 17. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimejaribu sana kuwakumbusha hilo, lakini hakuna anaye nielewa! Wengi wanazungumzia mambo ya SIASA zaidi tumesahau UTU! Mimi hili linanisikitisha SANA.
   
 18. M

  Maboga Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na mleta mada kwani hili ni suala muhimu sana. Kwa hali ilivyo sasa sioni uwezekano wa madaktari peke yao kutoa tamko kwamba wanarudi kazini. Suala hili linahusisha pande mbili Serikali na Madaktari. Tatizo ninaloliona ni serikali kuamua kufunga uwezekano wa majadiliano kwa kisingizio cha mahakama. Ina maana itasubiri kesi iendeshwe na hukumu kutolewa huko mahakani ndipo wananchi warejeshewe huduma kamili (na siyo huduma kiraka au bandia)? Hii itachukua miaka mingapi ukizingatia mwenendo wa kesi za mahakani katika nchi hii? Amri ya mahakama na vitisho vitarejesha ari ya kazi kwa madaktari? Punda unaweza kumpeleka kisimani lakini anaweza kuamua asinywe maji. Tuisihi Serikali na Mahakama ilirejeshe suala hili kwenye meza ya mazungumzo katika ngazi zote-madaktari na serikali, hata ndani ya bunge. Hilo tu ndilo litarejesha ari ya madaktari kutimiza wajibu wao na kuwarejesha kazini kiukamilifu wakati uchunguzi wa suala la daktari unaendelea na kesi kuendelea. Tunaomba hekima iwasaidie madaktari na serikali katika kulimaliza suala hili. Kuwafukuza madaktari kunaongeza fujo na kunaweza kukawa kichocheo cha kuwafanya wahamie nchi nyingine zinazowahitaji.
   
Loading...