Madaktari, hamjaona njia nyingine zaidi ya MGOMO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari, hamjaona njia nyingine zaidi ya MGOMO?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimox Kimokole, Jun 26, 2012.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimetazama Star TV leo asubuhi, Mtangazaji Baruhani Muhuza aling'ang'ania kuuliza "Hivi hakuna njia nyingine ya kuchukua zaidi ya hii ya Mgomo?" hata baada ya kuelezwa kwa ufasaha hatua zilizochukuliwa.

  Kwa kweli nilikereka sana na swali hili la mtangazaji, nikamuuliza nikiisemesha TV yangu kwa hakika nikijua kabisa hanisikii "Hebu toa njia nyingine uliyonayo ili Madaktari wachukue, toa basi" sikupendezwa na namna alivyokuwa king'ang'anizi bila kutoa ufumbuzi kama anao.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nawashangaa wana habari ni kwa nini hawakufuatilia mwenendo wa mazungumzo kati ya pande hizi mbili kwa kipindi chote cha siku tisini.wao husubiri madaktari wagome na kuanza kuuliza maswali ya kitoto au kusema ''wananchi ndio wanaoumia''
  waandishi makini walitakiwa kufuatilia nini kinaendelea baada ya migomo ya kwanza.
   
 3. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Kimokole na Wana JF,
  Umefika wakati wa hawa watu wachache kupewa darasa atleast waushughulishe Ubongo kwenye suala la Kufikiri.
  Unazi na kujali matumbo na upande fualani umepitwa na wakati. Inaonyesha jinsi mwandishi ambavyo hakufikiri pamoja na kuelimishwa.
  My Take: Issue kama hii ya Madaktari inapakiwa iangaliwe kwa umakini na pande zote mbili, sio upande wa madaktari tu, kluna Waalimu, Polisi na wengine.
  Nawakilisha

   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Ngoja huyo Mtangazaji Baruhani Muhuza apate na kuumwa ndipo atakapojuwa umuhimu wa Ma Daktari kwanini Wanagoma?

  Mtangazaji Mzima anazungumza maneno ya Pumba ahhh? Nchi yetu inakwenda kinyume nyume. huyo mtangazaji atakuwa ni

  mamluki aliyetumwa na Viongozi wake Wakubwa huyo hafai kutangaza habari kwenye TV. Mshamba mzima Mtangazi gani

  hajuwi Umuhimu wa Ma Daktari hapo nchini kwetu?Pasipo na Madaktari nchi yetu kweli hao Wagonjwa si Watakufa kama nzi

  tu? Huyo Mtangaji
  Baruhani Muhuza aache Pumba zake kwenye TV.Mkuu Kimokole
   
 5. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuna haja ya hawa wanaHabari kujitathmini upya kwa kweli. Wanaweka hisia zao zaidi kwenye mambo ya msingi tena wakitazama upande mmoja tu bila kufungua bongo zao
   
 6. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MziziMkavu kuna watangazaji wanakera kwa kweli, hata sijui ilikuwaje wakawa watangazaji
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Sifa za Mtangazaji inatakikana awe Mkweli wa Habari na asipendelee katika kueleza habari zake.

  Akiwa anapendelea chama fulani au au Serikali basi huyo sio Mtangazaji hafai kuwa Mtangazaji lakini Wengi Watangazaji ni Waongo na ni Watu wa Serikali haswa ukizingatia nchi zetu za ulimwengu wa 3 hakuna haki za KiBinadamu Mtangazaji

  akisema ukweli basi anaweza hata kupoteza maisha yake. Lazima Watangazaji katika nchi zetu za Ulimwengu wa 3 wawe

  hao Watangazaji wanapendelea Serikali hata kama hiyo Serikali ni ya Kidickteta ndio wataweza kuishi salama Wengi wa hao Watangazaji ni Waongo na wanaotoa habari za uongo kuipendelea Serikali iliyoko Madarakani.Mkuu Kimokole
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shilingi wengi tunajua ina pande mbili ila iko ya tatu hatuijui, hawa watangazaji mawazo yao ni finyu kwenye Tasnia ya habari. Kazi kweli tunayo...
   
 9. e

  ellyjr8 Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
  Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
  HALI HALISI HOSPITALINI:
  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
  Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
  1. Madai ya madaktari yalianza lini?
  2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
  3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
  4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
  5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

  SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
  Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

  VYOMBO VYA HABARI:
  Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
  Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
  Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
  Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
  MKAKATI:
  Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
  1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
  2. Wanatumia pesa ya nani?
  3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
  KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
  KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

  MAKOLIGI (colleague)??
  Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
  Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
  ..Solidarityforever..
   
Loading...