Madaktari Bingwa wa Bugando na Ubingwa wa Kulipua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Bingwa wa Bugando na Ubingwa wa Kulipua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Sep 3, 2009.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wiki iliyopita Muungwana mmoja alikwenda Kutibiwa Bugando, Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa --- alipofika mapokezi akaambiwa hana appointmenta kwa hiyo hawezi kutibiwa vinginevyo alipe shilingi 10,000 ili akatibiwe Private.

  Akalipa na kupangiwa Daktari Bingwa wa Kichwa, Kifua na Sikio --- folebi ilikuwa ndefu sana na hata maana ya Private ikakosekana -- na hapa swali likawa hiyo 10,000 nani na nani wanainywa Je na Daktari mhusika anapata mgawo?

  Haya, Dada mmoja aliyekuwa anasajili wagonjwa wa kuingia ndiyo alikuwa Kiboko, nadhani yule mama ni kama mwenyeji wa kaskazini, akawa mara anapokea simu anatoka na kuingia ofisini, akipigiwa simu anatoka hata muda wa dakika 20 hivi.

  Hata waliotibiwa ili kupata sasa tarehe ya kurudi nao ilikuwa kazi kujaziwa kwenye kadi, huyo dada alikuwa akijivuta na kutoka karibu kila mara hadi nikahisi kuna kicheche anamsumbua, maana simu zilikuwa hazikatiki, kama ameolewa sijui????

  Kutoka hiyo saa tano asubuhi aliyokwenda muungwana alitibiwa saa kumi jioni na wengine walikuwa bado wanalalama maana walifika pale asubuhi lakini walizidi kung'aa macho.

  Haya Ingia sasa kwa Daktari Bingwa, Kwanza akaitwa Muungwana baada ya kumuangalia kama dakika mbili tatu hivi Daktari bila kuuliza historia ya ugonjwa akaanza kuandika dawa, baadaye akaja Mwarabu mmoja akamchukua Daktari Bingwa na kukaa naye pembeni wakati amemuacha Mgonjwa, baadaye aliporudi akaandika dawa na kumpa Mgonjwa Cheti, bila hata ya kumuambia tatizo lake ni nini.

  la kujuliza Je hapa je huu ndiyo utaratibu wa Madaktari Bingwa tena ambaounalazimika kulipia ili uwaone, lakini je Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando unayajua hasa na Hasa Mkurugenzi ambaye huteuliwa na Rais?

  Kama madaktari Bingwa wa Kibiongo ndiyo hawa kwa nini hospitali za Rufaa Tanzania zisiwe makazi ya vifo.:confused:
   
 2. c

  chach JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 433
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Ndiyo utaratibu wa bongo eti hakuna migomo ya madaktari kwa sababu kazi yao ni ya wito na nyeti.Uliyoyaona ndo migomo yenyewe.
   
 3. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  NI kweli naamini kuwa kuna mgomo wa aina fulani hivi
   
 4. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kwa madaktari huu ni Mgomo baridi na kuna Daktari mmoja ananiambia siyo jambo la kawaida kwa daktari kutoamuambia mgonjwa tatizo lake.
   
Loading...