Madaktari bingwa Muhimbili kuanza mgomo kimapinduzi Jumatatu

Kuna mod mmoja hivi mjingamjinga.

Taratibu kiongozi,watakupoteza tena na kwa kipindi hiki tunahitaji mno michango ya wa wadau kama wewe hapa ukizingatia kwa sasa jf inapita katika kipindi kigumu likiwemo tishio la kufungiwa,kama ulivyoona ama kusikia leo bungeni Mchgj Dr Lwakatare akiongea kuhusu Jf
 
Hivi we huwajui watu wa kule?
Du kweli maMod kiboko unaweza kuukosa uhondo wa JF ukiwachokoza, mm nawaheshimu bora ukimbilie kwenye mahusiano au mambo ya kikubwa
kwa ujumla mm napinga wabunge kulipwa 330,000 hivi ni lazima kuwa na wabunge katika inji hii kuliko madaktari
maana mwisho wa yote tutafumuka na sisi wa majumbani kuunga mgomo huo
tafadhali mwenye ubavu aanzishe topic ya kuwapumzisha wabunge hadi 2015 tuwaokoe Madaktari waliosoma
mm nikisogea huko Bannnnnnnnnnnn
 
I support the doctors wana hoja hata kama hazitekelezeki wasikilizwe mezani kauli za ubabe hazijengi.
 
Mponda/Mpondwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaarghhhhhhhhhhhh, tumechoka!
Kwani kuwakamata akina Mponda,
Na kuwapondaponda,
Watanganyika wapendwa,
Tunasubiri nini kupewa?
 
I just new it, serikali inajidai kuzima moto kwa kutumia petrol, MATOKEO YK YATAKUA MABAYA KULIKO WALIVYODHANI
 
Hivi mgomo umeisha kwa maana kwamba serikali imefikia muafaka na hawa drs or?!!!wamerudi kazini?naona tamko la serikali wala hakuna hitimisho linalotamkwa?wamefukuzwa kwa mjibu wa kauli aliyoitoa PM au??jamani mbona maluweluwe tu???????
 
Madakatri Bingwa katika hospitali ya taifa Muhimbili wamefanya kikao cha dharura kujadilli hutuba ya Bwana Mponda na kukubaliana kuanza mgomo kupinga taarifa iliyotolewa na serikali Bungeni; Aidha katika taarifa yao ambayo itatolewa baadae naDr Ulimboka inaomba kada nyingine za Afya na zisizo za Afya kama Walimu kuunga Mkono Mgomo huo mkubwa na wakimapinduzi
Mbona hii taarifa siielewi,
Kwani Dr Ulimboka ni kiongozi wa Ma Daktari bingwa au kamati maalum ya MAT ?
 
TAARIFA YA KAMATI YA MUDA YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI KUFUATIA TAMKO LA BUNGE (ILIYOTOLEWA LEO KWENYE VYOMBO VYA HABARI);

B
aada ya taarifa ya bunge kuwasilishwa leo ijumaa, kamati ya madaktari inaazimia haya yafuatayo;
• Kamati inalishukuru bunge la jamhuri ya muungano kupitia mwongozo wa spika kwa kuiagiza kamati ya kudumu ya huduma za jamii kuanza kazi mara moja ya kukutana na jumui...ya madaktari.
• Kamati pamoja na jumuiya ya madaktari ipo tayari kukutana na kamati ya huduma za jamii.
• Kwa kuwa suala hili ni la umuhimu na dharura kubwa, Mkutano wa jumuiya ya madaktari unatarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 04/02/2012 kuanzia saa 4 asubuhi.
• Kamati inasikitika kuwa kauli ya waziri wa afya iliyotolewa bungeni ilijaa upotoshaji mkubwa kwa jamii na wabunge na kwa kuwa busara za naibu spika zilitoa ufafanuzi kuwa kauli hiyo ni ya upande mmoja na wangependa kusikia kutoka kwa madaktari lakini kanuni haziruhusu,kamati imeona kuwa ni muhimu kufafanua baadhi ya masuala yaliyopotoshwa na ambayo hayajatolewa ufafanuzi wowote;
1. Si kweli kuwa huduma zinaendelea kama kawaida katika hospitali tajwa,kwa mfano KCMC taarifa za jana zinaonyesha kuwa hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kusitisha huduma zote kasoro huduma ya magonjwa ya ngozi ,hali hiyo ililazimu Askofu mkuu wa KKKT kufika hospitalini hapo kuwasihi madaktari,jambo ambalo lilishindwa kutatua tatizo. Propaganda za waziri ni msiba mkubwa kwa taifa.
2. Si kweli kuwa madaktari bingwa walikataa kwenda mikoani,taarifa ya kweli ni kuwa taratibu hazikufuatwa kabisa,badala yake kejeli na ubabe ulitumika huku madaktari bingwa wengi kati yao wakihamishwa kupitia magazetini. Mfano upo wa madaktari ambao walienda kuripoti mikoani wakasumbuliwa na kuzungushwa kupewa masurufu ya safari,hospitali ya mkoa ikimuelekeza kuwa jukumu hilo ni la wizara na wakati huo huo wakienda wizarani wanaambiwa jukumu hilo ni la mikoa.
3. Mojawapo ya madai ya madaktari ni suala la uboreshaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira ya kazi, waziri amelikwepa na kupoteza muda wa wananchi kuzungumzia propaganda zisizo na tija.
4. Suala la bima ya afya kwa watumishi wa afya hajatolea tamko lolote.
5. Suala la uwajibishwaji wa watendaji wa wizara ya afya akiwemo yeye, amelikwepa kabisa.
6. Serikali inazungumzia na kutoa ahadi siku zote bungeni kuwa inapeleka watumishi wa afya wilayani na vijijini lakini Mh Waziri akifahamu kuwa dai mojawapo la madaktari ni kuomba serikali iingize posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa afya wanaopelekwa maeneo ya mazingira magumu mojawapo ikiwa mikoa ya pembezoni mfano ni Rukwa anapotokea waziri mkuu, hili hajalitolea tamko wala kulizungumzia kabisa.
7. Bw Waziri ametumia muda mrefu kupiga propaganda za mshahara badala ya kusema wao wanatoa ofa gani ili tuelekee kwenye meza ya mazungumzo.

• Mwisho kabisa , jumuiya ya madaktari inaona kuwa serikali haina nia ya dhati kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.
 
bado serikali inatumia mbinu ile ile iliyoshindwa kutatua mgogoro huu.kudanganya,vitisho na dhihaka.
 
Mbona hiyo taarifa sio ya ma Dr bingwa ,
Nahisi either mtoa mada amejichanganya kwa kusema Ma DR bingwa ,
Au kuna taarifa zaidi inabidi tuitafute kuhusu ma Dr bingwa
 
Mbona hiyo taarifa sio ya ma Dr bingwa ,
Nahisi either mtoa mada amejichanganya kwa kusema Ma DR bingwa ,
Au kuna taarifa zaidi inabidi tuitafute kuhusu ma Dr bingwa
madaktari bingwa ni sehemu ya jumuia ya madaktari tanzania.hii ni taarifa ya kamati kwa niaba ya jumuiya hiyo.sasa wakati umefika kwa madaktari bingwa kuingia kwenye mgomo.hata vita vya uganda vilianza na mgambo na baadae wanajeshi.
 
Steven Ulimboka has gathered sufficient media attention over the past two weeks enough for him to contest any political position. The guy has shwredly exploited the doctors' strike to magnify his popularity and he can not ask for more.

You are wrong on this one. The government through the PM has made him a more popular and respected national figure.
 
Hii nchi hata mwendawazimu anaweza akaongoza, mwacheni Mpona aendelee mapinduzi hayataletwa na kizazi hiki labda kizazi cha under 10, wote tunapiga kelele tu humu ndani, Mponda anaongea hivyo anatoka bungeni na leo anaweza kwenda popote na si tunamchungulia tu na kuchekacheka, wakati ilitakiwa hata kumtemeA MATE. Hapa naanza kuona uwezo wa akili wa Ma dr. kweli PCB zao wanaanza kuzitumia
 
madaktari bingwa ni sehemu ya jumuia ya madaktari tanzania.hii ni taarifa ya kamati kwa niaba ya jumuiya hiyo.sasa wakati umefika kwa madaktari bingwa kuingia kwenye mgomo.hata vita vya uganda vilianza na mgambo na baadae wanajeshi.
Lakini katika hayo maadhimio yao mapya hakuna sehemu inayozungumzia mgomo wa ma Dr bingwa ?
Mwenye taarifa zaidi atujuze plz ...
 
Kuna mod mmoja hivi mjingamjinga.
ni kweli na siyo mod mmoja tu...inabidi ianzishwe rumande na mahakama ya jf ili mtu apate nafasi yakujitetea
kabla ya kula ban...tunawazodoa bure viongozi wetu kwa kutumia mabavu wakati sisi wenyewe tuko hivyohivyo tukipewa mamlaka hata kidogo tu...!
 
Tanganyika , Tanganyika yangu nakupenda sana , ila kwa hali hii inavyo endelea , harufu kali ya damu inanukia, mzaha mzaha huzaa usaha ! wengi wetu tulikuwa mabingwa wa kuimiliki kalashnikov , na kwenye Range tulifika mpaka kwenye Tano bora ya kikosi, sasa naona wakati unasogea watu kukumbushwa ....... sitaki kuwazia . !
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom