Madai ya Zitto kukutana na Balozi wa Uingereza; Msajili wa Vyama vya Siasa awaandikia barua ACT-Wazalendo akitaka wajieleze

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Baada ya Gazeti la Jamvi la Habari kuandika habari iliyodai Zitto alikutana na Balozi wa Uingereza nyumbani kwa Balozi huyo,kuna barua mitandaoni(twitter) inayodaiwa kuwa ni ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akiwaandikia barua ACT-Wazalendo akitaka wajieleze.

Kulingana na barua hiyo,Msajili anataka kupata ukweli wa madai hayo yaliyoandikwa na vyombo vya habari.

Tweet yenye barua hiyo(barua ya tarehe 12/06/2020) imekuwa retweeted na baadhi ya watu akiwemo Zitto mwenyewe.

Zitto.jpg
 
Sasa mwandishi alijuaje mazungumzo yao yalihusu kusaidia uchaguzi wakati hakuwepo ?
 
Hilo jina tu la Msajili halimfai anatakiwa kuitwa kuwadi wa cccm. Hata aibu haoni yani badala kumwandikia Musiba aje atoe uthibitisho yeye anawaandikia walikaa kikao? Hivi gazeti la Musiba ni kusomwa kweli?Nimeshitushwa na mtu kama Msajili kusoma gazeti la Musiba. Shukuru sana ningekuwa ni magufuli ningekufukuza kazi usiku huu huu jinga kbs
 
CCM hawana akili kabisa, yaani Zitto kukutana na balozi ni kosa kisheria?
bure kbs hawa...hebu imagine huyo balozi ni demu na ana mahusiano ya karibu na Zito, sasa hapa si tutasema msajili wa vyama vya siasa anamuonea wivu wa KIMAPENZI Zito?!.

yanakurupuka hovyo kutaka kumfurahisha mkuu wao ambaye naye kimsingi ndicho anachotaka...basi angalau watende kwa weledi japo kdg.

ni kama wale police wa dodoma na utunzi wao juu ya kushambuliwa kwa Mbowe
 
Msajili anapoteza muda tu
Kwa kufanya hivi anazidi kuwatia hasira waingereza na washirika wake na hivyo kuudiscredit uchaguzi.
Zitto kwenda kwa balozi siyo tatizo maana kuwa balozi haimaanishi huna haki ya kufanya urafiki na watu locally
 
Hawa jamaa zangu hawajiamini kabisa, siku hizi Zitto akikutana na mzungu tu, hata akiwa mtalii pressure tupu!.

Wacheni dhambi muishi kwa amani.
 
Zitto alienda ubalozini Kama yeye au kama chama?ni haramu kwa mtu au chama kuomba mwaliko au kualikwa na balozi?serikali awamu ya tano acheni uoga October 2020 mtarudi kwa kuwa miaka mitano yote mmefanya mikutano ya
hadhara nyie wenyewe na kila Chombo cha habari kinawasifia na kuonesha habari zenu pekee
 
Acheni uzushi, mh zitt anashutumiwa kutafuta msaada wa kifedha kwa ambassador ambap ni kinyume na sheria za uchaguzi.
 
Back
Top Bottom