Madai ya wizi wa kura na kisa cha mashetani/majini

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,182
Wanabodi poleni na mihangaiko ya kila siku na hongeleni kwa ushindi wa Bidden. Leo ningependa niwaletee kisa cha mapepo ninachokifananisha na madai ya wizi wa kura.

Mwaka 2002 kulikua na mdada ambae alikua na mapepo mtaani tuliyaita mashetani. Kila siku jioni baada ya chakula cha usiku badala ya taarifa za habari na mambo mengine sisi tulikua tunaenda kupata burudani huko.

Yaani walikua wanaandaa ubani yeye anafunikwa na kuvukizwa (kupigwa nyungu) ili kumpandisha mashetani. Mashetani yakipanda yakiume alikua makorofi sana lakini yakike tuliimba na kucheza pamoja nayo.

Kuna siku moja kiti sijui alifanya upuuzi gani na aliyefanya nae huo upuuzi alikuwepo kwenye mduara wakati tukisubiri yapande. Sasa yalipopanda alikua ni jini wa kiume na aliunguruma kwa sauti nzito na kudai kuwa amekuja kwa kazi moja tu kutoa adhabu kwa kiti na huyo jamaa.

Kwakua hatukujua kua limefanyika kosa gani na nani kafanya. Sasa kwakua wengi tulikua karibu na huyo kiti, tulikaa attention kwa lolote. Baada ya muda kidogo kuna jamaa aliyekua kwenye mduara alitandikwa bonge la fimbo. Sasa ile sauti ya fimbo tukajua majini yamekuja mengi kutoa adhabu, tukaanza kukimbia hovyo kila mmoja na njia yake.

Kesho yake stori ikawa ni nguvu ya majini katika kisa kilichopita. Stori zikawa nyingi kwamba majini huwa yanaitana na ndio maana Jana yake kila mtu alikua na jini linalomfukuza. Kila mtu alitoa ushuhuda kuwa alifukuzwa na jini. Swali likawa jini yupoje.

Katika kutoa ufafanuzi wa kila mmoja ikaja kufahamika kuwa hakuna cha jini aliyefukuza mtu wala nini. Maana kiti miguu haikufanya kazi na kifua kilibanwa baada tu ya jini kutoka. Hata tuliokuwa tunakimbia tulikua tunakimbiana wenyewe kwa wenyewe na aliyepiga fimbo ni binadamu sio jini.

Baada ya kubaini hayo tukajiridhisha kuwa jini tulimuumba wenyewe na vurugu zote zilijengwa na akili zetu tu na hakukuwa na uhalisia.

MADAI YA WIZI WA KURA
Mwaka huu kulikua na uchaguzi ambao umeisha kwa kila chama kupata matokeo yake. Uzuri ni kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo kiliweka mawakala sehemu kubwa nchini. Mchakato mzima ulishuhudiwa na mawakala hao na fomu za matokeo wanazo.

Sasa baada ya kushindwa zimekuja stori za wizi wa kura. Lakini kama stori ya majini tu hakuna mwenye uhakika na jambo husika. Kila mtu ukimuuliza imetokea wapi? Anajibu sehemu nyingi tu nchini, majina hataji au hatà jina la mtaa tu.

Kuna walioenda mbali zaidi na kudai kuyashika masanduku ya kupigia kura lakini ukiwauliza yako wapi? Hawajui au wanakuambia wamechoma! Yaani ushahidi mkubwa kama huo unachoma ili iweje? Kwa jinsi jamaa wanavyopenda kuonekana wangeyapata kweli wangechoma?

Aliyepigwa fimbo anajua amepigwa na nani lakini wengine wanakimbia kimbia tu bila kujua wanakimbia nini. Yaani wanachojua kura zimeibwa, lakini ukiuliza *Zimeibwa wapi?, Kituo gani? Kura ngapi? Walioiba wako wapi? Hatà wao hawajui.

Aliyeibiwa alete ushahidi wa maandishi ili tumalize mgogoro. Chadema kwakua wana nakala za matokeo nchi nzima wajumlishe wao wenyewe au ikiwezekana watuletee vituo vilivyoibwa kura maana kila kituo ilikua ni watu chini ya 450. Mbona kwenye serikali za mitaa walionesha mpaka majina ya wenyeviti wa mitaa waliokatwa na makosa waliyofanya. Hapa wanakwama wapi?

Halafu yule aliyepigwa fimbo amejitoa kwenye zikiri eti ametishiwa maisha! Nani akutishie maisha wewe leo huna cheo chochote hatà cha ubalozi wa nyumba kumi?

Serikali toeni ajira za ualimu bhana nikafundishe shuleni mada ya How CHADEMA failed to organize protests in Tanzania.
 
Mabadiliko yako tumeyaona. Hatukushangai
IMG_20200831_022721.jpg
 
Baada ya uchguzi CCM inaendelea kuwa chama cha siasa chenye muundo wenye kueleweka kuanzia juu mpaka chini.

Chama kinaendelea kufanya vikao kama kawaida, kinaendelea kuchagua wenyeviti wa wilaya na mikoa kama kawaida.

Vyama vingi vinakuwepo wakati wa uchaguzi tu, ukimalizika vinapotea na kusubiri msimu mwingine wa uchaguzi.

Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubaliana na porojo za wizi wa kura, utamuibia vipi kura Zitto Kabwe wakati muda wote anapinga hata yale masuala ya muhimu ya kimaendeleo?.

Utamuibia vipi kura mtu anayezipinga ndege wakati anazitumia kwenda kwao Kigoma?. Umuibie kura ili iweje?.

Kaka wa Hai siku zote ni mwendo wa siasa za kutafuta ugomvi, watu wa Hai mwaka huu wamekataa kutumika kama mtaji wa kura zenye kuyasaidia maisha yake binafsi.
 
Baada ya uchguzi CCM inaendelea kuwa chama cha siasa chenye muundo wenye kueleweka kuanzia juu mpaka chini.

Chama kinaendelea kufanya vikao kama kawaida, kinaendelea kuchagua wenyeviti wa wilaya na mikoa kama kawaida.

Vyama vingi vinakuwepo wakati wa uchaguzi tu, ukimalizika vinapotea na kusubiri msimu mwingine wa uchaguzi.

Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubaliana na porojo za wizi wa kura, utamuibia vipi kura Zitto Kabwe wakati muda wote anapinga hata yale masuala ya muhimu ya kimaendeleo?.

Utamuibia vipi kura mtu anayezipinga ndege wakati anazitumia kwenda kwao Kigoma?. Umuibie kura ili iweje?.

Kaka wa Hai siku zote ni mwendo wa siasa za kutafuta ugomvi, watu wa Hai mwaka huu wamekataa kutumika kama mtaji wa kura zenye kuyasaidia maisha yake binafsi.
Haipendezi kumuuliza mtu mzima "jee una akili timamu?" Lakini kama nikufahamuvyo hapa JF, kuandika haya uliyoandika wakati hali halisi inajulikana hata kwa mtoto mdogo najisikia kukuuliza swali hilo.
 
Haipendezi kumuuliza mtu mzima "jee una akili timamu?" Lakini kama nikufahamuvyo hapa JF, kuandika haya uliyoandika wakati hali halisi inajulikana hata kwa mtoto mdogo najisikia kukuuliza swali hilo.
Niulize swali lolote lakini uhalisia wa mambo ni kwamba upinzani ni lazima uje na mikakati mipya.

Uje na mtazamo chanya wenye kuongozwa na substance badala ya hali iliyozoeleka.
 
Why was it so important for this government to go back to one party system??? And then in the end what made them realize that democracy demands that some Bunge Committees must be under opposition otherwise gov support from donors will not forthcoming! Then instead of begotiating like Zanzibar did within katiba law, with Chadema that had the right to send in viti maalumu they are continuing to break the katiba by endorsing speaker’s wabunge maalumu who do not belong to any party. Something that is against the national Constitution!! What examples are we setting for our young leaders??? That a country is run without the rule of law??? Whatbis the meanng of kiapo? Is it just a joke???
I suggest that ccm negotiates with Chadema just as Mwinyi did in Zanzibar for ccm to gain some aota of respect!!
 
Back
Top Bottom