Madai ya wanawake waliotelekezwa yanatuambia nini?

Naliangalia jambo hili kwa angle ingine, nikiwa na maana mwanaume anaweza kuwa na uwezo wa kawaida wa kutuna mtoto kwa mfano 100,000 kwa mwezi au 75,000 kwa mwezi....ila sasa huyu mama/mzazi mwezio akaona huo upenyo yeye akaacha kujishughulisha na kutafuta pesa zake mweyewe ile ya baba kwenda kwa mtoto ikawa ndio mshahara wake...

Na kujikuta hazitoshi tena kwa yeye na mtoto hapo sasa ndio balaa linapo anzia....pili...wamama kulea kwa kiwango cha juu kuliko kipato anacho pata hata kupelekea kuona hela ya malezi haitoshi.....kupelekea usumbufu kwa baba wa mtoto na baba wa mtoto akaona hata hicho kidogo anachopeleka kama hakina matumizi sahihi anakata kamba si kwa kupenda ila kwa kulazimika.

Mfano : Pahala flan bwana mmoja alikuwa ni driver tax na dada mmoja alikuwa muuza uji jioni ni kashata....mambo yakaenda bwana akapenda dada yule, mara akapata ujauzito...miezi sita ya kwanza dada huyu alikuwa akiendelea na biashara yake, miezi mitatu ya mwisho akapumzika ili kusubiri ujio wa mtoto...wakati wote huu bwana huyu alikuwa bega kwa bega mpaka ujio wa mtoto.....balaaa likaanza mwaka mmoja baada ya mtoto kuzaliwa na binti huyu kutotaka kurudi kwenye kazi yake ya awali kwa sababu analea na mzigo mzima akamwelekezea kijana huyu....na usumbufu mkuu ustawi wa jamii kuwa matumizi hayatoshi kila mwezi......mpaka naandika hapa bwana ilibidi aache kazi eneo lile mwanamke anapo lifahamu na kutokokea kusiko julikana na mama yule karudia kazi yake ya awali.

Wasalaam.
 
Back
Top Bottom