Madai ya walimu waliokosa ajira yatua OWM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya walimu waliokosa ajira yatua OWM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 26, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Madai ya walimu waliokosa ajira yatua OWM


  Na Benjamin Masese

  HATIMAYE sakata la baadhi ya walimu waliohitimu mafunzo yao ya ualimu mwaka 2009/2010 na kushindwa kuajiriwa limetinga katika Ofisi za Waziri Mkuu (OWM) na

  kuungwa mkono kwamba wana hoja za msingi za haki ya kuajiriwa.

  Tofauti na juzi ambapo walimu hao walitinga ghafla katika ofisi za Waziri Mkuu kwa maandamano baada ya kushindwa kupata majibu mazuri kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Hamisi Dihenga, ambapo walikumbana na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) getini na kuwataka kufuata utaratibu wa kuonana na viongozi husika, jana walipata mapokezi mazuri na maelezo ya kutia matumaini.


  Hata hivyo, jana walimu hao walipokewa na Katibu wa Waziri Mkuu na msaidizi wake baada ya kutimiza taratibu zote zilizotakiwa ambapo walifanya kikao cha pamoja kwa saa kadhaa kusikiliza madai yao na hatua zilichokuliwa na wizara husika.


  Viongozi hao walisema kuwa kwa mujibu wa maelezo ya walimu hao, kama kweli hawakusema uongo au kuchanganya mada, wanatakiwa kuajiriwa kulingana na mikataba na miongozo kutoka vyuoni walikosomea.


  Walisema kuwa kutokana na madai hayo kuwa na mlolongo mrefu wa maelezo, watahitaji kutafuta ukweli katika upande wa pili wa wizara, ili kujua utaratibu uliopo wa kutoa ajira kwa mwaka huu na kuahidi kutoa jibu kamili kesho.


  Hata hivyo viongozi hao waliwataka walimu hao kuwapa hoja zao za msingi kimaandishi zitakazowasaidia watakapokutana na upande wa wizara ambapo walimu waliandika na kuwakabidhi muda huo.


  Akizungumza na Majira, Msemaji wa walimu hao, Bw. Bakari Achimwale kutoka chuo cha walimu Shinyanga, alisema kuwa ameeleza ukweli wa mambo yalivyo pamoja na majibu waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa wizara ya elimu tangu wiki iliyopita hadi juzi walipopata majibu yasiyoridhisha na kuwakatisha tamaa.


  Alisema wao kama walimu halali waliosoma vyuo vinavyotambulia, hawatakubali kupoteza ajira yao kutokana na uamuzi mbovu uliotolewa na Wizara ya Utumishi kuajiri walimu 9,226 na kuacha wengine wenye vigezo kwa kisingizio cha kufeli somo moja.


  Alisema utaratibu huo wa kuajiri walimu waliofaulu masomo yote ni mgeni kwao, na katika mikataba ya chuo hawajawahi kuusikia.


  Juzi Bw. Dihenga alitoa tamko kwamba wizara haina mpango wowowte wa kuajiri walimu wengine huku akisisitiza kwamba lazima walimu waliofeli kujisajili upya kwa lengo la kurudia mtihani wao kabla ya Mei mwaka huu ili kuangaliwa upya.


  Alisema kuwa kulingana na maagizo kutoka wizara ya utumishi ya kutoajiri tena walimu, aliwataka walimu hao kulipia fedha zao Baraza la mitihani la taifa (NECTA) kurudia mtihani na si vinginevyo.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  serikali ya JK imevuna sifa ya kuwa ni ya zima moto tu...............
   
Loading...