Madai ya TRA kukamata akaunti za Benki na hata kuchukua kilichomo, Serikali iangalie tena, huenda hiyo Mamlaka ikatumika vibaya

East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,812
6,036
Serikali hii nguvu ambayo mmeipatia TRA kuwa na uwezo wa kushirikia account za bank za wateja (wafanya biashara) na hata kuchukua pesa, muingalie, huenda hiyo nguvu (Authority) wanaitumia vibaya. Kama mnawapenda wafanya biashara na mnapenda waendelee mtawalinda 🌽🌽🌽

#Uzi tayari
#maendeleo haya chama
 
Labda ungeeleza chanzo,
Kwa mujibu ya Sheria za Kodi na za benki,kamishna ana nguvu kisheria ya kutwaa akaunti za mlipa Kodi lakini hapo no baada ya kujiridhisha umekwepa Kodi na hutoi ushirikiano.
Tra hawaamki tu na kwenda kufunga akaunti
 
Walipitia mahakamani na wanayonguvu
Serikali hii nguvu ambayo mmeipatia TRA kuwa na uwezo wa kushirikia account za bank za wateja ( wafanya biashara ) na hata kuchukua pesa, muingalie, huenda hiyo nguvu ( authority ) wanaitumia vibaya. Kama mnawapenda wafanya biashara na mnapenda waendelee mtawalinda

#Uzi tayari
#maendeleo haya chama
 
Labda ungeeleza chanzo
Kwa mujibu ya Sheria za Kodi na za benki,kamishna ana nguvu kisheria ya kutwaa akaunti za mlipa Kodi lakini hapo no baada ya kujiridhisha umekwepa Kodi na hutoi ushirikiano.
Tra hawaamki tu na kwenda kufunga akaunti
Ni kweli. Unachosema, ila kuna uhusiano flani baina ya TRA na mlipa kodi ( Meza ya majadiriano ) haina urafiki sana japo sio kwa ofisa wote na wafanya biashara. Na ndipo balaa linaanzia hapo
 
Ni kweli. Unachosema, ila kuna uhusiano flani baina ya TRA na mlipa kodi ( Meza ya majadiriano ) haina urafiki sana japo sio kwa ofisa wote na wafanya biashara. Na ndipo balaa linaanzia hapo
Watu tu hawajui Sheriasheria inaruhusu rufaa kwa kamishna ukihisi umpigwa Kodi kimakosa,kamishna anao uwezo wa kurekebisha au kukupa ahueni,Kama hukuridhika unatakiwa kwenda baraza la Kodi kuishitaki TRA
 
Unafikiri wafanya biashara hawajui haya ? TRA wana ubabe flani wa kiuonevu. Ukianzisha vita ya kisheria nao na mmoja utafunga biashara, ni kama Trafick vimba useme gari yako haina kosa.. watachokonoa hadi wakupe mkeka

Huyu mtu ameelezea kitu flani, japo haki husiani sana na thread yangu ila ilikuwa inalekea kufanana
 
Naamini kabisa kuna baazi ya ofisa wa TRA , wanafanya kazi vizuri sana na kwa uadirifu wa hali ya juu. Na katika maeneo wanayo ongoza wafanya biashara wa maeneo hayo wana furaha na wana endelea ila kuna maeneo , aah! Kufanya biashara imekuwa jehamu ya moto
 
Back
Top Bottom