Madai ya sh 23,887,000 ya wafanyakazi wa kampuni inayotoa huduma ya chakula hospitali ya Mloganzila

Labia Mapunda

Member
Dec 4, 2021
13
6
Kuna wafanyakazi wanadai mishahara yao katika kampuni inayotoa huduma ya chakula hospitali ya Mloganzila shilingi 23,887,000.00 na uongozi wa hospita umeombwa msaada mara kadhaa lakini hawajatoa ushirikiano wowote na kitendo hichi kinaichafua hospitali hii kwasababu ni ya Serikali na mzabuni wanapaswa kumsimamia ili alipe wafanyakazi mishahara yao.

Hivyo tunaomba wizara ya Afya na Waziri husika aweze kusaidia kutatua hili tatizo kwasababu taarifa anayo juu ya hili suala na wana jamii foram tunaomba mtusemee hili suala liweze kupatiwa ufumbuzi na limufikie mh Rais aone jinsi watu aliowateuwa wanavyoshindwa kutatua shida za wananchi wake asanteni sana.

IMG_20211126_195737.jpg
 
Mpaka kufikia hapo ninaridhaa na wamefuata taratibu zote lakini wamekosa msaada ndio maana tunatakiwa kupaza sauti wapate haki zao maana mzabuni anasema anaidai hospitali jambo ambalo wafanyakazi haliwahusu
 
Kabisa kaka yaani inahuzunisha sana watu wamefanyishwa kazi tena kwenye sector ya serikali na wanaanza tena kuteseka bila kulipwa inauma sana
 
Hospitali inapaswa kumsimamia huyu mzabuni ili wafanyakazi wapate haki zao lakini imeshindwa kufanya hivyo
 
Kwasababu haina usiri na ndiomaana hata jina la kampuni pia sijaficha kwasababu linatakiwa likemewe hili suala ili wafanyakazi wapate haki zao
 
Mkataba kati ya hospital na mzabuni unasemaje?kuna kipengele kinachosema hospital imsimamie mzabuni kuhakikisha analipa mishahara ya wafanyakazi wake?
 
Hata kama mkataba haupo hivyo lakini mzabuni tayari anawaambia wafanyakazi kuwa yeye hajalipwa na hospitali na ndomaana nasema hospitali inawigo Moana sana wakuweza kuwasaidia hata kuwasemea tu sio kuwalipa
 
Kupaza Sauti Jamii forums sio pahala sahihi Kwanini Hamjafungua Kesi katika Kesi hiyo mdai pia Na pesa za ziada za Usumbufu na Mengineyo wajua wafanyakazi Uoga wenu unawaponza sana Na Wale Tucta ni Sifuri Jumlisha na Sifuri unapata Sifuri....
 
Bado wanaendelea na kazi (ni wafanyakazi kwa sasa) au mikataba ya ajira ilifika ukomo?
 
Bado wanaendelea na kazi (ni wafanyakazi kwa sasa) au mikataba ya ajira ilifika ukomo?
Mkataba haujafika mwisho lakini mwajiri na hospitali wanakamgogoro kuhusu malipo mzabuni anasema anaidai hospitali nao wanasema kuwa wanamdai mzabuni kwahiyo wafanyakazi Sasa hivi wapo tu wanaenda kazini na wengine wamejishikiza kwa mzabuni wa mda ambae anatoa huduma Sasa hivi kitendo kinachowaumiza sana wafanyakazi kwasababu hawajui hatma yao
 
Back
Top Bottom