Madai ya Serikali kufilisika na yanayoendelea ndani ya Wizara ya Fedha!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Wakati Serikali ikidaiwa kushindwa kuwalipa watumishi wake mshahara wa mwezi Januari 2014 mpaka sasa, kuna tetesi kuwa Waziri wa Fedha aliyeteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni Mhe. Saada Mkuya amewaandalia wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti ya Bunge pamoja na maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha safari ya kufanya 'utalii' kwenye nchi za Sweden ama Norway kwa muda wa siku zaidi ya kumi kama njia ya kujipongeza na kuwaweka sawa wabunge hao kwa bajeti atakayoiwasilisha katikati ya mwaka huu. Safari hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 02 - 12 Februari, 2014.

Safari hiyo iliyobatizwa 'Study Tour' kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye mambo ya bajeti na ukusanyaji wa mapato itajumuisha ujumbe wa watu zaidi ya thelathini ambao watagharamiwa kila kitu na Wizara ya Fedha ama Hazina jambo linaloonekana kuwa ni staili nyingine ya kutoa takrima kwa wabunge ili wapitishe bajeti za wizara husika bila mikingamo mingi baada ya staili aliyotumia aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo Bw. Jairo kugundulika hali iliyosabisha kupoteza nafasi yake.

Jambo la kujiuliza ni kuwa; inakuwaje Serikali inalalama kila siku kuwa haina fedha jambo linalopelekea kushindwa kulipa hata mishahara ya watumishi wake kwa wakati lakini inakuwa na uwezo wa kugharamia safari zisizokuwa na tija kwa taifa na ambazo zinagharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi?

(Nusanusa yetu imepata viambatanishi kadhaa kama uthibitisho wa kinachojiri ndani ya Wizara ya Fedha katika suala hilo ikiwemo barua na orodha ya wanaotakiwa kusafiri pasipo kujumuisha maofisa wengine ambao wako kwenye level ya chini)

page1.jpg

page4.jpg

page2.jpg

page3.jpg
 
Kila siku viongozi wetu wanalia serikali haina uwezo huku tunaendekeza ujinga wa kupitiliza.Hivi kama umeandaa bajeti yenye malengo mema kwa Watanzania kwanini utumia nguvu kubwa kuipitisha?

Huyu Waziri aache mchezo huku mtaani hali ni mbaya na ni majuzi tu wametubandika mzigo wa umeme kutokana na uzembe wao alafu wanakwenda kwenye upuuzi tour??????????

Sawa sisi ni vipofu lakini sasa mmejisahau mnatushika hadi mikono!!!!
 
Naomba waungwana mfanye juu chini post hii ianze kutembea kwenye mitandao mingine mi nawatumia rafiki zangu wote kwenye facebook. Pia kwa email hata kwenye jumbe za simu tuwaambie watu. Mi sijapata mshahara mpaka leo natakiwa kwenda likizo hakuna hela hivi serikali hii imelogwa na nani? Ghaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!! Hasira sana.
 
haingii akilini hii kabisa.kuna kazi zimesimama kisa ukosefu wa pesa.leo hii hazina inagharamii safari zisizo kuwa na tija yoyote huku hiyo hiyo hazina ikishindwa kulipa mishahara.imeshindwa kulipa wakandarasi wa ujenzi wa barabara mpaka kufikia kampuni moja ya kichina kudai zaidi ya US$ 400 m. nafikiri kilio cha Mathayo David kilikuwa sahihi kabisa.
 
Inasikitisha sana serikali kushindwa kulipa wafanyakazi wake kwa wakati na mambo mengine ya msingi kisha inaendekeza ujinga kama huu ambao hauna tija kwa taifa.
 
Tatizo kubwa ambalo tunalo ni Kuitaka Pepo lakini kufa hatutaki!
 
Kweli hawa CCM ni kama jino lililooza na linalokukosesha usingizi na ili usiku ufuatao uweze kulala vizuri basi dawa ni kuling'oa na kulitupilia mbali , kitendo hicho ndio kinatakiwa kifanyike 2015 na si vinginevyo la sivyo wataendelea kutugeuza geuza kama samaki
 
jamani eeee ! Bila kuondoa ccm hii nchi itakamuliwa hadi tone la mwisho la damu , baada ya mwigulu na malima kuchanganywa na huyo dada , nilijua lazima kitokee kitu very soon .
 
Back
Top Bottom