Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Nilistushwa na mabadiliko ya msimamo wa waendesha mashitaka, ambao ni Polisi katika kesi ya Kabendera hapo jana.
Nimewasikia waendesha mashitaka hao wakieleza kuwa upande wa mashitaka hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo na hivyo wamekubali kuwa mazungumzo ya upande wa mashitaka na mtuhumiwa yafanyike ili mtuhumiwa aachiwe huru!
Nimejiuliza hivi hatua hii imefikiwa baada ya Rais Magufuli kutoa kauli kali siku chache zilizopita akiwatuhumu Polisi hao kuwa wanaowabambikia kesi za uhujumi uchumi na utakatishaji pesa ili watuhumiwa hao waendelee kusota magerezani kwa lengo la kuwakomoa watuhumiwa hao?
Rais aliendelea kufunguka kwa kusema kuwa walaaniwe waendesha mashitaka hao ambao wanawabambikia kesi watuhumiwa hao kwa lengo tu la kuwakomoa ili wakae magerezani kwa kipindi kirefu sana.
Nimejiuliza hivi hii kesi ya Kabendera si imefikishwa mahakamani hapo zaidi ya miezi 6 iliyopita, na wakati wote huo waendesha mashitaka hao wamekuwa wakiendelea "kukomaa" kuwa ushahidi hawajaukamilisha?
Sasa iweje hivi sasa, baada ya kumsotesha Kabendera zaidi ya miezi 6 jela, ndiyo hao waendesha mashitaka waone hakuna haja ya kuendelea na kesi hiyo?
Hao waendesha mashitaka, ambao ni Polisi si wamekuwa wakidai, katika kipindi chote hiko cha miezi 6 kila kesi inapoenda kutajwa mahakamani, wanaomba kesi iahirishwe kwa madai kuwa ushahidi haujakamilika?
Kama ni hayo majadiliano kati ya mtuhumiwa na upande wa mashitaka, si huyo Kabendera alishayafanya zaidi ya miezi 4 iliyopita na akaeleza kuwa yeye hana hatia kwa makosa hayo wanayomtuhumu nayo hapo mahakamani?
Kama alivyosema Mheshimiwa Rais na Mimi niunge mkono kuwa walaaniwe waendesha mashitaka wote ambao ni Polisi, kwa kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji pesa kwa watuhumiwa na hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa mtuhumiwa kukaa gerezani kwa kipindi kirefu sana.
Ningependekeza kwa hao Polisi wenye tabia hiyo, ili na wao waweze kuona hayo matendo wanayoowafanyia Watanzania wenzao kuwa siyo mazuri, mahakama iweze "kuwageuzia kibao" na wao waweze kukaa magerezani kwa kipindi kirefu sana.
Kama hayo ni "maigizo" anayotufanyia Jiwe na yeye ndiye anayewaagiza hao Polisi wafanye unyama huo na yeye anawaruka hivi sasa, basi laana hiyo imgeukie yeye mwenyewe