Madai ya pesa za radar:MAHOJIANO YA NAIBU SPIKA Job Ndungai NCHI YETU HAIKO SERIOUS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya pesa za radar:MAHOJIANO YA NAIBU SPIKA Job Ndungai NCHI YETU HAIKO SERIOUS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Jun 25, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya wiki moja tumekua tukifuatilia swala la kurudishiwa pesa yetu ya radar kutokana na rushwa kwa viongozi wetu niseme RUSHWA kwa kua serekali yetu inaonekana bado haitaki kukubali kwamba pesa hiyo ilikua ni rushwa na sasa wameipatia jina jipya "NCHENJI"

  Sikiliza mahojihano ya BBC na Naibu Spika Job Ndungai inaonyesha ni vipi viongozi wa Serikali na CCM wasivyo serious.Ni vipi utume ujumbe ambao haujui sakata hilo la radar kwa upande wa Tanzania liko katika hatua ipi? Kisheria, kisiasa, kimaadili n.k.AIBU

  BBC Swahili - Habari - Tanzania bado yadai fedha zake
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Sisis watanzania ni wajinga sana. Kutokana na ujinga wetu ndiyo maana tunaongozwa na watu wajinga namna hii. Kwa hiyo tutaendelea kurudi nyuma kimaendelea hadi pale tutakapoamka. naibu Spika wa bunge letu anayekwakilisha nchi leo huko ni kipunga kabisa, hajui lolote bali anapiga bla bla tu.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Ndugai hajawahi kuwa na akili! Lkn ndio nchi yetu hii ilivyo, wajinga ndio wanakuwa viongozi siku hizi.
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ndugai licha kuwa hajui anachoongea licha ya kushindwa kukumbuka kuwa PCCB ilishawasafisha wahusika na hakuna uchunguzi wowote unaondelea juu ya hilo na pia kuhusu wahusika wa sakata la Radar huyu bwana anaonekana ni kama mwongo au mnafiki kuhusu wahusika kwa sababu wahusika wote wanajulikana akiwemo CHENGE na mpaka ikabidi ajiuzuru ina maana hata ili ndugai halijui. wahusika wanapaswa kuona aibu ndiyo hatua inayochukuliwa wala rushwa kwa nhci inayojifanya inafuata sheria?? mahojiano haya yamethibitisha kuwa ndugai empty head.

  huyu mtangazaji amejitahidi lakini inaelekea hakuwa na data za kutosha kwa maana angekuwa nazo angempiga ndugai km ngoma kwani
  maswali yote ameyajibu kibabaishaji kwani majibu yake yanajulikana kwa watanzania wengi
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ndungai kabanwa na kaonyesha udhaifu wa kufa mtu
  nimemkubali dada zuhura ana maswali ya msingi
  jamaa kila kitu hajui sasa kafuata nini hapo uingereza
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ndungai waliohusika wanapaswa kuona aibu kuwa kuhusika na ili suhala ,,,,,,,duh
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Perdiem..naam International Perdiems; akirudi kama atapitia Dubai anapakia gari lake moja kwenye meli sisi wengine tubaki tunalia eti bajeti ya serikali ni mbofu!!!! Nani kakwambia bajeti ni mbovu wakati wataalam wote wako serikalini?
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  SFO imefunika wahusika wa wizi kwa upambe wa uingereza , hii imetusikitisha watanzania na tumekosa nguvu. ndugai bwana

   
 9. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huyu jamaa hafukuzwe kazi hana maana kabisa

   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu pumbavu alipataje hii nafasi? au liapachikwa kiushikaji. Serikali ya tz inafanya mzaha na sana. Inashindwa kuwakamata Majamabzi kama ya kina Chenge?
   
 11. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndungai un
  aitia aibu nchi yetu kwa kuonekana bogus ugenini?
   
 12. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Job, anacheza ngoma asiyo ijua, majibu mengi aliyotoa anadai hajui! Amekwenda kufanya nini kama hajui?

  Eti wote waliohusika wanaapaswa kuona aibu, hasemi wanapaswa kuwajibishwa kwa kushtakiwa? Unafiki tu! The culture of impunity

  Job anadai SFO imewaakwamisha katika juhudi za kuwashtaki mafisadi wa TZ! Uongo mtupu! Kwanini wasiwapeleke hata hao SFO kwenye mahakama ya kimataifa walazimishwe kutoa ushahidi? Job anajua wakifanya hivyo ukweli utajulikana na wakuu wakwe watafikishwa mahakamni Chenge, Idris na wengineo... The culture of impunity! Job is a traitor!

  Job anadai ni "Hii biashara ya kimataifa", mbona sisi na Tanesco yetu tulipelekwa mhakama ya kimataifa na Dowans? Lipi limewashinda kupeleka mahakama ya kimataifa BAE? The culture of impunity!

  Job anadai SFO walifunika ushahidi ndio maana wameshindwa kuwashtaki BAe au Mafisadi wa Tanzania, unafiki pelekeni kesi mahakama za kimataifa SFO na BAE watalizimishwa kushirikiana nanyi kutoa ushahidi! This is cheap excuse for the culture of impunity and corruption!

  Job anatudanganya sisi sote, Ina maana kweli serikali ina nia ya kufanya uchunguzi, ina maana Job hajui Takukuru ilishawasafisha watuhumia na kuwapa hata clean certificate kugombea uspika! Je imeshafanya juhudi zozote kumpata middle-man wa rushwa? Au akipatikna ukweli utajulikna?

  Job anawakilisha serikali lakini hajui hata ni akina nani wlihojiwa? Kukingiana kifua unafiki tu! Job anasema, oh kesi hajiaisha, oh mara hata haijanza, oh eti kama kuna ushahidi mafisadi watashtakiwa.. hii yote indhihirisha nia ya serikali kuwaficha mafisdi wa radar!

  Job anadai fedha za fidia ambazo yeye anadai kimakosa ni zile zilizoibiwa zikirudishwa zitajenga nyumba za walimu, kununua madawati, vitabu nk> Vipi je zile dola milion aka vijisent zingerudishwa si zingeongezea nia hiyo njema ya serikali? Unafiki mtupu, fedha hizi zikirudi mikononi mwao ndio safari zitongezeka!

  Ndugu zangu watanzania a tunafanya kazi bure kupambana na rushwa kama kwanza hatutapambana na utamaduni wa kuwakingia kifua na kuwatukuza mafisadi na kutowaadhibu.

  If we do not stop the culture of impunity the fight against curruption is chasing wind! As good as useless!

  Job Ndugai anadhani anajijenga kisiasa lakini hii ni mmoja ya hasara kwa mtaji wake wa kisiasa!
   
 13. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [video=youtube_share;l-uDs6D-lQE]http://youtu.be/l-uDs6D-lQE[/video]


  tofatuti sasa wanapokuja kuulizwa mawali mepesi

  yule dada kauliza maswali ya mashiko lakini hawa jamaa wamewachekea hawa jamaa
  kimtindo kwa mfano maswali wanawauliza makavu bila dondoo

  wao wanasema kulikuwa na rushwa je aliyekula hiyo rushwa ni nani?
   
 14. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa wa Urban Pulse is simply an idiot !
   
 15. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hao Urbn Pulse ni waoga tu!
   
 16. U

  Utatu JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Pambaf - yote majizi tu haya! Anamdanganya nani, PCCB si wamesema hakuna rushwa? eti watu waone aibu. Haitoshi, majizi wasekwe lupango kwanza.
   
 17. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kunatofauti kubwa sana kati ya walivyoulizwa na ZUHURA na hii ya hawa jamaa
  viongozi wetu kama wasipokuwambia moja ya jibu ni SIJUI jua hiyo interview ilikuwa ya kuwa ogopa
  kwa sasa bongo mambo mengi serikali haina maelezo.

  wanaonegelea aibu ya taifa mara hela ya msaada inawafikia walengwa kuna anayefaidika na hela ya msaada nchi hii

  kwa kujenga hizo shule , nyumba na choo hela yote itaishia kwenye ufundi na material wana bei za ajabu ajabu tu hawa
  hata kampuni za tenda washazijua hakuna kitu hapo ni mwendo wa posho na tender board ndizo zitaimaliza hii pesa
   
 18. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  anasema waone aibu, baadaye anasema kuna uchunguzi, baadaye anasema waingereza wamefunika
  hakuna hatua hapa .
  kwanza kadanganya umma kila mtu anajua CHENGE aliojiwa na hao SFO
  kuna siri gani alishindwa kutaja chenge alijua kuna swali angepingwa kwa nini anatanua mtaani?
  hii ni dalili hakuna gamba kuvuka
   
 19. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #19
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Mahojiano na BBC kulikua na maswali,hivi kwa haya mahojiano ya hapo ubalozi kuna maswali?Picha inayoniingia kichwani inaonyesha ya kwamba walikua wamekusanyanyika hapo ubalozini kupata chai uku wakipiga soga kama ni mahojiano basi ni uhuru na mzalendo type.Hivi hao jamaa wameenda huku kuwafahamisha pesa tutazitumia vipi?!kwani ili vitu hivyo wanavyodai vitafanywa kutokana na pesa hizo wanataka kutuambia ili vitu hivyo vifanyike pesa inabidi iibiwe kwanza(Rushwa)Hizo ni porojo Waingerezaa wanachokitaka ni majibu sio soga na usanii.Serikali imechukua hatua gani kwa upande wake kuhusiana na watuhumiwa?Itafanya nini kuakikisha vitendo hivi havirudiwi?Je kunauhakika gani kwamba pesa hiyo itafika kunakokusudiwa?Je kitendo cha washukiwa kutochukuliwa hatua za kisheria na kuendelea kushikilia nafasi za uongozi katika chama na serikali na serikali yenyewe na hata ujumbe huo katika maelezo yao inaonekana hawatambui makosa yaliyotokea upande wao ata pale inapotakiwa kutamka kua ilikua rushwa wamekuja na mpya wanasema "chenji"Hii inamaanisha ya kua wizi huu ulifanyika kwa baraka za chama CCM na serikali.Kama ujumbe huo hoja unazokwenda nazo ni hizo za kujenga vyoo,nyumba za walimu,maabara n.k.Naona hata huko wanaokutana nao wanawashangaa.Tunakazi pesa nyingine imetumika kwa safari isio na tija fanyeni shopping rudini nyumbani, hata kama hizo pesa zitatolewa sio kwa jitihada au matunda ya safari yenu bali huruma ya waingereza.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wale wako matembezini tu . Wanatokwa jasho kudai eti pesa yao . Kweli wake wale wanazidi kutapanya .Masikinij Cheyo kaingia kwenye mtego kusema sema hovyo . Je wakizikosa pesa hizo watafunga mahusiano ya uballozi wa Uingereza ?Kweli wameshindwa kumtumie balozi wao nyumbani hadi wanakuja UK ?
   
Loading...