Madai ya maslahi ya madaktari wetu yashughulikiwe kwa wakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya maslahi ya madaktari wetu yashughulikiwe kwa wakati

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 17, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,619
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wameeleza kilio chao kwa serikali cha kufanya kazi katika mazingira magumu na kutaka yaboreshwe.


  Madaktari hao pamoja na wafanyakazi wengine wa hospitali hiyo, walitoa kilio hicho juzi kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, huku wakihoji sababu za kuwaongezea wabunge posho ya vikao kutoka

  Shilingi 70,000 hadi shilingi 200,000 kwa siku, na kusema kwamba wao kama Madaktari Bingwa wanaona vitendo hivyo ni udhalilishaji mkubwa wanaofanyiwa na serikali.


  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Dk. Prim Saidia, alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa wafanyakazi wa hospitali hiyo hasa Madaktari Bingwa hawakubaliani na hatua ya kuwarundikia posho wabunge huku wao wakiendelea kutaabika. Alisema kitu cha kusikitisha ni kwamba daktari ambaye amesoma na kupata shahada

  zaidi ya mbili anaendelea kupata posho ya Sh. 10,000 wakati katika ustawi wa nchi ndiye mtu muhimu na anayepaswa kuangaliwa kwa makini. Aliongeza kuwa kitendo cha kuwapa wabunge Sh. 200,000 huku madaktari na wafanyakazi wa hospitali wanalipwa kiasi kidogo na wengine hawalipwi kitu, ni kitendo cha kuwadharau.


  Alieleza kwa ujumla madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali hiyo wanafanya kazi kwa ukwasi mkubwa kutokana na wengi wao kushindwa hata kufika hospitalini kutokana na kukosa fedha za nauli.

  Malalamiko ya wataalamu wengi katika sekta ya umma wakiwemo madaktari kuhusu maslahi duni sio ya leo

  bali ni ya miaka mingi. Mara kadhaa serikali imekuwa ikiyapokea na kuahidi kuyashughulikia kadri ya uwezo wa bajeti unavyoruhusu. Wengi tunafahamu jinsi serikali yetu ilivyo na uwezo mdogo wa kifedha kuweza kuongeza maslahi kwa watumishi. Hata hivyo, pamoja na uwezoo mdogo wa serikali kimapato, bado serikali haijaonyesha nia ya dhati ya kushughulikia malalamiko ya wataalamu hao yakiwemo ya madaktari.


  Taaluma ya udaktari ni nyeti kwa maana kwamba wanataaluma hao wanahudumia watu wengi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya wakati mwingine nje ya muda wa kawaida wa kazi.


  Kutokana na hali hiyo, madaktari wanatakiwa kulipwa mshahara mzuri pamoja na marupurupu mengine ili waweze kufanya kazi zao kwa tija na ufanisi. Kwa kufanya hivyo, kungewasaidia kutekeleza majukumu yao bila kuwa na manungÂ’uniko wala tamaa ya kuiba mudawa kazi ili kwenda kufanya kazi nje ya mwajiri kwa ajili ya kuongeza kipato cha ziada.


  Hatusemi kwamba madai ya madaktari yashughulikiwe kwa kuwaongezea maslahi kwa asilimia mia moja, bali serikali iyaongeze hatua kwa hatua badala ya kutoa ahadi zisizotekelezeka. Tena ahadi hizo kutolewa wakati unapoibuka mgogoro na madaktari kulazimika kugoma. Uzoefu wetu unaonyesha kwamba migomo ya

  madaktari hususan katika Hospitali ya Muhimbili imekuwa ikiathiri wagonjwa ambao hawana hatia kutokana na kukosa huduma na wengine kupoteza maisha.


  Kwa bahati mbaya sana, hatua ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni ya kutaka kujipandishia posho ya vikao kutoka Shilingi 70,000 hadi Shilingi 200,000 kwa siku imeibua chuki miongoni mwa watumishi wa serikali na jamii kwa ujumla. Hatua hiyo inatafsriwa kuwa serikali inawajali

  wabunge kuliko watu wengine na ndiyo maana inawapandishia posho wanapozidai bila kujali hali ya uchumi.

  Hii ndiyo sababu madaktari wa Muhimbili juzi walipomweleza Dk. Nkya malalamiko yao kuhusu maslahi, walikuwa wakilaani kupandishwa kwa posho ya vikao kwa wabunge bila wao na watumishi wengine wa umma

  kuboreshewa maslahi. Ushauri wetu ni kwamba sasa umefika wakati kwa serikali kuangalia upya namna ya kushughulikia malalamiko ya watumishi wake wote badala ya kutoa ahadi wakati inapozuka migogoro ya kikazi hususan migomo na maandamano na baadaye kushindwa kuzitekeleza.


  Ili kuepusha mgogoro wa kikazi na madaktari, itakuwa vyema ikiwa madai ya maslahi ya madaktari wetu yatashughulikiwa kwa wakati na serikali. Vile vile tunawaomba madaktari nao watumie utaratibu mzuri wa mazungumzo katika kudai maslahi yao na wakumbuke kuwa suo wao pekee wanaostahili kuboreshewa mafao bali watumishi wote wa umma.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  bahati mbaya sijawa daktari mafisadi wangekoma wanapokuja kutibiwa
   
 3. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  .... Mkuu we acha tu ! Inauma ,inauma, inauma,inauma.
  ... Hasa kwa sisi tunaoishi huku kwenye mazingira magumu.
  Hata hiyo party time utaipata wapi ??! Labda kwa witchdoctor!
   
 4. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,367
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wanaotakiwa kupewa posho, pamoja na manesi, wafagiaji barabarani, wazoa uchafu, walimu, makuli bandarini, mapolisi, askari magereza, mahakimu, majaji n.k.

  NA SIO WABUNGE WETU!
   
 5. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  ... Mia kwa mia !
   
 6. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nani wa kusikia?
  nani wa kuelewa?
  nani wa kushughulikia?
   
Loading...