Madai ya korosho tandahimba polisi watumia risasi za moto.prof.lipumba aongea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya korosho tandahimba polisi watumia risasi za moto.prof.lipumba aongea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWIBA WA KATANI, Apr 19, 2012.

 1. MWIBA WA KATANI

  MWIBA WA KATANI Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.Waheshimiwa waaandishi wa habari ,naomba kutumia fursa hii kuwajuza japo kwa muhtasari yale yaliyojiri wilayani Tandahimba mpaka kufikia hali ya uvunjifu wa amani. Mnamo tarehe 11/04/2012, Chama cha CUF kiliandaa maandamano makubwa ya amani yaliyokuwa na lengo la KUDAI MALIPO YA PILI YA KOROSHO. Wakulima walilipwa shilingi 850/- kwa kilo na kuhaidiwa kulipwa malipo ya pili ya shilingi 350/- kwa kilo. Pamoja na Chama Cha Ushirika cha Wilaya kuuza korosho hadi kufikia shilingi 2030/- kwa kilo, wakulima wa korosho hawajalipwa malipo ya pili.
  Maandamano ya amani yaliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara Mhe. Julius Mtatiro na kwa uwezo wa Mungu na namna tulivyokuwa tumejipanga vyema, Maandamano yalikwisha kwa salama na amani, pamoja na kuwepo kwa kauli za kisiasa na za kejeli za kukatisha tamaa zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Bi. Hasna Mwilima, ambaye ndiye aliyepokea maandamano yetu. Mkuu wa Wilaya alieleza kuwa yeye hahusiki na wakulima kutolipwa malipo ya pili ya korosho zao na anayeweza kufafanua suala hili ni Mkuu wa Mkoa.Baada ya maandamano haya, tulifanya mkutano mkubwa wa hadhara ambao pia uliisha salama na ulikuwa na mafanikio makubwa. Mnamo tarehe12/04/2012, baadhi ya wananchi waliweka vizuizi vya magogio katika barabara kuu ya Mtwara-Newala kwa lengo la kuishinikiza serikali iwalipe madai yao ya malipo ya pili ya korosho kwa kuweka mabango yenye ujumbe mbali mbali wa kudai malipo hayo. Katika tukio hili, Jeshi la Polisi liliamua Kutumia nguvu kubwa Ikiwemo matumizi ya SILAHA ZA MOTO na MABOMU YA MACHOZI kwa ajili ya Kuwatawanya raia waliokuwa wanadai malipo yao. Polisi waliwapiga raia Bila huruma hadi kupelekea baadhi ya wananchi kuumizwa vibaya, akiwemo mtoto mdogo wa umri wa miaka 13 ambaye alipigwa risasi ya moto na amelazwa katika hospitali ya wilaya Tandahimba. Hali hii ya upigaji mabomu Ilidumu kwa takribani siku mbili kabla ya uongozi wa Jeshi la Polisi kuamua kutafuta suluhu kwa kukutana na wazee na viongozi wa Serikali za Vijiji na katika mazungumzo yao, walikubaliana kwa pamoja kuwa vitendo Vya uvunjifu wa amani visitishwe haraka ili kuweza kuipa fursa Serikali Ishughulikie kero za wakulima Ikiwemo suala la madai yao Hali ya amani Ikiwa imerejea na watu wanaendelea na shuguli zao Kama kawaida wakisubiri Serikali ishughulikie suala lao. Mnamo tarehe 17/04/2012, Kwa mshangao mkubwa Ilipatikana taarifa kwamba Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tandahimba inaungua moto. Kwa kuwa ofisi hii ipo katikati ya soko kuu la biashara Tandahimba, ilibidi wafanyabiashara baada ya kupata taarifa hii, waanze kukimbilia eneo la tukio ili kusaidia zoezi la uokoaji Ili moto usiweze kuteketeza sehemu kubwa ya SOKO na kuwasababishia hasara Kubwa. Lakini katika hali Isiyotegemewa, Polisi waliwazuia wale wafanyabiashara kuzima moto ule na badala yake wakaanza kuwashushia kipigo . Kitendo hiki cha Polisi kuwazuia wananchi kusaidia uokoaji, kinajenga mashaka ya nani na kwa dhumuni gani alisababisha moto huo? Moto umeteketeza zaidi ya maduka 52 na bidhaa Zote zilizokuwemo ndani ya maduka hayo. Waheshimiwa waandishi wa habari jambo la kusikitisha zaidi ni Kwamba, tukio hili la kuchoma nyumba za wakazi na wafanyabiashara wa Tandahimba linaonekana kuwa linamsukumo mkubwa wa viongozi wa serikali wenye mlengo wa CCM Kwani maduka mengi yaliyochomwa moto ama ni ya wafuasi wa CUF au ni ya wafuasi wa CCM ambao katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, walikuwa wakimuunga mkono aliyekuwa mgombea ubunge Kwa tiketi ya CUF. Maduka ambayo si ya watu wa aina hiyo, Likiwemo la Mkuu wa Kituo Cha Polisi Tandahimba hayakuungua kabisa. Aidha kuna watu kadhaa ambao wameumia kwa kipigo wakiwa kwenye harakati za UOKOZI. Miongoni mwa watu hao ni pamoja na MOHAMEDI MACHEMBA, ABDALLAH ABDALLAH ambaye amepigwa pamoja na Gari yake Kuchomwa moto, na MBARAKA MTUHI ambaye amechomwa Kisu na singe ya bunduki na amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Tandahimba. Siku ya Jumamosi tarehe 21/04/2012 Mwenyekiti wa CUF Taifa atakwenda Tandahimba akifuaana na naibu katibu mkuu bara Mhe. Julius Mtatiro. Chama cha Wananchi CUF tunaitakata Serikali Ifanye Uchunguzi wa Kina Juu ya kadhia hii na ichukue hatua zinazostahiki ikiwepo kuwawajibisha viongozi wote wa Serikali ya Wilaya na wa Jeshi la Polisi ambao itabainika wamehusika katika kusababisha vurugu hizi zilizopelekea kuteketeza mali na vitu vyenye thamani ya zaidi ya mamia ya milioni ya fedha. Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ameshindwa kufanya kazi ya uongozi wa wilaya wa kuhakikisha anatoa majibu ya busara kwa wananchi na kufuatilia madai yao. Amekuwa kinara wa kusababisha haki za binadamu za wananchi kuvunjwa. Rais aache utaratibu wa kuteua wakuu wa wilaya wasiokuwa na uwezo wa uongozi kwa hisia za kirafiki tu. Mfumo wa kununua korosho kwa stakabadhi ghalani hauna manufa kwa wakulima na unasababisha wakulima kudhulumiwa na kuongezewa umaskini. Serikali itoe leseni kwa wafanya biashara wanunue korosho kwa ushindani ili mkulima apate bei inayopatikana katika soko la dunia. Imetolewa;
  Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
  Mwenyekiti wa CUF Taifa
  19 Aprili 2012
  SOURCE TOVUTI YA CUF.TANDAHIMBA.POLISI WATUMIA RISASI ZA MOTO,CUF YAINGILIA KATI
   
 2. k

  kubane Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna kila dalili nyie CUF mlichochochea ayo mavurugu, mi najiuliza kwanini baada tu ya hayo maandamano yenu mliyoyaita ya amani ndo vurugu zitokee.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hii ni khatari kubwa.
  Ahsantum Prof Ibrahim kwa taarifa yako.

  Tunawapa pole huko Tandahimba.
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hizi ndizo siasa tunazotaka, hakuna kubembeleza magamba!!

  Ila wangekuwa CDM, ungeleta ujuha wako wa UDINI. Heshimu PHD yako kwa kuzungumza ukweli.
   
 5. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF siku zote ni chama vurugu hata pasipo stahili. Wanaishauri serikali ipi wakati na wao ni gamba B .
  CCM A wanatekeleza yale waliyozoea kuyafanya dhuluma ,unyanyasaji dhidi ya wananchi na ufisadi.Hivyo CUF kamwambieni mume wenu CCM A dhuluma na unyonyaji sasa basi kupitia vikao vyenu vya ndani sio kufanya vurugu.

  My take;
  Kama ni kweli hiyo taarifa imeandikwa na Prof Lipumba basi atakuwa amebakia jina tu kuwa alikuwa nguli wa uchumi.Leo hii nchi za kiafrika zinaangalia jinsi gani ya kuelekea kwenye kuwapa wakulima ruzuku kama ulaya na marekani ambao walianza kutumia mfumo wa Warehouse Receipt System 100 yrs ago.Leo badala ya kuleta mfumo mbadala kama mchumi,unakuja kuleta hoja za kuwarudisha walanguzi!!.

  Hao vijana ambao ni wafuasi wa CUF ndio waliokuwa ma middlemen sasa wameondolewa kwenye mkt chain wanjifanya wao ni wakulima wanaleta fujo.Wakulima wametulia makwao hata siku moja sio waleta vurugu.Leo mkulima amelipwa 800Tsh/1kg malipo ya 1 kwenye mfumo, B4 mfumo alikuwa hapati zaidi ya 400Tsh/1kg ( Kwa maana ya malipo yote)
   
 6. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kazi kweli msilete mzaa katika maswalanyeti yanayo gusa maswala ya wananchi
   
 7. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu SINA JINAI...

  Watu wa Tandahimba ni watu tofauti sana.. Kwa sasa wako radhi wauze Korosho zao,basi tu wajue wameuza,iwe kwa faida au hasara..kuliko kuambiwa wakae wangoje,inakuja,wasubiri..

  Yaani ni watu ambao wanaweza wakafanya maamuzi,na hawarudi nyuma! Yaani si vigeugeu...

  Yaani chama tawala kuja kushinda Tandahimba.. Itachukua miongo mingi sana.. Na hii nimekupa kama mfano tu wa hawa jamaa walivyo. Wakichoka,wamechoka. Wakisema sasa basi,hiyo ujue hata uje na kitu gani,hawakuelewi..

  Kwa kifupi ni watu ambao si wa kuwaendea kwa pupa.. Na uwe mwangalifu na ahadi zako..
   
 8. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,683
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  chanzo cha vurugu ni majibu ya kejeli na dharau toka kwa mkuu wa wilaya aliyepokea maandamano! Ila vurugu zilitokea siku mbili baada ya maandamano!
   
 9. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du ila wewe nae kichwa maji watu wanakufa we unaleta.umagamba wako.MWACHE PROF.LIPUMBA APIGANIE WANANCHI KAMA WE NA MAGAMBA YENU MNAENDELEA KUUA WANANCHI MDA WENU UMWFIKA WA KUPOTEA
   
 10. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ccm wanataka wafanyweje ili waachie nchi
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mleta thrid anaitwa katani katani alishinda ubunge tandahimba kilaza Juma Njwayo kamchakachua.VP katani umepona mkono? HASNA MWILIMA WA HAPA ARUSHA..DC TANDAHIMBA HAZIPANDI NA HUYU BWANA WA 'chuki ubinafsi na fitna'
   
Loading...