Madai ya CHADEMA Kanda ya Pwani kuhusu Kero ya mabasi ya mwendokasi yamuibua Waziri

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani Baraka Mwago amezungumzia Kero kubwa ya Mabasi ya mwendokasi inayowakumba wakazi wa Dar es Salaam.

Katika Salaam zake za mwaka mpya kwa Wakazi wa Kanda ya Pwani kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini alisema magari ya mwendokasi yamekuwa hayasimami vituoni na hayachukui abiria kwa muda unaotakiwa hali inayosababisha abiria kujazana vituoni na watu kuchelewa kwenye shughuli za uzalishaji mali.

Katika kile kinachoonekana kujibu kero zilizoibuliwa na Chadema Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo amefanya ziara ya ghafla kwenye vituo vya mwendokasi na kuonya watendaji huku akiwataka kutatua haraka kero zilizoibuliwa na wananchi ikiwemo abiria kujazana vituoni na mabasi kutokusimama kwenye vituo vingi.

Chadema Kanda ya Pwani imejipambanua kama msemaji wa wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika kero mbalimbali zinazowahusu na kuonyesha njia mbadala ya kuzitatua.
IMG-20200103-WA0047.jpg
 
Haya ndio mambo tunategemea kuyaona kwa cdm. Ukweli ni kuwa cdm inasikilizwa na wananchi, inapaswa kulifahamu hilo na kuitumia hiyo kete yake vizuri.
 
Back
Top Bottom