Madai mapya ya Marekani: Iran inataka kumiliki akiba ya urani ya Venezuela

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,878
Madai mapya ya Marekani: Iran inataka kumiliki akiba ya urani ya Venezuela
Jun 12, 2019 07:26 UTC
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani jana Jumanne alitoa madai mapya akisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafanya juhudi za kumiliki urani ya Venezuela.
John Bolton amedai kuwa Venezuela ni nchi yenye akiba kubwa zaidi ya urani duniani na kwa sababu hiyo nchi hiyo imegeuzwa na kuwa mlengwa mkuu wa Iran. Bolton amezituhumu pia Russia, Cuba, China na Iran kuwa zimejiimarisha huko Venezuela na kwamba nchi hizo ni tishio kwa maslahi ya Marekani. Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais Donald Trump amedai kuwa madola ya nje yanafanya jitihada za kujipenyeza Venezuela na kwa hivyo kuna haja ya kuzungumziwa doktrini ya Monroe. Kabla ya haya pia, Bolton alizituhumu Iran, Russia, Cuba na China kuwa zinaingilia masuala ya ndani ya Venezuela.
Washington inalihesabu eneo la Amerika ya Latini kama eneo salama kwake la kuingilia masuala ya ndani ya eneo hilo kwa mujibu wa doktrini ya Monroe iliyowasilishwa mwaka 1823 Miladia na James Monroe, rais wa wakati huo wa Marekani. Katika miezi ya karibuni, Marekani ilikusudia kufanya mapinduzi Venezuela kwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Caracas.
Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido tarehe 23 Januari mwaka huu alijitangaza kuwa rais wa nchi hiyo kwa kuungwa mkono waziwazi na Marekani na waitifaki wake; hatua ambayo ilitajwa na serikali na wananchi wa Venezuela kuwa ni mapinduzi dhidi ya rais halali wa nchi hiyo Nicolaus Maduro. Aghalabu ya nchi zikiwemo Iran, Russia, China na Cuba pia zimelaani mienendo hiyo ya Marekani na kusisitizia ulazima wa kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala nchi na umoja wa ardhi ya Venezuela.
4bsi7ffc936bee1frpn_800C450.jpeg
 
View attachment 1125976
Lione mustachi wake kama fagio, pumbaaaaaavu.
 
Urusi INA maslahi mapana Venezuela, USA akileta choko choko patachimbika. Mpaka Sasa USA umeshindwa kumuweka Rais wao wamtakae Venezuela
Trump hana mpango wa kupigana vita yoyote ile katika utawala wake. Kuna vichwa kama Maddog aliviondoa mapema vile havina lugha vinaijua zaidi ya vita.
Alipomuondoa yule jamaa ndiyo nika conclude kuwa Trump hana mpango wa kupigana vita yoyote ile ila anachokifanya hivi sasa ni kumjaza ujunga Iran na wenzake. Russia ameshastukia huo ujinga na yeye kaamua ausome upya mchezo.
 
Back
Top Bottom