Inaguresheni
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 294
- 130
Zitto ana uwezo wa kuufanya research?Moja kasoro kubwa inayotumaliza Watanzania ni hii tabia ya wanasiasa kutudumuza kuwa kila kitu kifanywe ni (mwingine) na sio sisi wenyewe. Zitto is simply full of hot air. Yeye amefanya nini, amelima hata nusu eka ya mchikichiki? Anataka watu wa Kigoma WALETEWE WACHINA, WAARABAB, WAMERAKANI ETC kulima michikichiki? Kwanini asihamasiche watu wa Kigoma wakalima?
Mbegu zilizopo ni za asili na zina viwango duni. Research Institution za Tanzania ndio zilitakiwa ziandae Mbegu. Wizara ya kilimo iwajibike. Alafu ndio tumzodoe Zitto kwa kutolima hiyo robo eka. Mwalimu wangu wa uchumi A level aliwahi kutuambia Wafaransa wanakopa sera zilizofanyiwa tafiti chuo kikuu na wanazimodifai wanasongesha uchumi wao. 2014 Nilienda Uganda wamewaleta wataalamu kutoka Indonesia wamewawezesha wakulima wa michikichi meneja wa mradi akaniambia wanazalisha zaidi ya 75% inayotumika Uganda. Kampuni ya Bidco imeingia mikataba maalumu na serikali ya Uganda. Visiwa vilivyopo ziwa Victoria vyote vimegeuzwa mashamba. Kisiwa kimojawapo nilichotembelea kinaitwa Kalangala. Huyo meneja mradi aliniambia Mbona Tanzania hamlimi na amewahi kufanya kazi Tabora na anaijua kigoma? Tusipokuwa na taratibu wa kuwahoji Viongozi wetu na uwezo wa kuwawajibisha wanapofanya madudu tukakalia siasa na kuhoji mbona yeye hajalima. Je akilima ekari Mia zitatatua tatizo? Hii issu ni ya kitaifa sio ya Zitto na bila idara za serikali kuingiza fedha Zitto huwezi chochote hata angelima ekari 1000. Hivi hata bajeti ya kilimo ya mwaka huu umeisikia ilivyo ya aibu? Tujaribu walau kuiga Uganda, serikali imeingiza fedha na kushirikiana na wawekezaji sio kuwatisha.