Madagascar na Utawala - Kenya-Zimbabwe-Comoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madagascar na Utawala - Kenya-Zimbabwe-Comoro

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Mwiba, Mar 22, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tanzania opposed to Rajoelina leadership

  2009-03-21 12:03:14
  By Felister Peter


  Tanzania has condemned the forced resignation of Madagascar President Marc Ravalomanana and said it does not recognise the regime of his successor, Andry Rajoelina.
  ``Forcing a democratically elected head of state to resign by a mutinous faction of the military, at the instigation of a section of the population, is a serious setback for the cause of entrenching the spirit of democracy and good governance on the African continent,`` read the statement.

  _________________________________________

  Je Utawala wa Sultani CCM unawatisha wanajeshi wetu ,kuwa wasijaribu wala wasifikirie kuwaondoa madarakani ?

  Ujumbe kwa wanajeshi wa Tanzania ,hakuna wakati mzuri wa kufanya vitu kama wakati huu ,kama mnaiona namna hali ya nchi inavyoendeshwa basi nyinyi kama mmekula kiapo cha Mwalimu Nyerere hamtamuonea haya mvivu mzembe na mzururaji basi kusema kweli WaTz wamechoka na tabia iliyojitokeza baada ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ,tabia ambayo wananchi hawana wa kumtegemea zaidi ya wanajeshi ambao ,kila unamemsikia manung'uniko ya kuwalaani viongozi au Chama cha CCM ambacho wengi wa viongozi wake wameifanya nchi hii kuwa sehemu ya mtaji wao binafsi ,wananchi ambao walitegemea ujaji wa vyama vingi vya siasa kuwa mkombozi lakini bado Mtawala CCM anaendelea kuonyesha ubabe kwa kutumia sehemu ndogo ya vyombo vya dola kujiweka madarakani ,kwa kuiba kura kubadilisha matokeo na kutumia hazina ya nchi katika kuwanunulia na kuwadanganya wananchi walio masikini kwa kuwapa kofia na fulana ili kuununua utu wao ,udhaifu wa viongozi wa CCM katika kuwatumikia wananchi umepotea na walicho au wanachokifanya hivi sasa ni ubabe tu wakuwaburuza wananchi. Hakuna asieelewa namna wizi unaofanywa na viongozi wa serikali ni kitu tokea kilikuwa siri mpaka sasa ni mchana kweupe viongozi wa Chama kimoja serikali moja wanaogombania ulaji wanaonekana waziwazi kwenye vyombo vya habari ,hili si jambo la kulitazama na kulichekea ni aibu kubwa na si kwa wananchi walio wanyonge hata kwa Jeshi ambalo ni dhamana na mlinzi wa Nchi hii ,asionewe haya mtu , si mkubwa si mdogo viongozi wa Sultani CCM wamebadilika roho na hawana imani na mwananchi wa kawaida kila alie kwenye uongozi anatesa kivyake na hakuna wa kumgusa ,haya yanaonekana na yapo open kabisa.

  Isionekane kama nachochea hapana ,kwani kwa hapa tulipofikishwa ni sehemu ambayo kwa nchi za wengine ungelikwisha sikia matokeo ,na hasa hali hii iliyopo kama Raisi wetu Kikwete angekuwa muungwana wa kweli basi angekwishaivunja serikali na yeye mwenyewe kujiuzulu ,maana matatizo yaliopo kwenye vyombo vya serikali si madogo ,ukiangalia kuanzia ngazi za Polisi mpaka mawaziri ni vurugu mechi tupu,ukiangalia mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino si mambo madogo kwa kiwango yalichofikia ,ukiangalia mauaji ya Pemba yaliofanywa na polisi kwa kuiweka CCM madarakani si mambo ya kutazamwa na kuambiwa kuwa wamejitakia wenyewe ,ni uwazi wa kuonyesha nchi inakaliwa kimabavu na watu wachache ,watu ambao wameshindwa kutazama na kuulinda utu wa mtu mwengine.

  Angalia Burundi ,ni juzi tu wameuliwa albinoes haikupita wiki wauaji wamekamatwa kwa mpigo na kesi zao zipo katika hatua ya kufikishwa mahakamani ,nchi ambayo ilitawaliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka ,leo hii wameonyesha kuwa uwezo wa kuendesha nchi wanao na usalama wao uko macho ,sisi tusiokuwa na matatizo ya kivita ,nchi yenye wananchi watiifu kabisa ,vyombo vyetu vinashindwa kuzuia zaidi ya kuonekana wakiwa wamebeba mitutu kuzuia maandamano ya kisiasa ,na polisi wanajigamba eti wamefanikiwa kuzuia maandamano ,jambo ambalo limeruhusiwa kikatiba ,naweza kusema na kumpa Mbowe asante sana kwa kuwakachia polisi kuvunja mkutano wako hilo ni jambo la kupigiwa mfano na hapo inaonyesha jinsi uvumilivu unapoelekea mwisho ,heko Mbowe na wananchi wa Kilimanjaro kwani polisi si kweli kuwa wapo kwa ajili ya usalama wa wananchi bali wapo kwa ajili ya usalama wa Wafuasi wa Sultani CCM peke yao.

  Hapa watu wanakamatwa na viungo na kila kitu lakini utaona kesi inazungulushwa na haijulikani itakavyoishia ,wala husikii mhusika ameweza kuwataja waliomtuma na mganga aliewaelekeza shughuli hiyo ,ni aibu na mambo mengine yanaonekana wazi wazi kuwa wakubwa waliomo serikalini nao wamo maana kama hawamo basi ,wangekuwa wakisisitiza kuwepo na uwazi katika wale wanaohusika lakini huenda jina la Chama likaharibika ,mauaji ya Arusha ingawa tume imeundwa lakini tume hiyo haikubaliki kwani imefungasha wahusika ambao ni polisi ,haki katika nchi hii ipo wapi ? wachunguzi huru wapo wapi ? Imekuwa ni mtindo kuundwa tume na halafu kuzungulushana au kuzungulusha matokeo kesi ya Zombe hadi leo inakwenda na mauzauza ya wengine kufa na wengine kuumwa ,ni katika kulindana au sio ,yule mgonjwa ameambiwa kuwa amekula sumu ,nini kimefanywa kuchunguza sumu hiyo alitiliwa wapi ? Vinasa sauti katika waliotiliwa wabunge kesi imeishia wapi ? Utaambiwa uchunguzi unaendelea ,ni kulindana.

  Sasa huko madagascar wana yao na yaliyotokea wanayajua wao zaidi na sababu iliyopelekea kuyafanya wao wenyewe ndio wanaijua .

  Hapa hatukusikia watu kuikanusha serikali ya Mwai Kibaki wala ya Mkuu Robert Magube ,maana hao wawili wote ni wababe ,na wanautambua ushindi wa wafuasi wa Sultani CCM unavyopatikana,makele ya Utawala wa Sultani CCM kwa wengine isiwe vitisho kwa wanaotaka maendeleo Tanzania ,hamtahesabika kuwa mumeshinda ushaguzi wakati nia na madhumuni ni kuendeleza matakwa binafsi ya kulindana ,hilo sidhani kama litakuwa jambo la kuendelea kukubalika na WaTanzania walio wengi.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Demokrasia ni kauli na uamuzi wa umma. Kama umma umeamua kuwa umemchoka Ravalomanana na hawana njia nyingine yeyote ya kumwondoa basi wamefanya maandamano kuikosesha serikali nafasi ya ku "function." That is democracy. The will of the people. Sio lazima uwe uchaguzi wa kura za kuibiwa! Nawapongeza ndugu zangu wa Madagascar.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa Hapa Tz moyo wa kufanya hayo upo ? Ikiwa mtawala anatumia washawasha na risasi za moto ? WaPemba wameweza kwa kiasi fulani katika jaribio lao la mwanzo ,je Tanganyika au Tanzania kwa ujumla kwa hali hii ya wizi wa mchana tutaweza fahamu kuwa Sultani CCM anategemea risasi ,maana kila siku zinavyokwenda wanachama au wafuasi wake wa daraja la chini wanamkimbia ,hivyo atabakiwa na risasi tupu.
   
 4. Kiumbemzito

  Kiumbemzito Member

  #4
  Mar 22, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hallo mkuu!
  Pamoja na maandishi yako mareefu kuhusu SULTAN CCM sijaona ni mantiki gani uliyotumia kuona hao wnajeshi walio amua kumuondoa kiongozi aliyechaguliwa na wengi yani kidemokrasia na kumuweka mpiga disko wao wa zamani DJ hainiingii akilini hata kidogo. kwanza katiba yetu hapa haishabikii upuuzi kama huo.
  na bahati jeshi letu la sasa lina wasomi wengi ambao hawawezi kufanya mambo kama hayo tuna Mabrigedia DR.Prof...... wengi tu kwa hiyo hayo ya madagascar ni yale enzi za 'Yesu angesema acha wafu wazike wafu wenzao ' hapa kwetu wameenda shule bwana.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kama huyo rais wa Madagascar aliweza kuondolewa na mpiga disco basi alikuwa amesha "loose touch" na raia wa kawaida.
   
 6. Kiumbemzito

  Kiumbemzito Member

  #6
  Mar 22, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Lakini hapa kwetu si unaona wagombea wote wa urais wa upizani wameombwa na wapigakura wao , wanachama wao wakagombee ubunge kwenye majimbo yao, ina maana tiari raisi wanae anae wafaa na chama kinacho wafaa! kwa sababu asilimia 82% za JK zilipigwa na watu wote wa CCM na Wa vyama vingine tiari Mboe anataka kwenda kugombea ubunge , Mrema wamemuomba achane na uraisi kabisa sasa huyo SULTAN ATANG'OKA KWELI?
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  MODS tafadhali angalieni kama misingi na malengo ya JF yanalingana na post za aina hii na iwapo mtaona kuwa hailingani tafadhali chukueni hatua muafaka.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tz raha yake kwa sasa JK katoa uhuru wa kutoa mawazo/maoni!

  Saa ingine naona kama tuaabuse huu uhuru!

  Kila uhuru ni lazima uwe na mipaka kiasi flani!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  What'w wrong with this post? Yaliyotokea Madagascar ni siri?
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Thats for MDS to decide.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Najua wafuasi wa Sultani CCM lazima wataichukia hii posti lakini ,siwashangai kuendelea kuwepo kwa Mheshimiwa Kikwete wengine ndio hapo wanapopataka maana kula kwa vijiko na umma sasa akitokea akitokea mlala hoi huko kambini na kuwakurupusha na kuwapeleka mchakamchaka lazima wafuasi wa CCM maji wataita mma,hakuna anaetaka au anaetamani hali ya kupinduana lakini mkae mkijua ,huko yanakotokea na kushinda mwanzo na senene senene zake pamoja na sababu ni haya mambo ya wizi usiochukuliwa sheria,wizi wa kulindana ,wache tu ndio wanaojua kutumia umeme na maji safi,wachache tu ndio wanaomiliki magari ya kifahari ,wachache tu ndio wanaofaidika na hazina ya nchi hii ,unafikiri mwisho wake ni kitu gani ?
  Ni lazima tuseme ili walioko madarakani waamke na kuona wanayoyafanya sio haki ,kwa kuwa wao tu wamemiliki vyombo vya mitutu ,wanapowania uongozi fikira zao ni zipi ?
  wanagombea ubunge na kufika mpaka kwenye uwaziri na uraisi ,hivi ni nini lengo la wao kuwa viongozi ,je ni kila anepata uongozi ndio aamue kivyakevyake ,kila aneukwaa uongozi ndio nafasi ya kupokea rushwa na kuliliza Taifa.
  Nini dhamana ya uongozi ,uko wapi uwajibikaji ? Au uwajibikaji ni kupotea kwa mafaili ya kesi ,au uwajibikaji mafaili kupandishwa na kushushwa ,je watu waliokubali dhamana hawajui kazi zao ,ni kupatiana nafasi kwa sababu ni mjomba na shangazi ?

  Viongozi wanaongoza nchi yenye watu zaidi ya milioni 36 ,je viongozi hawa wanatumia nafasi hizo kucheza na maisha ya mamilioni ya watu hawa ,sasa fikiria Nchi ina mawaziri walikuwa kiasi ya sitini wakapunguzwa na kupataganywa na kubakia kama ze arubaini ,sasa viongozi au utititri wa viongozi hawa nini faida yao kwa Taifa hili au ni kuonekana tu kuwa mimi sasa ni mkbwa na kutotumia dhamana aliopewa kutimiza wajibu wake wa uongozi ,siku hizi kazi hazifanyiki zaidi ya malumabano kila kukicha linazuka jipya,maadili ya uongozi hayafuatwi ,daraja za uongozi hazithaminiwi tena,mipaka ya uongozi haipo ni vurugu mechi ,uongozi na mipango inaonekana kwenye kushughulikia vyama vya upinzani ama huko mipango na mikakati ni mizuri sana ,Viongozi wa Taifa wanasikika wazi wakisema kwanza Chama halafu kinacho fuatia hakimalizwi kikajulikana ni kipi ,maana ya maslahi ya Chama kwanza ni kulazimisha haki kumezwa ,pale haki inapoonekana kupindishwa kwa kuwa wapindishaji ni wa Chama tawala hivyo viongozi wa Taifa inabidi wapindishe sheria ili kuwalinda wahusika ,au si kweli ? Kiongozi atachaguliwa kwa jinsi anavyoliendesha Taifa na sivyo anavyokiendesha Chama.

  Jinsi wananchi walivyoweka matumaini kwa Kikwete basi Chama chochote kile ambacho angeamua kugombea basi naamini wananchi wangempa ushindi na vyama vingine vilikuwa tayari kumpokea na kumweka kama mgombea wao ,matarajio ambayo leo hii hayapo si kwa kuwa Kikwete ni mbaya katika uongozi lakini Chama alicho si Chama kinachojali maslahi ya wananchi na sera zake hazieleweki ni za kubabaisha na za tamaa mbele mauti nyuma ,huo ndio ukweli ,so far tunaposema ni wakati wa jeshi kuingilia kati haina maana kuuwa au kuuwana ,ni kuilazimisha CCM kuondoka madarakani na halafu sheria za kweli zichukue mkondo wake ,maana yanayofanywa na kutokea ndani ya CCM hayaleti fikira nzuri kwa siku zijazo zaidi ni kumkatisha tamaa mwananchi ,kuna yule Waziri juzi alisema kuwa Tanzania inategemea ...Tanzania accented its nuclear ambitions yesterday, saying plans were underway to start uranium extraction ready for the country to revert to one of the world`s highly rated renewable energies. Mwaka 2011 huyu wakati huo hatakuwa Waziri anajenga matumaini kwa serikali gani anaipangia serikali gani ?Wakati huo yeye atakuwa hayupo kwa maana hiyo anajaribu kuikwepa hali iliyopo na kuibebesha serikali nyingine ,ni kwa nini ndani ya miaka hii ya serikali aliyomo hafanyi kweli na tukaona ? Kama huku sio kusema uongo ni kitu gani ,mikakati 2011 .

  Tazama anapozidi kujichanganya ..." ``It needs a lot of consideration; but I think the government can sell the uranium without processing it,`` he said.

  I Think..... huyu jamaa anajua maana yake ,hana uhakika wa anachokisema hivyo statement yake yote ni ya kutiliwa shaka ,Waziri huyo anarapu tu .

  Ngeleja said in case it was found that Tanzania had sufficient uranium for electricity generation, the government would embark on it, observing international laws on atomic energy use.

  Hivi atueleze huu uchunguzi wa Uranium ulianza lini hapa Tanzania ikawa hadi leo hapajajulika ukweli ,what about Iran Connection with CCM ambapo imedaiwa walitoa dau ili kukamilisha wizi wa uchaguzi na macho yakiwa kupata gawio la uranium.

  Waziri huyu kila akikurupuka anawazuga watu hii ni mara ya pili anagusia suala hili la kujenga matumaini ,sasa anawapa WaTz baada ya miaka mitatu kwa ufupi amesema 2011sijui alikosea hesabu.

  So far nchi inahitaji mabadiliko makubwa ya uongozi ,uongozi wa CCM ndio kama tunavyouona huyu anapanga hili mwengine anakuja na lake na kupangua kila kitu.
  Lipumba amewambia na kuwashauri kuwa lazima watu wakutane wapange cha kufanya kwa maana ameshaona kuwa Nchi imepoteza uongozi katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ,kuna hitaji hatua muhimu za kuchukuliwa watu Milioni 36 sio wa kuwafanyia mchezo wa kitoto na kuwadanganyakila siku ,matatizo yanakuwa ,yanazidi yanazaliana ,ameona tuwahi kabla haijakuwa too late ,ni mtu mwenye uzoefu wa matatizo ya kimataifa ,namshauri Kikwete asione aibu wala haya akubali kuitisha kikao cha pamoja ili kuinusuru nchi hii na balaa linalotokana na Black hole ya uongozi mbovu ndani ya CCM.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nasoma NYT Book review wikiendi hii.

  [​IMG]

  Katika kitabu chake kipya "War Guns and Votes" Mwandishi Paul Collier, ambaye awali aliandika kitabu kilichosifiwa sana "The Bottom Billion" anavipa umuhimu mkubwa sana vionjo vingi vya demokrasia kama uhuru wa kujieleza na uhuru wa mihimili ya serikali kusigishana kuliko hata anavyotoa umuhimu kwa uchaguzi.

  Muandishi anaonekana hata kuyakubali mapinduzi ya kijeshi kama kweli uongozi wa kisiasa unakuwa wa kifisadi.

  Muandishi ana pointi muhimu, tatizo moja kubwa tulilonalo ni kuwaachia wanasiasa waamue mambo kwa niaba yetu. Kadiri wananchi tutakavyowaachia wanasiasa watuamulie mambo yetu ndivyo wanasiasa watakavyozidi kutumia dhamana hii kujikwapulia wanachotaka bila kujali wananchi. Mapinduzi ya kweli inabidi sio tu yatoke kwa wananchi, bali pia yaendelee kutazamwa na kulelewa na wananchi.

  Kuchukulia mfano wa Madagascar, Ravalomana alikuwa meya wa Antananarivo, akawa anabeba sauti ya watu kuhusu ufisadi wa Didier Ratsiraka aliyekuwa rais wakati huo, akamtoa kwa kuwapa watu ahadi nyingi za mabadiliko. Lakini inaonekana kuwa mpinzani na kumtoa rais si kazi ngumu kama kutekeleza ahadi na maadili yanayowaweka wanamapinduzi hawa madarakani.

  Zaidi ya kusema hayo, inafaa pia tuangalie ubaya wa mapinduzi yasiyofuata kanuni za kidemokrasia kwa njia ya uchaguzi.Tunaweza kuweka misingi ya kukubali mapinduzi yasiyofuata uchaguzi kwa kusema chaguzi zinachafuliwa - na hivyo hazina maana - na kuacha mlango kwa kila mbabe wa kijeshi na mwenye kipaji cha kuwachota watu kwa kauli, aweze kuchukua uongozi.Kwa maneno mengine, ingawa ni kazi ngumu, ni vizuri tukaangalia zaidi jinsi ya kuimarisha uthabiti wa chaguzi zetu kuliko kushabikia mapinduzi yasiyofuata kanuni za demokrasia ya uchaguzi.

  Ningependa kuona wananchi wa Madagascar wanaendelea kuwashurutisha viongozi wao wawe wawazi, kwa maana bila uwazi ufisadi haukawii. Tayari kuna habari kuwa Rajoelina aliwahonga wanajeshi wengi ili wam-support, kuna mpaka wengine wanasema kuwa sababu ya kweli iliyomtoa Ravalomana kwenye urais si ufisadi bali ni kanuni zake za kupunguza matumizi jeshini na kuongeza matumizi katika huduma za jamii.

  Kwa hiyo kwa sasa tuunge mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na watu (au yanayoweza kuwa ya kifisadi ambayo yanaripotiwa kuongozwa na watu) au tuendelee na kanuni yetu ya kutotambua serikali zilizoingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi? Tuna criteria gani inayoweza kutuongoza kwamba kukiwa na hiki na hiki, hata kama kuna mapinduzi ya kijeshi tutayakubali? Au tunayakataa mapinduzi ya kijeshi yote, hata kama yanazuia mauaji ya halaiki?

  Kwa sasa, hatuna habari zaidi na inakuwa sawia kulaani mapinduzi ya kijeshi angalau kwa kuonyesha kanuni, na yeyote anayesema kuwa mapinduzi haya yameongozwa na watu atakuwa na kazi ya kutujhakikishia demokrasia inajengeka Madagascar kabla hatujaitambua serikali hii.Demokrasia hii haiishii tu kwenye uchaguzi - ambao hata kina Mwai Kibaki na Robert Mugabe wameshinda kinyemela- bali itaendelea pote kwenye taasisi za kijamii zinazohitaji kujengwa katika misingi ya demokrasia, kuanzia uhuru wa kujieleza, uhuru wa misingi mitatu ya dola kusigishana kimizani pamoja na kuondoa utawala usiochaguliwa haraka iwezekanavyo.
   
  Last edited: Mar 23, 2009
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Besides, because news organizations in these countries are weak and objective information scarce, citizens probably don't even know how well or how badly their leaders are performing.
   
 14. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwiba salam,
  Mkuu itakuwa bora tena bora sana tukiwa makini katika kuyaangalia mambo haya ya siasa na uongozi, viongozi na wananchi waongozwao.Tusichagawe wala kuwa na ghadhabu tunapotoa maoni yetu. Kuna msemo wa wahenga usemao KAMA HUJUI KUFA LIANGALIE KABURI kwa mada uliyoweka jamvini ni wazi pamoja na kusihi kwako yaelekea ungekuwa Jeshini na Bega limechafuka kidogo saa hizi mkuu ungeshafunga kazi na jamaa waliokuwa CCM wanapiga Kwata!!!!! na Makaburi ya mapinduzi yapo PAKISTANI NIGERIA NA jirani SOMALIA. Kwa hiyo mkuu MWIBA kama MWIMBO unaoimba ni mzuri SHIKA BANGO UTANGULIE WAFUASI WATAKUFUATA.
   
Loading...