Madafu yaendelea kuporomoka, leo yaanza kunusa 1,500 kwa US$1 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madafu yaendelea kuporomoka, leo yaanza kunusa 1,500 kwa US$1

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ntemi Kazwile, May 19, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Je hii maana yake nini?

  Kwa wiki kadhaa sasa shiling ya Tanzania imeendelea kupoteza thamani ikilinganishwa na dollar ya Marekani kwa speed ambayo si ya kawaida. Mpaka mwishoni mwa mwaka jana US$1 ilikuwa inacheza kwenye Tshs 1,300 lakini leo hii US$1 inacheza kwenye Tshs 1,460 -1,500. Hii si habari njema sana kwa uchumi wetu kwa sababu kila kitu kitapanda ukizingatia kuwa vitu vingi vinaagizwa nje ya nchi kwa kutumia (mafuta, bidhaa nyingi za maisha ya kila siku).

  Je hii ni dalili nyingine ya kushindwa kwa serikali ya Kikwete?
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dalili mbaya sana hii ndo maana fuel ni very expensive sasa.Tanzania zaidi ya uijuavyo, uchumi poromoka mbaya.Sielewi mkulu atasemaje kuhusu hili au bado maisha bora kwa kila mtanzania?
   
 3. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni hatari sana hii,
  Na cha ajabu,ndani ya mwezi huu tu...ipanda zaidi ya30-50 shillings..hii ina maana gani jamani wanauchumi?
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kama umekuwa ukifuatilia miaka ya nyuma, hii ni hali ya kawaida kabisa kwani waagizaji/wawekezaji husita kuagiza kwa kuhofia pengine yanaweza kutokea machafuko nao wakapata hasara. Baada ya election hali inarudi kama kawaida
   
 5. m

  mapambano JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Ahsante baba kwa mitakwimu na mi-graph hiyo --- picha husema zaidi
   
 7. b

  bnhai JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuelekea kwenye uchaguzi lkn hali imekuwa mbaya mno. Nadhani umefika wakati sasa ikafanyika intervention but with cautious. Kwanini?
  Kwasababu kpimo chetu siku zoote kimekuwa ni US dollar lakini ukweli ni kwamba dollar imeregain chap chap hivi karibuni against almost all major currencies kwahiyo TSh haiwezi kufurukuta.
  Lakini zipo hatua tunaweza kutumia km kuongeza dollar kwenye mzunguko (interventaion-forex quantitative easing) na kuzuia matumizi ya sarafu za kigeni nchini na huku tukijitahidi kuzalisha kwa wingi ili kupunguza kuagiza vitu nje.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kama export of goods imeshuka ambayo ni chanzo cha foreign currency specifically USD, while imports of goods which is the source for spending USD abroad, ni wazi kutakuwa na Increase in demand for USD locally ultimately will lead into high price of dollar (high exchange rate).

  Another source huenda kuna movement of our forex into foreign banks kwa njia za kifisadi na kuacha ombwe, ila pia inawezekana BOT wamezuia ku-release USD in the locala market kwa sababu wanazozijua wao. Huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo tutarajie low foreign investments flowing in Tanzania and sometime even movement of capital outside due to the fear of election chaos. Unajua ni hatari sana kuuweka uchumi mikononi mwa wageni ambao wakati wa amani wanachuma na kutunyonya, inapokaribia wakati wa uchaguzi wanahofia vurugu na kukimbiza mitaji yao nje.

  Ila hii yote inasababishwa na sera za CCM za kutopunguza politcal risks kwa Investors kwa kuonesha kuwa watatenda haki katika uchaguzi na hivyo possibility of political chaos will be low. Matendo kama kukatalia baadhi ya vyama usajili wa kudumu, kupiga danadana kesi ya mgombea binafsi, kutokuwepo tume huru ya uchaguzi; hivi vyote ni viashiria vya kutokuwepo free and fair election which might lead into political violence afterwards.
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu tuko pamoja, lakini kuna ukweli mwingine ambao inawezekana umefichika na haujauzungumzia hapo kwenye maelezo yako. Ukiangalia uchumi wa dunia kwa ujumla dola ya marekani kwa mwezi huu imepata nguvu za ajabu. Ukweli huu unaweza kuuona kwenye exchange rate ya dola dhidi ya Euro. Euro imepoteza nguvu kwa dola na leo BBC nimesikia wanasema bei za bidhaa kule marekani na hasa mafuta vimeshuka bei wakati bei ilibaki bila kubadilika for the past 13 months. Hivyo kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola kumechangiwa na mambo mengi zaidi ya tunavyofikiria.

  Tiba
   
 10. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wazuie matumizi ya dollar ndani ya nchi! Period

  TRA wanacharge in terms of dollars, Hotels almost zote zinataka dollar, wafanyabiashara kariakoo wanatrade kwa dollar. Unategemea nn kwenye situations kama hizi! Na tusitegemee kwamba dollar itashuka, tukumbuke wafadhili wataacha kutusaidia kwenye budget ya mwaka ujao kwa kiwango tulicho tarajia, so tutakuwa na scarcity ya poreign currencies.

  Government izuie matumizi ya dollar ndani ya nchi, pamoja na ubadilishaji holela wa shilling kwenda dollar! Tujifunze kutoka South Africa.
   
 11. d

  damn JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu, Notice in red, kwa kweli inashangaza TZ ilivyoachia mambo kiholela hasa kwenye exchage of currency, nchi zilizoendelea huwezi kukuta vioski vya kubadili fedha kama ilivyo TZ.

  huu umbayuwayu sijui utaisha lini
   
Loading...