Mada yenye ukakasi: Majini yanayoishi nasi hapa duniani yenye umbo la kibinadamu (Demons/fallen angels in human form)

Hii ni kweli na mimi imenitokea ni muhanga wa hilo.
Kila nikioa ndoa zinavunjika,nikimpa demu ujauzito unaharibika miaka inaenda tu.
Mwanzoni sikujua tatizo ila baadae wakaanza kujitokeza kunipa ishara ndotoni
Nina maswali kwako mkuu,twende taratibu

Umesema baadae wakaanza kujitokeza kukupa ishara,ni kina Nani hao?
 
Hapa watu huwa wanachanganya,anachofanya Jini hapa ni kumchezea mtu na kumfanya kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi au kuota ndoto akifanya mapenzi au kukosa hamu,lakini hakuna ndoa kati ya jini na mwanadamu.
Ndoa ipo mkuu ila sio ya halali.
Tena akiamua mnazaa kabisa watoto ila wewe unakuwa huna access nao hao watoto kwa sababu wanaishi kwenye ulimwengu wa majini.
 
Hili nalisia kwako. Naomba unieleze linawezekana vipi hili.

Mwanadamu aliye umbwa kwa udongo anawezaje kuzaliana na Jini aliye umbwa kwa moto ?
 
Jini ana uwezo wa kujigeuza katika umbile analotaka mkuu.
Hili jambo nimelifuatilia kiundani sana sio kwa kusoma majarida.
Ni jambo limenitokea mwenyewe
 
Kuna umbile ambalo jini hawezi kujibadilisha kwalo. Lakini kujibadilisha katika umbile fulani halimfanyi Huyo jini akawa kwenye silika hiyo. Jini amepewa uwezo wakuflow katoka mwili wa mwanadamu kama damu inavyo flow. Na jini katika mwili wa mwanadamu kuna sehemu anazotumia kuingia na kukaa pia.

Ila kuhusu kuingiliana kimwili hili halipo zaidi ya kufanya vitimbi vya kumfanya mtu asipende jambo fulani hili lipo,ila kuzaa na kuingiliana kimwili hili halipo.
 
Hapa watu huwa wanachanganya,anachofanya Jini hapa ni kumchezea mtu na kumfanya kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi au kuota ndoto akifanya mapenzi au kukosa hamu,lakini hakuna ndoa kati ya jini na mwanadamu.
Umesema anachofanya jini ni 'kumchezea' mtu na kumfanya kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi au kuota ndoto..me hiyo Hali ya kumchezea mtu ambayo hujaisema kumchezeaje si ndy hiyo ambayo kuna mdau mbu wa dengue anaisema kwamba ndy hiyo ya kufanya mapenzi na binadamu? Hebu fafanua hapo kwenye 'kumchezea' mkuu
 
Kuna umbile ambalo jini hawezi kujibadilisha kwalo. Lakini kujibadilisha katika umbile fulani halimfanyi Huyo jini akawa kwenye silika hiyo. Jini amepewa uwezo wakuflow katoka mwili wa mwanadamu kama damu inavyo flow. Na jini katika mwili wa mwanadamu kuna sehemu anazotumia kuingia na kukaa pia.

Ila kuhusu kuingiliana kimwili hili halipo zaidi ya kufanya vitimbi vya kumfanya mtu asipende jambo fulani hili lipo,ila kuzaa na kuingiliana kimwili hili halipo.
Ingekuwa hivyo basi jini mahaba asingekuwa na wivu kwa binadamu.
Fuatilia vizuri mkuu,usitosheke na hiyo concept ndogo uliyojifunza.
Ingia hata google uliza utajifunza zaidi mkuu.
 
Mimi ni muislamu,nilitembea kwa wale watu wa vitabu na mitishamba sijui niwaiteje ili uwaelewe vizuri
Nimekuelewa mkuuPole s.Kupitia maelezo yako kuna kitu nimejifunza kikubwa sn hasa hii koment

Kwamba ulitembea Kwa watu wa vitabu na watu wa miti shamba lkn hata sasa hujafanikiwa..mkuu Mshana Jr nashukuru Kwa ule ushauri
 
Ingekuwa hivyo basi jini mahaba asingekuwa na wivu kwa binadamu.
Fuatilia vizuri mkuu,usitosheke na hiyo concept ndogo uliyojifunza.
Ingia hata google uliza utajifunza zaidi mkuu.
Kuwa na wivu hakumaanishi kwamba kuna maingiliano,yeye anakuwa na wivu ili kutimiza kazi yake,na si kwamba kuna muingiliano wa kimaumbile katika jimai (Tendo la ndoa).

Hata ukirejea katika historia ya uchawi,huwezi kuutenganisha Uchawi na Majini,na uchawi wa aina ya pili unahusisha kufarakanisha baina ya mke na mme,siyo kwamba mfarakano unatokea kwa wao majini kujiweka fizikali,la hasha,bali kuwashawishi na kuweka vikwazo,na hiki ndicho hufanyika pia katika suala la kumzuia mtu na matamanio au kuchukia kuolewa au kuoa na mfani wa hayo.
 
Umesema anachofanya jini ni 'kumchezea' mtu na kumfanya kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi au kuota ndoto..me hiyo Hali ya kumchezea mtu ambayo hujaisema kumchezeaje si ndy hiyo ambayo kuna mdau mbu wa dengue anaisema kwamba ndy hiyo ya kufanya mapenzi na binadamu? Hebu fafanua hapo kwenye 'kumchezea' mkuu
Naposema kumchezea ni kumfanyia jambo la uongo na kumfanya mtu asiwe na hali ya kutaka kuoa au kuolewa. Majini wamepewa uwezo huo. Kuna watu unakuta wanachukia kufanya tendo la ndoa au wengine wanakosa hamu kabisa,hii ni miongoni mwa dalili za kufanyiwa vitimbi na majini,lakini hakuna tendo la ndoa baina ya jini na mwanadamu. Japo kuwa ukisoma vitabu vya wanazuoni wa kale husema ya kuwa ndoa kati ya jini na mwanadamu ipo,lakini kuna mambo wanashindwa kuyaweka kazi sababu ukweli ni kinyume chake.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom