Mada yenye ukakasi: Majini yanayoishi nasi hapa duniani yenye umbo la kibinadamu (Demons/fallen angels in human form)

nzaghamba

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
747
1,000
Amini unachoamini, ila ukweli ni kuwa majini walio na umbo la kibinadamu hapa duniani wapo, na tunaishi nao Aisha j
hiyo inaitwa luga gongana,anachokikataa mwenzako hapo ni kuwa jini ni kiumbe tofauti na Malaika ni kiumbe tofauti...Malaika hawaasi na wanafanya walichoamrishwa na Muumba wao kwamba ibilisi ni uzao wa majini walioasi na sio uzao wa Malaika(Malaika wameumbwa kutii amri ya Mungu pekee hawana choice ya kuasi)
 

Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,858
2,000
Kwa mara ya kwanza ilikuwa Jana ulipoleta uzi humu kuhusu Jack Chacha wa Corner Bar (Ambiance)
Kuwa yeye ni Jini
na Leo hapa unakataa kuwa hauwezi kuwataja!
Kifupi JF umejiunga hata wiki haujamaliza ila nahisi una mambo mengi sana!
Unachokihubiri na unachokitenda ni vitu viwili tofauti sana!
Binafsi nimekujibu tu ila sikutaka hata nikujibu coz ni mtu usiyeishi maneno yako!
Labda basi niamini kuwa wewe mwenyewe ndiye Jini au?
Hizi story za majini umekazana nazo sana Boss kulikoni?
Pole sana mkuu..

Nikufahahamishe tu kuwa mimi si mleta

mada ..soma vizuri usikurupuke ..


Sijajiunga juzi humu na hata hili jina

natumia kwa vile tu nilishindwa kurejesha

lile la mwanzo.nilisahau pass yake!


Hata hivyo nina miaka..mimi nimechangia
hoja tu kama wewe na wengine

mlivyochangia ...

Halafu ni vizuri ukaongelea mada zaidi

kuliko watu..umekwenda chaka mkuu..
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,401
2,000
Sasa wewe si utuambie vizuri wewe na majini wenzio mlivyo ili tuelewe?
Iko hivi mkuu,majini wana ulimwengu wao wa kijini ambao sisi binadamu hatuuoni ila mara moja moja huwa wanaamua kuja katika ulimwengu wetu japo huwezi kuwaona kirahisi wao wanatuona ila kuna muda hujitokeza na kujionesha katika maumbo mbalimbali ya kibinadamu au wanyama kwa muda mfupi na kwa lengo fulani.
Sasa hakuna kitu cha kusema eti jini awe classmate wako au mpangaji mwenzio miaka na miaka uwe unamuona kila siku japo wana uwezo wa kuishi katika nyumba yako ukapishana nao kila siku na usiwaone.
Mimi katika nyumba yangu ninayokaa kuna kipindi walikuwa wananisumbua sana usiku nikilala wanafungua milango lakini nikitoka kucheki sioni mtu na nakuta milango ya vyumbani iko wazi na muda mwingine walikuwa wanatembea juu ya bati usiku unasikia nyayo zinatembea au wanadondosha vitu vizito kama tofali lakini ukitoka nje kucheki hakuna kitu,muda mwingine unasikia bomba la maji limefunguliwa nje maji yanamwagika lakini ukienda nje kucheki ni pakavu hakuna maji yaliyomwagika.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,401
2,000
Naam.

Elimu ya dini.

Aam kupitia matukio ya watu na kusoma matukio hayo vitabuni.

Unaposema ni mchezo tu ulitakiwa kumalizia mchezo una chezwa na nani ?

Naweza kuthibitisha ya kuwa hivyo ni vitimbi vya majini kama wanavyo fanya vitimbi hivyo katika ndoto.
Mkuu kama unasema umejifunza hayo kupitia elimu ya dini kajifunze zaidi elimu ni bahari usitosheke na hiyo elimu uliyonayo.
Ingia google uliza maswali mbalimbali ya kuhusu majini utajibiwa na maulamaa mbalimbali wa kimataifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom